Monday, June 18, 2018

SHALOM MAANA YAKE NINI?

Image may contain: text

Shalom ni neno la kiebrania lenye maana ya 'amani'. Na neno hili wakati mwingine kipekee kabisa limekuwa likitumika kama salamu ya kusalimiana au kuagana (Hello au goodbye - kwa kiingereza kuonyesha msisitizo). Linaweza kumaanisha amani kati ya Mungu na mwanadamu au kati ya mtu na mtu au mtu na kikundi cha watu. Kwa kiarabu neno hili shalom ni sawa na neno salaam, sliem. Kule nchini Syria wanaita shlomo.

JEHOVAH SHALOM =BWANA ni Amani Yangu (Waamuzi 6:24)

Neno amani katika lugha ya asili Kibiblia lina maana kubwa sana, zaidi ya vile watu wanavyodhani siku hizi. Katika Agano la Kale, neno Amani huitwa * SHALOM* na lina maana kwamba;
Ukamilifu
Usalama
Uzima na 
Kujaliwa hali njema.

Habari njema ni kwamba, Yesu Kristo ndiye Amani ya kweli; uwe na pesa, au usiwe na pesa, Lakini kama unaye Yesu Kristo, Amani tele moyoni. Isaya.9:6,7 Efeso .2:14-18

Lakini katika Agano Jipya, tunapata Ongezeko la maana ya Amani, kwa Lugha ya Kiyunani: yaani, *EIRENE* neno Eirene maana yake ni:

Amani na utulivu (a quietness)
Mahusiano kati ya mtu na mtu (Join or bind together)
Baraka na Mafanikio ( a Prosperity)
Uzima na Afya njema
Haki na furaha ya Roho wa Bwana
Uponyaji wa roho, nafsi, na mwili.(a Divine healing)

Lakini pia, SHALOM kwa maana nyingine humaanisha, mtu aliye na nguvu; hodari wa Kumiliki "mamlaka" ya yule aliyekuwa na nguvu kuliko sisi, na aliyekuwa akitutawala "kimabavu" yaani Ibilisi.

Kwa maana hiyo, tunaposema SHALOM maana yake ni Kuharibu mamlaka ya adui katika maisha yetu ya kila siku. Ukiujua ukweli huu, hupaswi kuacha "kutamka" SHALOM Mara kwa mara kadiri inavyowezekana; kwa vile kila unatamka Shalom, ndivyo unavyozidi kuiharibu mamlaka ya shetani na utawala wake!

Shalom,

Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

2 comments:

Unknown said...

Hakika Bwana Mungu akuongoze zaidi nimebarikiwa..🤝

Anonymous said...

Bwana MUNGU akuze huduma yako wala pasiwe na mtu wala kitu cha kuzuia Huduma yako ndg katika BWANA. SHALOM.

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW