Friday, December 7, 2018

NDOA YA WAKE WENGI NI HALALI?

Image may contain: text
NDOA YA WAKE WENGI NI HALALI?
Kwa muda fulani, Mungu aliruhusu mwanamume awe na wake wengi. (Mwanzo 4:19; 16:1-4; 29:18–29) Lakini Mungu hakuanzisha mpango wa mwanamume kuwa na wake wengi. Alimpa Adamu mke mmoja tu.
Yesu Kristo alikazia mpango aliokuwa ameanzisha awali wa mwanamume kuwa na mke mmoja. (Yohana 8:28) Yesu alipoulizwa kuhusu ndoa, alisema hivi: “Yeye aliyewaumba hao kutoka mwanzo aliwafanya mwanamume na mwanamke na kusema, ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.”—Mathayo 19:4, 5.
Kwenye 1 Wafalme 11:1-3, kwa nini Suleiman alikuwa na wake 700 na Masuria 300, kinyume cha amri ya Mungu ya kwenye Kumbukumbu la Torati 17:17?
Kumbukumbu 17:17 inasema mfalme asiwe na wake wengi, na kwa kitendo hicho, Suleiman alifanya dhambi. Kuoa wake ilikuwa ni njia ya kuimarisha ushirikiano na falme nyingine, lakini pia ilikuwa ni makosa kutokumtii Mungu. 1 Wafalme 11:1-4 inasema kuwa Suleiman alifanya dhambi kwa kuoa hawa wake wageni, na kuugeuzia moyo wake kuwa mbali na Mungu.
Hard Sayings of the Bible uk.229 inalitumia jambo hili kwa njia ya kupendeza sana. Ingawa Suleiman angeweza kuweka viwango vya juu kama mfano, alianza kujiona kama hana haja ya kuzuiliwa na Mungu kwa njia hii. Leo hii kama kiongozi wa kikristo anajiona kuwa hayumo kwenye mipaka ambayo Mungu ameiweka kwa Wakristo wa kawaida, kiongozi huyu atakuwa kwenye shida kubwa sana ya kiroho. Kwenye Kurani, hakuna mwanaume anayeruhusiwa kuwa na zaidi ya wake wanne, isipokuwa Muhammad tu, ambaye alitokea kuwa na wake karibu 15 baada ya Khadija, na Masuria wawili.
Zaidi ya hayo, Muhammad na Waislam wengine walikuwa na wasichana mateka na watumwa, na Kurani inawaruhusu Waislam kufanya tendo la ndoa na wanawake ambao wanawamiliki kwa nguvu ya mikono yao. (Sura 4:24; 23:5-6; 70:29-30; 33:50,52 Abu Dawud juzuu ya 2 na.2150 uk.577)
Tabia hii ya Muhammad na Waislam kuoa wake wengi inavunja Amri ya kwenye Kumbukumbu la Torati 17 aya 17.
Katika Agano Jipya, 1 Timotheo 3:2, 12 na Tito 1:6 zinasungumzia "mume wa mke mmoja" katika orodha ya sifa za uongozi wa kiroho.
" Wakati sifa hizi ni mahsusi kwa ajili ya nafasi za uongozi wa kiroho, wanapaswa tumika sawia kwa Wakristo wote. Je, si Wakristo wote hawaswi kuwa "zaidi ya aibu ... kiasi, nidhamu, heshima, ukarimu, na uwezo wa kufundisha, si mlevi, wala mgomvi bali awe mpole, apendaye, si mpenda fedha" (1 Timotheo 3:2 -4)? Kama tumeitwa kuwa watakatifu (1 Petro 1:16), na kama viwango hivi ni vitakatifu kwa wazee na mashemasi, basi ni takatifu kwa wote.
Baadaye, mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu aliongozwa na Roho ya Mungu kuandika hivi: “Kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 7:2) Pia, Biblia inasema kwamba katika kutaniko la Kikristo ni lazima mwanamume aliyefunga ndoa na ambaye ana majukumu ya pekee awe “mume wa mke mmoja.”—1 Timotheo 3:2, 12.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW