Monday, June 25, 2018

BIBLIA – NENO LA MUNGU LILILOVUVIWA

 

                         SOMO LA 1                     Ufafanuzi: 2 Petro 1:19-21

Tunapoanza kuangalia Biblia na ujumbe wake unasemaje hebu kwanza tujibu baadhi ya maswali ya kawaida yaliyoulizwa.

“Biblia Takatifu” maana yake nini?
Neno “Biblia limetoka katika neno la Kiyunani ‘biblos’ likiwa na maana “Kitabu”.  “Takatifu” ni neno lenye maana ‘weka kando” au “tenga”, likiwa ni jambo lililowekwa kando au limeweka wakfu kwa ajili ya Mungu kwa hiyo kuitwa “Biblia Takatifu”hiki kitabu kiliitwa hivyo kwa sababu kilionekana kuwa ni neno la Mungu lililovuviwa, kilitengeka kabisa toka katika vitabu vingine vyote vilivyowahi kuandikwa.

Biblia iliandikwa lini?
Kwa kweli Biblia ni mkusanyiko wa vitabu au maandiko ambayo yaliandikwa kipindi kirefu takribani miaka 1600 na waandishi wengi tofauti.  Vitabu vya kwanza viliandikwa na Musa karibu 1500 KK, ambapo cha mwisho kiliandikwa na Yohana Mtume kuelekea mwisho wa karne ya kwanza.

Kwa sababu gani Biblia imegawanyika katika Agano la Kale na Jipya?
Kama tukitazama orodha ya majina ya vitabu kabla ya dibaji tunaona kwamba Biblia ina vitabu 66. Waliofasiri waligawa hivi vitabu katika Agano la kale na Jipya miaka mingi baada ya kuwa vimeandikwa. Agano la Kale lina vitabu 39 vilivyoandikwa kwa kiebrania kabla ya kuzaliwa Kristo.  Agano jipya lina vitabu 27 vilivyoandikwa katika lugha ya Kiyunani –Kigriki baada ya Kristo.

Mahali gani ilipoandikwa Biblia?
Palikuwa na watu wengi ambao Mungu aliwachagua kuiandika Biblia zaidi ya muda wa kipindi kirefu.  Ingawa zaidi waliandika wakiwa katika nchi ya Israeli, walikuwepo baadhi kama Daniel na Ezekieli walioandika wakiwa Babeli na wengine kama Mitume walioandika wakiwa katika majimbo tofauti ya dola ya kirumi.  Ukweli wa kushangaza ni kwamba ingawa Biblia iliandikwa kwa kipindi hicho kirefu, sehemu nyingi tofauti na waandishi wengi, ujumbe wake ni kwa kulingana sawa na umekuwa mmoja.  Hali hii peke yake inaonyesha kwamba Mungu ndiye aliyekibuni.

Ni jinsi gani Mungu aliwafanya hawa watu waandike Biblia?
Kuna ushahidi mwingi katika Biblia unaotuambia namna Mungu alivyofanya ujumbe wake unakiliwe.  Mtume Petro anaeleza jinsi hii” … hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu Fulani tu.  Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu (2 Petro 1:20 –21).

Petro anaeleza ya kwamba Mungu aliteua watakatifu au watu wenye kumcha Mungu ambao kwao akawajulisha nia yake. Hawa watu waliandika ujumbe ambao walipokea toka kwa Mungu.  Haya maandishi yaliyounganika yamekuwa kitabu tunachokifahamu kuwa ni Biblia.
Ni kwa sababu gani Biblia iliandikwa?
Swali hili linajibiwa na mtume Paulo namna hii. “Kila andiko, lenye pumzi Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki ili mtu wa Mungu uwe kamili, amekamilika apate kutenda kila tendo jema” / 2 Timotheo 3:16 – 17).

Kwa sababu hiyo Biblia ilitolewa ili kumfundisha mwanadamu kuhusu Mungu na kusudi  lake, na kumwongoza katika njia ya maisha yampendezao Mungu na kuwapa thawabu wale wenye kumtii.

Ni jinsi gani tunaweza kuthibitisha ya kwamba Mungu yupo na kwa kweli Biblia ni Neno lake?

Hili ni swali lenye busara sana lakini jawabu halitatanishi wala si gumu kulifahamu, maana Mungu mwenyewe alitazamia, naye ametoa jawabu sehemu nyingi katika Biblia.  Moja kati ya hili ni katika unabii wa Isaya:-  Maana mimi ni Mungu wala hapana mwingine, mimi ni Mungu wala hapana aliye kama mimi, nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote” (Isaya 46: 9-10).

Tazama kadhia ambazo Mungu ametoa hapa:

Yeye peke yake ni Mungu wala hayupo mwingine.  Ikiwa hii ni kweli basi Mungu wa Biblia peke yake ndiye Mungu wa ulimwengu, na kwa hiyo dini zote nyingine zenye kudai kumwabudu Mungu Mwingine sio za kweli.

Aweza kujulisha mambo yajayo.  Tunafahamu kwa kuona kwamba hakuna mtu wa kumtegemea awezaye kujulisha yajayo.  Katika Biblia Mungu anajulisha kabla matukio ambayo ni vigumu kubashiri, kunena kibinadamu lakini yametokea kwa usahihi kabisa.

Anauweza kutimiliza aliyoeleza habari zake kabla ya kutokea. Sio tu anauwezo wa kujulisha habari ya mambo yajayo, bali pia kuhakikisha yanatimia kwa wakati wake.

Kutokana na hili twaona kwamba Mungu ametoa njia iliyo rahisi sana ambayo kwayo mtafutaji halisi wa ile kweli aweza kupata jawabu la swali “Je! Yupo Mungu na Biblia ni neno lake? Hatutakiwi kuwa na akili nyingi mno au wenye elimu vizuri ili kutafuta jibu.  Inategemea upande wetu kuwa wanyoofu katika kupima mambo kwa maneno ya akili ambayo yameonyeshwa katika Biblia. Unabii ulio katika Biblia unathibitisha kwa nguvu kadhia yake kuwa ni pumzi ya Mungu.  Kwa kifupi tutaona baadhi ya unabii rahisi na kupima dai la Mungu kwamba aweza kujulisha yajayo.

Ukweli Mwingine wa kukumbuka

Biblia Agano la Kale ni dhahiri lilikamilika zaidi ya miaka 200 kabla ya kuzaliwa Kristo.  Septuagint (Tafsiri ya Kiyunani Agano la Kale) inatoa ushahidi wa kihistoria kuhusu jambo hili.

Gombo la Bahari ya Chumvi linasaidia katika kujua tarehe ya Agano la kale.
Ya kwamba Yesu Kristo aliwahi kuishi alihubiri Injili na kuuawa hayo yote yamesemwa dhahiri mbali na taarifa ya Biblia na wana historia walioishi kipindi kile kile yalipotokea.

Ukweli huu unaweza kuthibitishwa na Maktaba inayotegemewa na watu wote.

Katika ukweli huu uliothibitishwa kihistoria sasa tunaweza kupima iwapo Mungu aweza kujulisha hasa mambo kabla hayajatokea tukitambua kwamba utabiri uliofanywa katika Agano la kale umefanywa karibu miaka 250 kabla ya kutimi katika Agano jipya.

Unabii wa kusulubiwa Kristo
Ona kidogo  maelezo yaliyoanza katika unabii ulio katika Zaburi 22 kuhusu kusulubiwa Kristo na jinsi kila maelezo yalivyotimia.  Zaburi hii iliandikwa na Daudi miaka 1000 kabla ya kuja kutimia.

Zaburi  22        Tukio lilipotimilika
Mst 1               Maneno ambayo Kristo atanena akiwa msalabani              Mathayo 27:46
Mst 7-8            Matendo na maneno ya Wayahudi wakiwa kando ya msalaba     Math  27:39-43
Mst 16             Namna hasa ya kufa – kwa kusulubiwa.                                        Math 27:35
Mst 18             Namna ambavyo nguo zake zitagwanywa            Math 27:35; Yn 19:23-24

Ingekuwa vigumu kwa mwanadamu kubashiri matukio haya katika maelezo ya jinsi hii.  Maelezo mengine yanatutaka tu kuamini ya kwamba Yesu mwenyewe, wakati wa Wayahudi waliokana dai lake kuwa ni Masihi, na askari wapagani wa kirumi wote walishirikiana kutekeleza kumsulubisha Yesu na hivyo kutimiza unabii wa Agano la Kale, tena wakaona wawadanganye watu waamini ya kwamba Biblia si neno la Mungu.  Kamwe hili si wazo lenye akili wala ni lenye busara.

Sio tu Zaburi 22 ilibashiri kusulubiwa Kristo bali pia, katika aya ya 22, ufufuo wake.

Baadhi ya unabii kuhusu mataifa.
Nabii Isaya aliishi katika nchi ya Israeli kati ya mwaka760 – 700 KK katika siku zake dola kuu mbili zenye nguvu zilikuwa Ashuru iliyokuwa upande wa kaskazini na Misri upande wa Kusini.

Katika Sura yakeya 13 Mungu alifunuwa kupita kwake kuinuka na kuanguka kwa dola ya Babeli.  Tunatakiwa kutambuwa kwamba utabiri wake wa kwamba Babeli itakuwa dola yenye nguvu ulifanyika si chini ya miaka 100 kabla ya tukio.  Ingawa hivyo unabii wake sio tu unahusu kuinuka kwa Babeli bali pia kuangushwa kwake na Waajemi.  Waajemi waliiangusha Babeli mnamo mwaka 536 KK, kwa hiyo utabiri huo uliafanyika karibu miaka 200 kabla ya kutokea.

Sio tu Isaya alinena kuharibiwa utawala wa Babeli, bali alisema ya kwamba mji hautakaliwa nao utakuwa jangwa.  Huu ulikuwa ni utabiri wa ajabu kwa mji ambao katika siku zake ulikuwa ni mmojawapo wa maajabu ya ulimwengu wa kale (Isaya 13:17-22) .
Hata hivyo hayo sio yote! Tena Isaya alitaja jina la mfalme atakaye iangusha Babeli – Mtu aliyeitwa Koreshi (Isa 45: 1-2) kwa kuongelea hili, Isaya alieleza amri, atakayotoa Koreshi, ya kuwataka Wayahudi waliotawanyika katika dola yake warudi Yerusalemu na wajenge tena Hekalu ambalo liliharibiwa na Wakaldayo (Isaya 44:27-28: Ezra 1:1-4)

Unabii huu unakwenda mbali zaidi ya ubashiri awezao kuufanya mwanadamu.  Ni Mungu tu awezaye kujulisha yajayo.

Ona unabii huu ulikuwa na maana gani katika ulimwengu wa leo.  Ulikuwa na lazima.

Kutabiri taifa litakalokuwa likitawala ulimwengu miaka 100 tangu hapo
Tena likatabirika taifa litakalo angusha nguvu hii ya kwanza miaka 200 tangu hapo.
Ukataja mtawala wa taifa hili la pili.
Na kutaja amri ambayo atatoa alipofikia kuwa na mamlaka

Ni wazi hali hii haiwezekani kwa mtu kutabiri.  Walakini, Mungu kupitia nabii wake Isaya alifanya hivi kikamilifu.  Kwa hivi Mungu hawezi tu kutabiri yajayo, bali pia anaweza kutimiliza kwa usahili wa kushangaza.

Ajabu ya Unabii wa Danieli.
Daniel aliishi kati ya mwaka 600 – KK 534. Unabii wake ulitabiri;
Kuanguka kwa utawala wa Babeli (Daniel 5:25-31)
Kuinuka na kuanguka kwa utawala wa Waamedi na Waajemi (Dani 8:20)
Kuinuka na kuanguka utawala wa Uyunani (Dn 8:21)
Kuharibiwa mji wa Yerusalemu na Warumi mnamo 70 BK (Den 8:9-11)
Mwaka wa Kusulubiwa Yesu Kristo (Dan 9: 24 – 27).

Usahihi wa unabii wa Daniel umeshangaza watu ambao wamekuwa wakiichunguza ‘kweli’ kwa uhalisi, nao wameweka katika hali ngumu wenye mashaka na mafundisho ya dini na wasioamini kuwa yupo Mungu.

Mungu amejulisha nini yajayo?

Tunaweza kusoma Biblia kwa ujasiiri, tukijuwa ya kwamba kama Mungu ametimiza unabii wake wakati uliopita, kwa hakika atatimiza alichotabiri kwa wakati ujao.

Haya ni matukio kwa kifupi tuonayo kabla yake yaliyotabiriwa kipindi chetu.

Kutakuwa na hali ya kuanguka kwa uadilifu na heshima katika jamaii (Luka 17:26-30)

Wayahudi watarejea katika nchi ya Israeli, na Yerusalemu kuwa kitovu cha mivutano ya kimataifa (Zekaria 12: 2-3; Ezekieli 38: 8,12)

Yesu atarudi mwenyewe na wa kuonekana wazi duniani (Mdo 1: 9-11)
Mungu ataanzisha Ufalme wake duniani ambao utaingia mahali pa utawala wa binadamu (Daniel 2: 44)
Ufalme huu utatimiza sala ya Bwana “ Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe duniani, kama yalivyo mbinguni” (Mathayo 6: 9-10)
Yerusalemu utakuwa makao makuu ya huo  ufalme (Yeremia 3:17)
Yesu  Kristo atakuwa Mfalme kipindi hicho (Ufunuo 11: 15, 18)
Katika siku hiyo wakazi wa dunia kwa hiari watajifunza njia ya Mungu wala hakutawa na vita tena (Isaya 2:2-4)

Je! Kuna ujumbe binafsi katika Biblia ulio kwa ajili yetu?

Naama upo.  Mungu anawapa wanaume na wanawake tumainila kushiriki ulimwengu huu mpya na Bwana Yesu Kristo ajapo. Huu ujumbe wenye tumaini unaitwa Injili, ambao unamaana habari njema za ufalme wa Mungu ujao, na wokovu toka dhambi na mauti kupitia Bwana Yesu Kristo .  Huu ni ujumbe ambao Kristo na Wafuasi wake waliuhuribiri (Marko 16:15-16).

Muhutasari wa Maana
Biblia ni neno lenye pumzi ya Mungu, limetolewa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu / 2 Petro 1:20-21)
Ilitolewa ili binadamu aweze kufahamu mpango na kusudi la Mungu na aweze kuwelewa njia zake (2Timotheo 3:16-17)
Kutimia kwa usahili unabii wa Biblia unathibitisha ya kwamba Mungu yupo na kwamba Biblia ni neno lake lililovuviwa (Isaya 46:9-10)
Unabii ambao bado haujatimia unajulisha kwamba Yesu Kristo atarudi hivi karibuni hapa duniani kusimamisha ufalme wa Mungu duniani (Dan 2:44 Math, 6;9 – 10; Mdo 1:9-11)

SOMO LA 1 –Maswali.

1.         Maneno “ Biblia Takatifu” Maana yake nini?
2.         Kuna vitabu vingapi katika Biblia?
3.         Ni jinsi gani Mungu alifanya Biblia hata ikaandikwa?
4.         Ni kwa sababu gani Mungu akafanya Biblia ikaandikwa?
5.         Ni kwa nini Unabii ni moja ya ushahidi mkubwa wa kwamba Biblia ni neno la Mungu?
6.         Baadhi ya matukio gani ambayo Mun

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW