na Tony Alamo
Karibu na Yeriko katika Israeli ipo sehemu iitwayo Sodoma na Gomora.1 Kama unaweza kuiona, utafahamu bila shaka kwamba MUNGU ni MUNGU mwenye kuhukumu!2 Unaweza kuchukua vipande vya njano vya salfa, ambavyo huungua unapoviwasha. Ni mahali pa kutisha ambapo hujawahi kuona. Milima yaonekana kana kwamba MUNGU alivikata vilele vya milima katika vipande vikubwa-vikubwa, kisha, kwa ngumi YAKE kubwa, akaponda kila kitu na kusawazisha, akazika katika chumvi, salfa (kiberiti) na moto. Beba nyumbani kipande cha salfa (kiberiti) kama ukumbusho. Chukua kipande kingine ukiweke kwenye sanduku la kupigia kura wakati umma unaposema, “Hebu tupige kura tuone kama ndoa ya jinsia moja ni sawa.” Kamwe usithubutu kusema pamoja na halaiki ya watu kwamba NENO LA MUNGU si la kweli! Hatuwezi kujua sawa, baya, jema, au ovu bila NENO LA MUNGU!3
Eneo lote hili lina joto kuliko sehemu nyingine yoyote katika Nchi Takatifu. Pia ni sehemu ambayo haina uhai. Kuna milima mikubwa ya chumvi karibu yake.4 Haijalishi ni kiasi gani mto Yordani hutiririka na kumwaga maji yake baridi katika Bahari ya Chumvi, maji ya bahari ya Chumvi ni chumvi sana, na kamwe hayawezi kuendeleza uhai, wala kutoa samaki. Kuanguka kwa milima kumelifanya eneo hilo kuwa ukiwa sana, na kuna kreta kubwa katika ardhi karibu na hoteli. Eneo hili huitwa Engedi, likimaanisha “jicho la kondoo.” Zipo hoteli tatu kubwa huko, na nyingine ndogo kumi, zote zikiwa na mabwawa ya kuogelea. Kreta kubwa na maharibiko halisi vilikuwa kwenye barabara ya nyuma inayotoka Engedi kwenda Beer-sheba. Unaposimama juu kwenye pembe za kreta, unaweza kuona vizuri zaidi uharibifu, eneo la milima iliyoporomoka ya Sodoma na Gomora. Nyuma ya kreta, kuna milima iliyofunikwa na mawingu na ukungu juu yake. Ukimya na ukiwa humfanya mtu kuwa na hofu. Haiwezekani kabisa kuona chini kwenye kreta, ni pana sana.
Kuna kreta ngapi kubwa katika ardhi – ardhi iliyopasuka mashimo makubwa – ambayo imesababisha uharibifu na maziko ya Sodoma na Gomora? Yeriko ni lazima ihusishwe pia, kwa sababu Sodoma ni wilaya tu ndani ya Yeriko. Unaposhuka na barabara ya mlimani kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, masikio yako huzibuka, kama vile unatua na ndege. Yeriko ipo chini sana ya usawa wa bahari, sehemu iliyo chini kuliko sehemu zote za nchi. Ni kwa sababu MUNGU aliponda na kusawazisha eneo lote. Aliifanya sehemu hii kuwa chini kuliko sehemu zote za ardhi kwa sababu ya dhambi walizotenda.5
Yeriko, isipokuwa mji, karibia yote ni tupu, na isiyo na uhai, kwani ni nchi iliyolaaniwa. Inatia huzuni. Mazingira ni mabaya mno. Haijalishi ni mara ngapi watu wanajaribu kuiendeleza nchi, kwa namna fulani kuleta maisha na furaha ndani yake; lakini nchi hiyo inawashinda na haiendelei. Unaweza kuona mapango na nyumba ambazo zimeharibiwa. Watu waishio humo ni wachache, na wengi wao ni wachungaji. Mfumo wao wa maisha ni mbaya sana na wa kikatili, kama ardhi yao ilivyo katili, na nyuso zao huonekana ngumu kama mwamba.
Watu hadi leo hii, huchukua mawe ya salfa, kiberiti, ambavyo MUNGU alimwaga juu ya eneo hilo. Huchukua kumbukumbu na kuwasha mawe ya salfa kwa kiberiti. Wezi wa makaburi (Majambazi) na wanaakiolojia hutembelea maeneo haya mara kwa mara kuangalia makaburi na majeneza. Majambazi huchimba usiku, wakisaka miili, mitungi, vikombe, vito, na samani ambavyo wanaweza kuviuza kabla ya wanaakiolojia kuvipata. Wanajaribu pia kuchimba mapango yaliyoharibiwa na nyumba kutoka kwenye miamba, kiberiti na salfa.
Yeyote atakayetazama ukubwa wa uharibifu katika eneo hili hatakuwa na shaka kwamba ni uharibifu alioufanya MUNGU kulihadhibu eneo hili, kwani nchi yote ya Israeli ni ya kijani na iliyostawi, isipokuwa sehemu ya Sodoma na vijiji vinavyoizunguka. Hivi punde MUNGU ataleta uharibifu WAKE katika dunia hii tena na juu ya ulimwengu wote.6
Nchini Marekani, hatujawahi kuona tetemeko la ardhi kubwa zaidi ya 9.2 kwa kiwango cha skeli za Richter. Ni rahisi kuona kwamba, kama uharibifu alioufanya MUNGU katika Sodoma na Gomora ungepimwa leo kwa skeli ya Ritcher, ungesomeka 25.0 au zaidi. Hii ni bila hata ya kuzingatia mvua ya moto na kiberiti juu ya watu kwa sababu ya vitendo viovu vya ngono, kama ushoga na uzinzi.7
Eneo lote hili linastahili kuwa ushuhuda wa MUNGU kwa watu wote, hasa wale wapotovu wanaofanya ushoga na usagaji. Baada ya kuona yote haya, utatambua kwamba MUNGU hafanyi mzaha. Humaanisha kile Asemacho.8 Ni nyakati za mwisho, hivyo usifanye mzaha hali kadhalika unaposali sala hii kwa MUNGU:
BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11
Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13
BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.
Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).
Mahali ilipo Sodoma na Gomora
Mwanzo 19:27-28 inasema, “Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za BWANA, naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru.”
Katika miaka ya 1980, mgunduzi wa kiakiolojia wa maeneo ya Kibiblia, Ron Wyatt, alibaini maono wa ajabu wa “maumbo” alipokuwa akipita katika pwani ya Bahari ya Chumvi. Kwake yalionekana kama kuta za mji na majengo, ila katika rangi nyeupe. Kwa miaka mingi hakufanya lolote kuhusu kile alichokiona, lakini mnamo 1989, Ron aligundua jambo ambalo lilimshawishi kwamba maumbo haya yenye rangi nyeupe hayakutokana na mabadiliko ya kijiolojia.
Zaidi ya Matabaka ya Kijiolojia
Ron aliona barabara ambayo vitu vyeupe vilikuwa vimekatiza na sehemu ya ndani ikiwa na vitu vilivyoonekana katika mpangilio wa tabaka ambazo zilionyesha dhahiri kwamba haya yalikuwa ni zaidi ya matabaka ya kijiolojia.
Katika kutafuta kwenye Biblia, dalili kulingana na maandiko yao, Ron na mkewe Mary Nell walipata marejeo andiko ambayo yanataja miji minne inayounda sehemu ya mipaka ya Wakanaani:
“Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha” (Mwanzo 10:19).
“Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha” (Mwanzo 10:19).
Itakuwa ni jambo la ajabu kwa Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu kila mmoja kuorodheshwa kama alama za mpaka kama yote ingekuwa katika eneo moja, upande wa kusini mwa Bahari ya Chumvi. Ni mantiki kwa miji iyo kuwa katika umbali kutoka mmoja hadi mwingine ili kujumuisha kila mmoja wa miji hiyo kama alama za mpaka.
Sehemu ya maeneo aliyoona Ron, kwa hakika, yalikuwa yametengana kwa umbali usiopungua maili hamsini au zaidi. Mji mmojawapo ulikuwa kaskazini mwa Yeriko, ambao kulingana na maandiko inaashiria Seboimu utakuwa kaskazini mwa Bahari ya Chumvi.
“Naye Sauli, na mwanawe Yonathani, na watu walikuwapo pamoja nao, wakakaa huko Geba ya Benyamini; lakini Wafilisti wakatua katika Mikmashi. Nao watekaji wa nyara wakatua katika marago ya hao Wafilisti, vikosi vitatu; kikosi kimoja kikageukia njia iendayo Ofra, mpaka nchi ya Shauli; na kikosi kingine kikageukia njia iendayo Beth-horoni; na kikosi kingine kikageukia njia ya mpakani ielekeayo bonde la Seboimu upande wa nyika” (1 Samweli 13:16-18).
Baadaye 1989, Ron na Mary Nell Wyatt walitembelea eneo hilo chini kidogo ya Masada na wakachukua sampuli ya vitu vyeupe ambavyo vilivunjika haraka mikononi mwao na kusambaratika katika chembe mithili ya poda ya talkum. Wakati huo, Mary Nell aliona moja ya kapsuli ya kiberiti ikiwa imegandamana na kipande cha majivu yaliyosindiliwa; hata hivyo, hakuna hitimisho lililopatikana wakati huo, kwamba kilikuwa ni kitu gani.
Mnamo Oktoba 1990, Ron Wyatt na Richard Rives walirudi katika eneo hilo. Walipokuwa wakilichunguza eneo hilo lililoko chini ya Masada, waligundua kwamba mvua ilikuwa imenyesha. Walipokuwa wakishangaa mahali hapo, Richard aliona kitu mfano wa chumba kilicho wazi au pango kwa mbali na walipokaribia pango walikutana na rundo kubwa la majivu ambalo lilikuwa limeanguka muda huo kutoka juu – labda kwa sababu ya mvua iliyokuwa imenyesha muda huo. Ron aliposimama kutazama, aliona gololi nyingi za njano ndani ya majivu yaliyosambaratika, zote zikiwa zimezungukwa na ukoko mwekundu-mweusi mithili ya pete. Alipojaribu kutoa moja, alitambua ilikuwa ni salfa. Kwa uchunguzi wa karibu, sasa akiwa anajua nini anatafuta, ilifahamika kwamba vyote vilivyokuwa ndani ya mabaki ya majivu vilikuwa ni vitu vya mviringo kama mpira vikiwa vimezungukwa na salfa (kiberiti).
Baada ya uvumbuzi wa kiberiti, utafiti wa kiakiolojia wa Wyatt ulianza kuchunguza kama kiberiti walichoona kilipatikana katika mfumo huu sehemu nyingine yoyote. Ron na Mary Nell Wyatt pamoja na Richard Rives walikwenda kwenye Taasisi ya Smithsonia, mjini Washington D.C. na kuchunguza salfa yao katika namna tofauti, hakuna iliyokuwa ya mviringo yenye poda za salfa. Na kuongeza, hakuna iliyokuwa imezungukwa na utando. Ombi liliidhinishwa na Taasisi ya Smithsonia kuchunguza salfa zilizokuwa na mwonekano tofauti. Salfa zilikusanywa kutoka sehemu mbalimbali duniani, zenye zaidi ya vielelezo hamsini. Hakuna hata moja kati ya hizo zilizoonyesha tabia sawa na salfa ya kiberiti iliyopatikana karibu na “miji ya Bonde.”
Ron Wyatt hakuwa mtu wa kwanza kugundua kiberiti karibu na Bahari ya Chumvi. Wakati William Albright na Melvin Kyle walipotoka kuiona miji ya Sodoma na Gomoara mnamo 1924, wao pia, waliona vipande vya kiberiti kusini mwa Bahari ya Chumvi.
“…sehemu ambayo kiberiti kilinyesha itaonyesha kiberiti. Naam, inaonyesha; tuliokota salfa halisi, katika vipande vikubwa kama ncha ya dole gumba langu. Imechanganyika na mchanga wa milima magharibi mwa bahari, na sasa imesambaa katika mwambao wa bahari hata upande wa mashariki wa bahari, kama maili nne au tano kutoka kwenye pembe yenye tabaka. Kwa kiasi Fulani imetawanyika mbali na kwa mapana juu ya bonde hili.” (Ugunduzi wa Sodoma na Dk. Melvin Kyle, 1928, uk. 52-53)
Wala Melvin Kyle hakuwa wa kwanza kuona mabaki ya majivu. Kumbukumbu nyingine ya miji hii inatoka kwa Josephus katika kitabu chake cha Nne, Wars of the Jews, (Vita ya Wayahudi), Sura ya VIII:
“Sasa nchi hii imeteketezwa kwa namna ya kuhuzunisha, na hakuna anayetamani kuikaa;…ilikuwa nchi ya kale yenye furaha sana, kwa matunda iliyozaa na utajiri wa miji yake, ingawa yote sasa imeteketezwa. Inatokana na ukengeufu wa wakaazi wake, ulichomwa kwa radi; Kutokana na madhara hayo bado yamo mabaki ya moto ule wa Mungu; na athari (au vivuli) vya miji mitano bado huonekana...”
“Sasa nchi hii imeteketezwa kwa namna ya kuhuzunisha, na hakuna anayetamani kuikaa;…ilikuwa nchi ya kale yenye furaha sana, kwa matunda iliyozaa na utajiri wa miji yake, ingawa yote sasa imeteketezwa. Inatokana na ukengeufu wa wakaazi wake, ulichomwa kwa radi; Kutokana na madhara hayo bado yamo mabaki ya moto ule wa Mungu; na athari (au vivuli) vya miji mitano bado huonekana...”
Maelezo ya Josephus yanaeleza vizuri kabisa kile kinachoweza kuonekana katika sehemu hizi za majivu:
“...imeteketezwa yote.”
“...imeteketezwa yote.”
Maelezo ya uharibifu wa Sodoma, Gomora, na “Mabonde yote” havikuwa hadithi za kale. Lilikuwa tukio la kihistoria ambalo lilitokea hasa kama maelezo ya Kibiblia yalivyobainisha.
http://www.wyattmuseum.com/cities-of-the-plain.htm
http://www.wyattmuseum.com/cities-of-the-plain.htm
Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:
Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide
P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078
Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686 • Faksi: (661) 252-4362
Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.
Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.
Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.
Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.
Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo
Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.
Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.
MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)
USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.
Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:
© Hatimiliki Aprili 2015 Haki zote zimehifadhiwa, Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo ® Imesajiliwa Aprili 2015
SWAHILI—VOLUME 21200—SODOM AND GOMORRAH
SWAHILI—VOLUME 21200—SODOM AND GOMORRAH
footnotes:
2. Mwa. sura. 6-7, Hes. 11:1, Kum. 4:24, 10:17, 32: 4, 15-16, 19-26, 35:43, Zab. 2:1-5, 12, 7:11-12, 11: 5-6, 21:8-9, Isa. 30:1-3, 30, 33, 66: 15-16, 24, Yer. 7:20, 10:10, 21:11-14, Omb. 4:11, Nah. 1:2-8, Mat. 25:31-46, 2 Kor. 5:10-11, Ebr. 10:30-31, 2 Pet. 2:4-9, Yud. 7, Ufu. 14:9-11, 20:11-15 return
3. Kut. 20:1-7, Kum. 5:1-21, Yos. 1:8, Zab. 119:9, 104-105, 130, Mit. 6:23, Mal. 4:4, Yoh. 5:24, 8:31-32, 12:48, 15:3, 2 Tim. 3:15-17, Yak. 1:21-25, 2 Pet. 1:19 return
6. Isa. 13:3-13, 24:1-21, 34:1-10, Eze. 22:25-31, 24:6-14, sura 38, Yoe. 1:13-15, Zef. 3:8, Mal. 4:1, Mat. 24:3-7, 21-22, 29-34, Lk. 17:24-30, 2 Thes. 1:7-10, 2 Pet. 3:3-12, Ufu. 6:15-17, 8:7-13, 9:1-19, 11:18, 16:1-11, 17-21, 19:11-21 return
7. Mwa. 19:4-13, Law. 18:20, 22, 20:13, Kum. 22:5, 23:17-18, Amu. 19:22-28, 1 Fal. 14:22-24, Rum. 1:18, 24-32, 1 Kor. 6:9-10, 18, 10:8, 2 Kor. 12:21, Gal. 5:19-21, Efe. 5:3-6, Kol. 3:5-7, 1 Thes. 4:3, 1 Tim. 1:9-10, Ebr. 13:4, Yud. 7, Ufu. 2:21, 9:21, 22:15return
8. Hes. 23:19, 1 Sam. 15:29, Zab. 119:89, Mit. 19:21, Muh. 3:14, Isa. 14:24, 40:8, Yer. 4:28, Eze. 24:14, Dan. 4:35, Mat. 5:17-18 return
Prayer footnotes:
1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return
2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return
3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return
4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return
5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return
6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return
7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return
8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return
9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return
10. Heb. 11:6 return
11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return
12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return
13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return
No comments:
Post a Comment