Monday, October 29, 2018

BIBLIA YENYE VITABU VYA DEUTEROKANONI NI IPI?

Image may contain: one or more people



VITABU VYA APOKRIFA

(Apocrypha – Hidden)

Apokrifa humanisha iliyofichika, ni maandiko yaliyokuwa yamefichika kwa maana ya kwamba hayakujulikana.

Neno Apocrypha linatokana na neno la kiyunani apokruphos ambalo ni muungano wa maneno mawil apo—mbali ya- na kruptolkruptos—iliyofichwa.

Vitabu vya apokrifa ni vitabu ambavyo Wakatoliki, na WaOthodox wa Urusi huvikubari kama maandiko makuu yanayofaa kufundishia imani.

Vitabu vya apokrifa ni maandiko ambayo yalichapishwa baada ya kipindi cha Nabii Malaki hadi kufikia mwisho wa Karne ya kwanza ya Ukristo.

Baadhi ya Vitabu vya apokrifa tutakavyo viangalia ni

1 Wamakabayo

2 Wamakabayo

Judithi

Tobiti

Wimbo wa Sulemani

Esdras

Baruch

Sira

Ombi la Manase

Hekima ya Sulemani

Walaka wa Yermia

Kutokana na Ushahidi tunaoupata katika agano jipya ni wazi kwamba Wayahudi walikuwa na Kitabu (Vitabu) ambavyo waliamini kuwa ni Sahihi na vinafaa kufundishia—CANON. Vitabu hivyo viliitwa Musa(Sheria), Manabii, na Zaburi au Torati na Manabii au Musa na Manabii. Tazama Math 5:17-18, 7:12, 11:13, 22:40. Luka 16:16-19, 24:27,44 Yohaa 1:45. Mdo 13:15, 24: 14. 28:23 na Rumi 3:2

Mwanahistoria Flavius Josephus (Karne ya Kwanza) akiandika katika mwaka wa 90 alitaja vitabu 24 vilivyokusanya historia ya Wayahudi ya kila ambacho kiliaminika kama Uvuvio.

Vitabu 5 vilindikwa na Musa, Vitabu 13 viliandikwa kati ya Musa na Mfalme Atashasta (Artaxerxes) wa Waajemi. Vitabu 4 vilikuwa vimejumuisha mashairi (vitabu vya Mashairi) na Nyimbo, Zaburi, Methali, Muhubiri, Maombolezo (Against Apion 1:38-40)

Kisha Josephus akaendelea kusema “Ni kweli kwamba Historia yetu imekuwa ikiandikwa toka wakati wa Atashasta, lakini maandiko hayo hayajachukuliwa kuwa ni maandiko sawa na maandiko ya kale ya Mababu zetu. Hii ni kwa sababu, hakuna mfuatano wa Manabii toka wakati huo.

Na ni kwa kiasi gani tumekuwa na msimamo mkali na kuaenze maandiko hayo na kuchunga asije mtu akaongeza katika maandiko—Toka wakati huo, haijawahi kutokea mtu kuongeza maandiko hayo au kupunguza au kufanya badiriko lolote ndani yake.” (Against Apion 1:38-40)

Hivyo Jusephus alishikilia msimamo wa Wayahudi wote kwamba maandiko yote yaliyoandikwa baada ya Utawala wa Atashasta (yaani baada ya Wayahudi kutoka utumwani Babeli) kuwa hayana Uvuvio kwa kuwa hakukuwa na Unbii katika kipindi hicho katika Israel.

Utagundua kuwa Sababu kubwa anayoitoa Josephus ya Kukataa maandiko hayo ni kwasabubu hakukuwa na unabii. Vitabu vyote nilivyovitaja hapo juu viliandikwa katika kipindi hicho.

Vitabu vilivyoorodheshwa na Josephus ndivyo hivyo ambavyo huunda jumla ya Vitabu 66 vilivyomo katika biblia inayokubaliwa na Waprotestant wote duniani. Sababu iliyowafanya waprotestant kuvikataa vitabu hivyo ni Sababu hiyo hiyo iliyotolewa na Josephus. HAVIKUANDIKWA NA MAANABII WALIOTUMWA NA MUNGU. NI WATU TU WALIKUWA WAKIJIANDIKIA HISTORIA NA MAMBO YA WAYAHUDI.

SABABU NYINGINE KWANINI WAPROTESTANT WANAVIKATAA VITABU HIVYO.

Makosa yaliyomo
Yudith 1:17 Nebukadneza ni Mfalme wa Ashuru

Tobit 5:13 Malaika alisema Uongo (Azalia Mwana wa Mzee…)
Tobit 6:1-8. 14 Vinafundisha Uchawi
Baruku 3:4 Baruku Mwandishi wa Yeremia ananukuru Daniel
Baruku 3:4, 12:43-45 Vinafundisha Maombi kwa Wafu.

Niwazi kabisa kwamba Vitabu hivi havina mafundisho yenye Uvuvio na vinapingana na vitabu vingine 66 vya Biblia.

Ndiyo maana basi Biblia inayokubarika kwa Waprotestant wote ni ile yenye Vitabu 66.

By Philip Josephek

Max Shimba Ministries Org

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW