Sunday, July 1, 2018

Je,kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?

Related image


Taarifa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.

Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa

Gabrieli alivyomtokea Mama wa Yesu

Alienda kwa Mariamu aliyekuwa msikitini Qurani 19:16-17 Saratul Mariam
  1. Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Nyumbani kwake .Luka 1:26-28
  1. Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji gani wala mji gani wala hata nchi haijulikani. IsitosheQurani inasema kuwa Jibrili ndiye aliyemleta utume Muhammed asiwapelekee Mayahudi (hana kosa),Soma Qurani 2:97 Suratul Al-Baqarah
  1. lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na malaika Gabrieli akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya IsraelLuka 1:26
Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.
2.Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu Mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili Qurani 19:7 Suratul Mariam
  1. Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu Luka 1:28.
  1. Jibrili alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe Mwana Mtakatifu Qurani 19:19 Suratul Mariam
  1. Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu QuranI 19:21Suratul Mariam. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la Mwana kwa Mariamu. Balialisema ili nikupe Mwana Mtakatifu.
  1. Lakini malaika Gabrieli alimwambia Mama waYesu kuwa utachukua mimba Luka 1:31
5. Malaika Gabrieli alisema kwaMariamu Mama wa Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu Luka 1:31, 2:21 Gabrieli hakusema kuwa atampa Mwana Mariamu. Bali alisema Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani mtoto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.

Tofauti ya kuzaliwa kwa Isa na Yesu ni hii.

Isa bin Mariam.
Yesu Kristo.
  1. Isa alizaliwa katika shina la mtende Qurani 19:23 Suratul Mariam.
  1. Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe Luka 2:7
  1. Kuzaliwa kwa Isa haijulikani kama mimba ya mama yake ilichua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa Qurani 19:22-23 Suratul Mariam.
  1. Lakini Mariamu Mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia Luka 2:6-7
3.Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa
  1. Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa manabii walitabili kuzaliwa kwa Yesu, Isaya 7:14, 9:6 utabili huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia Mathayo 1:18-23
  1. Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchialiyozaliwa Qurani haikueleza.
4. Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya israel Tazama Luka 2:8-16. Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotowe na Nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme – hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode Mkuu akitawala Yuda tangu
  1. Isa aliongea na watu akiwa mtoto mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii Qurani 19:30-33 Suratul Mariam.
  1. Yesu hakuongea na mtu akiwa mtoto mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12 Luka 2:42-49.

Image result for yesu sio isa
Hivyo tunaona kwamba kuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa.Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW