Kwenye injili, kuna vianzo gani vya habari kuhusu Yesu mbali ya Biblia vilivyoandikwa kabla ya mwaka 200 BK?
Inawezekana
mtu kufikiri kuwa maisha ya Yesu na Ukristo havikuelezwa, hata nje ya Biblia. Moja
ya malengo ya kutoa nukuu hizi ni kusitisha madai ambayo watu wenye kushuku
wanayatoa kuwa Yesu hakuwahi kuishi hapa duniani.
Cornelius
Tacitus (aliyeishi karibu mwwaka 55
hadi karibu mwaka 117 BK) alikuwa mwanahistoria wa Kiroma aliyeandika kuhusu
matukio ya Roma na Uingereza kuanzia mwaka 15-70 BK. Dharau aliyoionyesha
inadhihirisha kuwa hakuwa rafiki wa Ukristo. Kwenye Annals 15:44 aliandika: “. . . Lakini juhudi zote za kibinadamu, zawadi
zote za kifahari za Mfalme, na kuiridhisha miungu, havikuondoa imani mbaya kuwa
moto mkubwa [wa Roma] ulitokana na amri [ya Mfalme]. Kwa ajili hiyo, ili
kujiepusha na taarifa hiyo, Nero alikazia hatia yake na kutoa mateso makubwa
zaidi kwa kundi la watu lililochukiwa kwa ajili ya mambo yake yasiyopendeza, ambalo
watu wengi waliliita Wakristo. ‘Christus’, ambaye jina hili lilitokana naye, alipewa
adhabu kubwa zaidi na mmoja wa maliwali wetu, Pontio Pilato, wakati wa utawala
wa Tiberius, na ushirikina wenye kusumbua sana, ambao ulidhibitiwa kwa muda,
uliibuka tena Uyahudi, mahali ulikoanzia, na hata Roma, ambako mambo yote yenye
kuchukiza na kuaibisha kutoka sehemu zote za dunia hufanya makao na kupata
ummarufu. Kwa ajili hiyo, kwanza kabisa watu waliobainika kuwa na hatia
walikamatwa; kisha, baada ya taarifa zao, umati mkubwa ulionekana kuwa na hatia,
si kwa ajili ya kuuunguza mji bali kuwachukia binadamu wengine. Vifo vyao viliandamana
na dharau za kila namna. Wakiwa wamefunikwa na ngozi za wanyama, walishambuliwa
na mbwa na wakaangamia, au walisublubiwa msalabani, au walihukumiwa kutupwa
kwenye moto na kuunguzwa, kutumika kama mwanga wakati wa usiku, wakati mwangaza
wa mchana unapokuwa umeondoka . . .”
Tacitus kwenye Histories kitabu cha 5 pia anaongelea undani wa vikosi mbalimbali
vya Kiroma, cha 5, 10, 15, 12, na watu wengine kutoka vikosi vya 18 na 3
walivyozimisha maasi Uyahudi na kuuteketza mji wa Yerusalem.
Nukuu za Tacitus zimechukuliwa kutoka kwenye
kitabu kiitwacho The Annals and The
Histories kilichoandikwa na P. Cornelius Tacitus, Encyclopedia Britannica,
Inc. 1952.
Mara Bar-Serapion alikuwa Mshamu wa kawaida
aliyemwandikia mwanae, Serapion, barua baada ya mwaka 73 BK. Anamsihi kuiga
mwenendo wa watu wenye hekima katika historia ambao walkufa kwa ajili ya mambo
waliyoyaamini, kama vile Socrates, Pythagoras, na mfalme mwenye hekima
aliyeuawa na Wayahudi. Kazi hii imo kwenye jumba la Makumbusho la Uingereza (British
Museum).
Josephus alikuwa mwanazuoni wa
Kiyahudi aliyezaliwa mwaka 37/38 BK, aliyeandika mambo mazuri kuhusu Kristo. Kuna
vifungu viwili ambavyo anamwongelea Yesu. Kwenye kifungu cha kwanza, Josephus
anaongelea maisha na huduma ya Yesu (Antiquities
of the Jews 18.3.3, au 18 §§63-64), na kwenye kifungu cha
pili anamtaja Yesu kama kaka yake Yakobo (Antiquities
of the Jews 20.9.1, or 20 §§200-203). Kuna matoleo mbalimbali ya
kifungu cha kwanza, lakini tutaongelea kwa ufupi matoleo ya Kiarabu na
Kilatini. Toleo la Kilatini, ambalo limeonyeshwa hapa, na toleo la Kiarabu,
ambalo liliandikwa karne ya 10, yanafanana sana isipokuwa toleo la Kiarabu
halina sehemu zilizopigiwa mstari.
“Karibu
na kipindi hiki, Yesu, mtu mwenye hekima, kama ni sahihi kumuita mtu, kwani alikuwa mtendaji wa mambo ya ajabu, -
mwalimu wa watu kama hawa waliopokea kweli kwa furaha. Aliwavuta kwake wengi wa
Wayahudi, na wengi wa mataifa. Alikuwa Kristo; na wakati Pilato, kwa
mapendekezo ya wakuu wa watu miongoni mwetu, alipomhukumu asulubiwe, watu wale
waliompenda tokea mwanzo hawakumuacha, kwani alitokea kwao tena akiwa hai siku ya tatu, kama ambavyo
manabii wa Mungu walivyokuwa wametabiri mambo haya na kisha mambo mengine ya
maajabu elfu kumi kuhusu yeye; na kabila la Wakristo, walioitwa hivyo kwa jina
lake, hawajatoweka leo.” (Antiquities of
the Jews 18.3.3, iliyoandikwa karibu mwaka 93-94 BK). Kifungu hiki
kimetolewa kutoka Josephus: Complete
Works. Kregel Publications 1960. Maneno haya ni muunganiko wa tafsiri ya William
Whiston (1867) na toleo la lenye kutumika sana lililotolewa na Porter na
Coates, Philadelphia, Pennsylvania).
Toleo la Kiarabu ambalo ni fupi kuliko la
Kilatini huchukuliwa kuwa sahihi zaidi. Toleo lolote lililo sahihi, huu ni
ushuhuda wa kuwa Yesu alikuwepo hapa duniani na kuwa alisulubiwa.
Lucian wa Samosata, (pia alifahamika kama Lucian
Mgiriki) mwandishi tashtiti wa karne ya pili, aliyeandika kuhusu Kristo, “. . .
mtu aliyesulubiwa Palestina kwa sababu ya kuanzisha mfumo wa kidini ulimwenguni
. . . Pia, mto sheria wao wa kwanza aliwashawishi kuwa wote ni ndugu wa kila
mmoja wao baada ya kukiuka kwa kukataa miungu ya Kigiriki na kwa kumwabudu
mwalimu wa filisofia mwenyewe aliyesulubiwa na kuishi kwa kufuata sheria zake.”
(The Passing Peregrinus -pia inaitwa The Death of
Peregrine 11-13).
Clement wa Roma alikuwa askofu wa Kikristo
aliyeliandikia kanisa lililoko Korinto, kimsingi aliwauliza kwa nini hawakuwa
wanatii mambo ambayo Paulo aliwaandikia miaka 50 iliyopita. Barua ya Clement
iliandikwa mwaka 97/98 BK.
Pliny Mdogo alikuwa liwali wa of
Bithynia aliyewaua Wakristo wengi kwa sababu ya imani yao. Alimwandikia Mfalme Trajan
mwaka 112 BK na kumuuliza endapo aendelee kuwaua wanaume, wanawake, na watoto
kwa ajili ya kutokuiabudu sanamu ya mfalme. Pliny anasema kuhusu Wakristo, “hata
hivyo walithibitisha kuwa hatia yao yote ilikuwa kwamba walikuwa na mazoea ya
kukutana kwenye siku moja iliyopangea kabla ya jua kuchomoza, baada ya kuimba
mistari ya nyimbo kwa kupokezana wakimtukuza Kristo kama Mungu, na kuweka kiapo
cha kutokufanya matendo yeyote maovu, bali kujiepusha na ulaghai, uizi, uzinzi,
kutokusema uongo, kutokukataa jukumu wanapotakiwa kulitimiza (Epistles 10.96). Pamoja na hayo, Pliny pia
anatupa habari kuhusu Waesene.
Papias ni askofu mwingine
aliyekuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Aliandika kazi nyingi sana karibu na
miaka 110 hadi 130 BK. Kwa bahati mbaya maandiko yake yamepotea, isipokuwa
maelezo mafupi yaliyotolewa na Eusebius wa Kaisaria (aliyeandika karibu mwaka
325 BK). Eusebius anasema kuwa pamoja na mambo mengine, Papias alisema kuwa
Injili ya Mathayo iliandikwa kwenye Kiebrania, Marko alikuwa mkalimani wa
Petro, na kwama Papias alifundisha kuhusu kuja kwa Yesu kabla ya kipindi cha
kutawala kwake duniani kwa muda wa miaka elfu moja, yaani ‘premillennialism.’
(Eusebius alikuwa haamini uwepo wa kipindi hicho, hivyo anaitwa ‘millennialist’).
Ignatius alikuwa mwanafunzi wa Mtume
Yohana. Aliandika barua kwa makanisa mengi, na alikufa ama mwaka 107 au 116 BK wakati
wa utawala wa Mfalme Trajan.
Polycarp askofu wa Smyrna, alikuwa mfiadini Mkristo
na mwanafunzi wa Ignatius aliyeongea kuhusu Kristo. Alikufa karibu mwaka c.163 BK.
Irenaeus, askofu wa yon (Ufaransa), alikuwa mwanafunzi wa Polycarp,
na mfiadini aliyeishi kutoka mwaka 120/140-202 BK. Aliandika andiko kubwa dhidi
ya mafundisho ya uongo ya wakati ule kutoka mwaka 182-188 BK.
Didache (au Mafundisho ya Mitume Watakatifu) kilikuwa ni kitabu cha kiada cha mafundisho
ya kanisa ambacho mtunzi wake na tarehe ya kuandikwa havifahamiki, inakisiwa
kuwa karibu mwaka 380 BK.
Justin Martyr alikuwa ni mwanafilosofia
Mgiriki aliyezaliwa ama mwaka 110 au 114 BK. Alibadili dini na kuwa Mkristo karibu
mwaka 138 na kwa mujibu wa kazi yake, First
Apology ilikuwa miaka 150 baada ya Kristo kuzaliwa. Kwenye utetezi wake wa
kwanza na wa pili, na kazi yake, Dialogue
with Trypho the Jew, Justin anaeleza kuwa Yesu ni Mungu. Chronicon Paschale inaeleza kuwa Justin
aliuawa kwa sababu ya imani yake mwaka 165 BK.
Suetonius, mwanahistoria wa Kiroma na
afisa wa mahakama aliyeandika karibu mwaka 120 BK, anasema kuwa “Wakati
Wayahudi walipokuwa wanafanya vurugu zilizotokana na Krestus (Chrestus, ni
tahajia nyingine ya Kristus [Christus], yaani Krsto), aliwafukuza Roma (Life of Claudius 25.4).
Theophilus, askofu wa Antiokia alikuwa mwandishi wa kwanza
anayefahamika sasa kutumia neno la Kigiriki lenye kumaanisha Utatu (Triad) kwenye To
Autolycus kitabu cha 2 sura ya 15, uk.101. Aliandika kati ya mwaka 168 na 181/188 BK.
Clement wa Alexandria, huyu ni tofauti na Clement
wa Roma aliyeongelewa hapo awali, ambaye aliishi kutoka mwaka 193-217/220 BK. Aliandika
kwa kiasi kikubwa sana ikiwa ni pamoja na wimbo wa Kristo na kazi kubwa iitwayo
Miscellanies.
Hippolytus aliandika kutoka mwaka 225-235/6
BK na aliandika Refutation of All
Heresies. Hippolytus alikuwa mwanafunzi wa Irenaeus.
Tatian aliishi
kutoka mwaka 110-172 BK na aliandika mpangilio wa injili nne unaoweka pamoja
matukio yanayofanana wenye karibu 79% ya mistari yote ya kwenye injili. Kwa
bahati mbaya, baadaye aliiasi imani na kujiunga na Waenkrate (dhehebu la
Kinostisia la karne ya pili waliokuwa wanazuia kuoa au kuolewa, kula nyama na
kunywa mvinyo), dhehebu la mafundisho ya uongo la Kinostisia (harakati kizushi
ya zama za kanisa la Kikristo la karne ya pili BK iliyokazia kuwa mada ni ovu
na kuwa uhuru unapatikana kwa ufahamu).
Talmudi za Kiyahudi zinamwongelea Yesu sehemu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Babylonian Talmud, Tol’doth
Yeshu, Barailu, Amoa ‘Ulla’, Yeb. IV 3, na Baraita. Tazama
pia Tractate Sanhedrin.
Phlegon alikuwa mwandishi wa
Kigiriki kutoka Caria na mtumwa wa Mfalme Harian aliyeachwa huru. Aliandika
muda mfupi baada ya mwaka 137 BK kuwa kwenye mwaka wa nne wa kipindi cha 202
cha miaka mine baina ya michezo ya Olimpiki [33 BK] kulikuwa na “kupatwa kwa
jua kukubwa zaidi” na kwamba “kulitokea giza saa sita mchana [saa 6:00 kamili] hata
nyota zilionekana mbinugni. Kulitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Bithynia, na
vitu vingi vilipidnuliwa huko Nikea” (Case
for Christ, uk.111). Nukuu nzima kwa mujibu wa Baker Encyclopedia of Christian Apologetics, uk.384 inasomeka: “Yesu,
alipokuwa hai, hakujipa msaada wowote ule, lakini alifufuka baada ya kufa na
kuonyesha alama za kuteswa kwake, na kuonyesha jinsi mikono ilivyochomwa nan a
misumari” na baadaye “kupatwa kwa jua wakati wa utawala wa Kaisari Tiberius, ambao
unaelekea kuwa ndio muda Yesu aliposulubiwa, na tetemeko kubwa lililotokea
wakati huo” kwenye Origen Against Celsus
kitabu cha 2 sura ya 33, uk.455 kwenye Ante-Nicene
Fathers juzuu ya 4, na Julius Africanus Events
in Persia sura ya 18, uk.136. Tazama pia Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 59, uk.455.
Thales (au Thallus) alikuwa
mwanahistoria wa Kipalestina aliyetajwa na Julius Africanus (aliyeandika mwaka 232-245
BK) Julius anaongea kuhusu giza lililotkea wakati wa Kristo, “Giza hili
Thallus, kwenye kitabu cha tatu cha historia yake, analiita, kama inavyoonekana
kwangu bila sababu, kupatwa kwa jua” (The
Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6 kipande cha 18, uk.136). Muktadha ni Julius anapoongelea
jinsi muda kuanzia amri ya Ahasuero hadi kusulubiwa kwa Kristo, ulivyotimiza Danieli
9.
Mwanahistoria wa Samaria, Thallus, ambaye ni
tofauti na mwanahistoria wa Kigiriki, Thales, alikuwa anafahamika sana. Kazi
zifuatazo zinamtaja Thallus.
Justin Martyr’s Hortatory Address to the
Greeks kitabu cha 9, uk.277 inawataja
Thallus, Philo, Josephus, na wengineo.
Theophilus to Autolychus sura ya 29, uk.120 anamtaja Thallus, pia kabla ya
hapo Berosus ambaye ni mwanahistoria Mkaldayo aliyeongea kwenye uk.121.
Octavius wa Minucius Felix sura ya 22, uk.186
Tertullian’s
Apology sura
ya 19, uk.33 inawataja Thallus na Josephus.
Julius
Africanus kipande cha 18, uk.136.
The Shepherd
of Hermas
ni kazi ya Kikristo ambayo mwandishi wake hafahamiki iliandikwa karibu mwaka 160
BK.
Athenagoras alimwandikia mfalme wa Roma
utetezi wa Ukristo karibu mwaka 177 BK.
Aristides wa Athens na Quadratus pia wanafahamika kuandika utetezi wa Ukristo, lakini tuna
baadhi tu ya maandiko yao yaliyohifadhiwa.
No comments:
Post a Comment