Saturday, November 24, 2018

MUHAMMAD ALIVUNJA AMRI KUMI ZA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

No automatic alt text available.

Amri kumi ni sheria kumi katika Bibilia ambazo Mungu aliwapa taifa la Israeli muda mfupi baada ya kutoka Misri. Amri kumi hasa ni ufupisho wa amri 613 ambazo ziko katika sheria ya Agano La Kale. Amri za kwanza nne zahusika na uhusiano na Mungu.

MUHAMMAD ALIVUNJA AMRI YA KWANZA: 

“Usiwe na Mungu mwingine ila mimi.” Amri hii inapinga kuabudu miungu mingine ila tu Mungu wa kweli. miungu mingine yote ni ya uongo.

KWENYE Surat Al Ankabut 46. Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.

Kwenye hiyo aya hapo juu, Muhammad anadai kuwa Mungu wa Wakristo, Wayahudi na Waislam ni mmoja.

Je, Yehova Mungu wa Wakristo ndio Allah wa Quran?

Lipo wapi Jina la Yehova ambalo ni Yahuh kwa Kiarabu kwenye Quran ili tukubaliane nae?

Mungu mwenyewe alisema: “Watajua kwamba jina langu ni Yehova.” (Yeremia 16:21)

Sasa, wote tunafahamu kuwa Biblia ilikuja miaka 650 kabla ya Quran na kwenye hiyo Biblia Mungu alisema kuwa yeye jina lake ni "MIMI NIKO", "YEHOVA" n.k. LAKINI CHA AJABU, Allah HAKUSEMA KUWA YEYE NI "MIMI NIKO" AU "YEHOVA" kwenye hayo majina yake 99.

Je, Allah ni nani huyu, maana teyari anapinga na YEHOVA wa kwenye Yeremia 16 aya 21 na AMEKATAA kuyatumia hayo majina ya Mungu wa kwenye Biblia?

Zaidi ya hapo, wapi Mungu anasema kwenye Taurat kuwa jina lake ni Allah?

Wapi Mungu anasema kwenye Zaburi kuwa Jina lake ni Allah?

Wapi Mungu anasema kwenye Injili kuwa Jina lake ni Allah?

Haya ni maswali rahisi sana kwa Waislam na hayahitaji jazba katika kuyajibu zaidi ya wao watuletee aya kutoka Taurat au Zaburi au Injili kuwa Mungu anasema kuwa yeye jina lake ni Allah.

Lakini katika kufanya utafiti nimegundua kwamba Allah si Mungu wa kweli bali ni Shetani kwamujibu wa Qruani Surat Muhammad aya ya 15. inasema hivi “mfano wa pepo aliyowaandalia waja wake Mwenyezi Mungu iko hivi, ndani yake kuna mito ya maziwa na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywaji. humo watapata kuburudishwa kwa matunda ya kila namna na samahani kutoka kwa mola wao.”

Lakini ukisoma Qruani hiyo hiyo Sura ya 5 aya ya 90, inasema hivi: “Enyi mlioamini bila shaka ulevi na kamari na kuombwa yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni uchafu na ni kazi ya shetani.” 

Sasa rafiki yangu kwa mujbu wa aya hizi hebu fikiria, aya ya kwanza imesema Allah katika pepo yake kuna mito ya ulevi, lakini Qruani hiyo hiyo imesema ulevi ni kazi ya shetani, kama aya zenyewe ndizo hizi hoja yangu inakuja hapa: 

Yeye Allah kama siye shetani amepata wapi ulevi hali yakuwa ulevi ni wa shetani? 

Lakini Biblia imesemaje kuhusu ulevi: Walevi na wachawi na wazinzi hawataurithi ufalme wa mbinguni. Mungu anasema katika Isaya Ole wao waamkao asubuhi na kufuata ulevi.

Mpendwa kuwa macho hizi ni nyakati mbaya za Mpinga Kristo.

USIKOSE SEHEMU YA PILI 

Shalom,

Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW