Monday, August 20, 2018

ETI MTOTO MMOJA WA NUHU ALIACHWA NJE NA KUMEZWA NA MAFURIKO


UTATA MKUBWA KATIKA KORAN

ETI MTOTO MMOJA WA NUHU ALIMEZWA NA MAFURIKO

HUU NI MSIBA MKUBWA SANA

Tuanze kusoma aya za Koran:

Surat Hud 42. Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe naye alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri.

43. Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji. (Nuhu) akasema: Leo hapana wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu ila aliye mrehemu mwenyewe. Na wimbi likawatenganisha, akawa katika walio zama.

Quran iliyo kuja miaka zaidi ya 630 baada ya Biblia inatatanisha kwa kudai eti mtoto mmoja wa Nuhu alimezwa na Mafuriko. Je huyu mtoto jina lake nani? Kwanini Koran haitaji majina ya watoto wa Nuhu?

LAKINI NILIPO ISOMA BIBLIA ISIYO NA SHAKA NDANI YAKE INASEMA HIVI:

NUHU alikuwa na mke na wana watatu. Wana hao ni Shemu, Hamu na Yafeti. Kila mmoja wao alikuwa na mke. Kwa hiyo, jamaa ya Nuhu ilikuwa yenye watu nane.

Kisha, Nuhu na jamaa yake wakaingia katika safina. Ndipo Mungu akaufunga mlango. Nuhu na jamaa yake walingoja humo ndani. Mwanzo 6:9-22; 7:1-9.

“Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe.” Mwanzo 6:18

Mwanzo 9:18-29 SUV
18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani. 19Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.

Biblia imetaja watoto wote wa Nuhu huku Koran ikiweweseka bila ya kutaja ni nani kati ya Shemu, Hamu au Yafethi aliachwa nje na kumezwa na mafuriko.

Tunaposema Koran ni BANDIA huwa hatubahatishi.

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW