Ufunuo 6:12 Kisha nikatazama, na wakati Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa sita, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi; jua likawa jeusi kama gunia la manyoya; MWEZI WOTE UKAWA MWEKUNDU kama damu;
MUHURI WA SITA WAFUNGULIWA
Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama? [Ufuunuo 6:14-17]
Tumeona katika Muhuri wa sita kwamba Ishara kuu zilitokea zikithibitisha kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho na kwamba Yesu alikuwa yu karibu kuja. Kama tulivyokwisha kuona Tarehe1 November Mwaka 1755AD lilitokea tetemeko kuu ambalo halijawahi kuwapo kamwe tokea dunia iumbwe, na tarehe 19 May mwaka 1780AD Jua liligeuka giza kuu na jeusi bila sababu yoyote ya kisayansi ama ya kiasili, na Usiku wa tarehe hiyohiyo Mwezi ulibadilika rangi na kuwa kama damu pia bila maelezo yoyote ya kisayansi ama ya kiasili. Tarehe13 mwezi November, Mwaka 1833AD Nyota zilianguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake utikiswapo na Upepo Mwingi. Matukio haya yote yamekwisha kupita, na hivyo Watakatifu wanapaswa wakutazamie kurudi kwa Yesu mara ya pili siku yoyote na mda wowote ule tangu mwaka mwaka 1750AD na kuendelea.
Ufunuo 6:12 BHND
12Kisha nikatazama, na wakati Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa sita, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi; jua likawa jeusi kama gunia la manyoya; mwezi wote ukawa mwekundu kama damu;
Matendo 2:20 BHN
20jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kutokea ile siku kuu na tukufu ya Bwana.
Yoeli 2:31 NEN
31 Jua litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa mwekundu kama damu, kabla ya kuja siku ya Bwana ile kuu na ya kutisha.
Lakini tukio la Mbingu kuondolewa kama Ukurasa bado halijatokea, na tukio hili litatokea wakati Yesu atakapoonekana akija juu ya mawingu ya Mbinguni.
Yesu atakuja tena katika nguvu kuu na Utukufu mwingi, na kila jicho litamwona. Katika siku hiyo Mbingu zitaondolewa kama Ukurasa unavyokujwa nazo zitatoweka kwa mshindo Mkuu. Viumbe vya asili vitaunguzwa, na dunia itatetemeka sana kama Mlevi na nchi itafumuliwa na vitu vyote vitateketea [2Petro 3:10-12].
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
No comments:
Post a Comment