Friday, December 7, 2018

JE, MUHAMMAD NI MTUME NA NABII WA UONGO AU WA KWELI?

Image may contain: 1 person, text


Ndugu msomaji,
Mara nyingi Waislam wamekuwa wakisema kuwa, eti, Yesu alitabiri kuja kwa Muhammad, pale alipo sema kuhusu Roho wa Kweli, la hasha.
Nabii ni mtu gani?
Nabii ni mtu aliyeteuliwa rasmi kwa vigezo vya Kiungu ili kuleta ujumbe wa Mungu kwa wanadamu, kwa maneno mengine nabii ni msemaji wa siri za Mungu.
Nabii: Ni mtu ambaye ni msemaji wa Mungu (a mouthpiece of God) .Husimama kati ya Mungu na binadamu, mwenye jukumu la kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu. Nabii anapokuwa msemaji wa Mungu, huvuviwa na Roho wa Mungu, bila ujumbe wake kuwa na makosa. Nabii hujizuia kabisa utashi wake, nafsi yake, na mawazo yake, anapokuwa anatoa ujumbe wa Kinabii toka kwa Mungu. Wakati mwingine Mungu mwenyewe hutia maneno yake vinywani mwao (Kum 18:18, Yer 1:9). Nabii ni mtumishi wa Mungu (Zekaria 1:6) na mjumbe wa Mungu 2 Nyak 36:15).
Ni kweli kuwa Yesu alitabiri kuja kwa manabii, lakini kamwe hakusema lolote kuhusu utume wa Muhammad zaidi ya kukiri kuwa watu wenye sifa kama za Muhammad ni Mitume na Manabii wa Uongo.
Miongoni mwa wanadamu wanaoitwa nabii na mtume, ni mtu aitwaye Muhammad s.a.w ibn Abdullah, ibn Abdu Mutallib, ambaye ni mtume na nabii katika dini ya Kiislamu.
Pengine wewe msomaji wa somo hili unaweza kushangaa ni kwa vipi sisi ambao si Waislamu bali Wakristo tuanze kuhoji habari za Muhammad s.a.w mtume wa Waislamu? Jibu lake ni kwamba kitabu cha Qur’an kinachotumiwa na Waislamu kimetutaja sisi Wakristo mara 62 kikitutaka kuupokea, kuuamini na hatimaye kuufuata ujumbe wa Muhammad s.a.w kwa madai ya kuwa yeye ni nabii na mtume wa mwisho hata kwetu Wakristo, aliyetumwa na Mungu.
YESU ATABIRI KUHUSU MTUME WA UONGO AMBAYE NI MUHAMMAD
Tahadhari ya Bwana Yesu: Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani alituonya kuhusu kuwatambua manabii na mitume wa uongo kabla Muhammad hajazaliwa (amezaliwa 570 B.K), wala kabla Uislamu haujaanzishwa na Muhammad mwaka 610 B.K, wala kabla ya kuwepo kitabu kinachoitwa Qur’an. Tunayasoma maonyo hayo ya Bwana Yesu katika
Mathayo 7:15-16 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali, mtawatambua kwa matunda yao”.
Mathayo 24:11-13 “Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi na kwasababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka”.
Yesu katika Ufunuo alisema kuwa watakuja Manabii na Mitume wa Uongo.
Ufunuo 2:2 Nayajua matendo yako na taabu yako, subira yako, na kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume nao sio, ukawaona kuwa waongo.
Je, Muhammad ni nabii wa Mungu?
Je, Muhammad anasifa za nabii wa Mungu?
Hebu endelea na somo hapa chini:
JINSI YA KUMFAHAMU NABII WA UONGO:
Kwa hivyo Muhammad ni miongoni mwa hao Mitume ambao ni waongo, ambao sisi kama Wakristo yatupasa kuutambua uwepo wao hapa Duniani, kwani tumeshapewa angalizo la kuwatambua hawa wanaojiita Mitume na Manabii, hali ya kuwa ni waongo
1 Yohana 4:1-3
1 Wapenzi msiamni kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu: kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani. 2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; KILA ROHO IKIRIYO KWAMBA YESU KRISTO AMEKUJA KATIKA MWILI, YATOKANA NA MUNGU, 3 Na Kila roho isiyomkiri Yesu, haitokani na Mungu. Na HII NDIO ROHO YA MPINGA KRISTO ambayo mliskia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Vigezo hivi tulivyopewa na Biblia Takatifu kuwajua manabii na mitume wa uongo ni muhimu sana tukavichunguza katika maisha ya wale wanaoitwa nabii au mtume
Kila nabii na mtume ambaye yeye hakubali kuwa Kristo alikuja katika mwili, kwa maana kuwa Mungu alidhihirishwa katika mwili, hiyo roho yaani huyo nabii si ambaye anatokana na Mungu, huyo ni Nabii anaetokana na shetani, kwa mujibu ya maandiko Matakatifu, Kristo alidhirishwa katika mwili.
1 Timotheo 3:16 Na Bila shaka siri ya utauwa ni kuu, Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na Malaika, akahubiriwa katika mataifa. akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu,
SASA KAMA MNATAKA KUAMINI KUWA KWELI Muhammad ni nabii na mtume wa uongo, waulizeni wafuasi wake,
SWALI LA KUPIMA UNABII WA MUHAMMAD:
Je! Kwa mujibu wa uislamu, Wanakubali kuwa Mungu alikuja kwa njia ya mwili wa kibinadamu na kuonekana?
Wakikubali, basi tambueni kuwa Muhammad ni mtume wa kweli, na wakikataa basi mjue kuwa Muhammad ni nabii na mtume wa Uongo.
SIFA ZA NABII WA KWELI:
Nabii wa kweli hupata ufunuo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu:- 2Petro 1:20-21.” Mkijua neno hili kwanza,ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,wakiongozwa na Roho Mtakatifu”.
LAKINI MUHAMMAD YEYE ALIPATA UNABII KWA NJIA HII, SOMA
Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
Je, wapi katika Injili au Taurat au Zaburi tunasoma kuwa Manabii na Mitume katika Biblia walipata kwa njia ya homa na kukiri kuchezewa na mashetani kama Muhammad wa kwenye Quran?
1 Petro1:10-11 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi na wakati wa namna gani ulioonywa NA ROHO WA KRISTO ALIYEKUWA NDANI YAO ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaokuwako baada ya hayo…..” (maneno ya msisitizo kwa herufi kubwa ni ya mwandishi)
Ufunuo 19:10 “Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndiyo roho ya unabii”
Biblia Takatifu imetuonya kuwachunguza mitume na manabii. Katika kitabu cha Ufunuo 2:1-2 “ Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao siyo ukawaona kuwa waongo”
Kwa mujibu wa aya hizi Muhammad s.a.w hastahili kuitwa nabii na mtume wa Mungu wa Kweli, bali anaangukia katika kundi la manabii na mitume wa uongo.
Mungu awabarikisana, na tuendelee kujifunza kweli, na kweli itatuweka huru.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
For Max Shimba Ministries Org.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW