Saturday, May 26, 2018

WAISLAM WANADAI ETI MUNGU WA WAKRISTO NI KAHABA KUFUATANA NA ISAYA 23 AYA YA 17

Image may contain: one or more people, people sitting and text
Je, haya madai ya Waislam ni ya kweli?
Kama kawaida yao, Waislamu wanaendelea kudanganywa na walimu wao na kujipa matumaini kuwa wako kwenye njia ya uzima kutokana na kile wanachoamini kuwa Biblia si Neno la Mungu bali Quran ndiyo Neno la Mungu.
Mojawapo ya uongo mkubwa na wa wazi unahusu aya zilizoko kwenye kitabu cha Isaya. Aya hizo zinasema hizi:
“Hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba. Twaa kinubi, tembea mjini, Ewe kahaba uliyesahauliwa; piga vizuri, imba nyimbo nyingi, upate kukumbukwa tena. Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.”—Isaya 23:15b-17.
Waislamu hulishikilia andiko hili kwa nguvu na kwa kejeli nyingi wakisema, “Mnaona ninyi Wakristo’ Mungu wenu ni kahaba. Mungu gani wa kufuata huyu. Njoni kwa Allah.”
Kwa Wakristo wasio makini, maandiko ya aina hii yanawapotosha kabisa na kuwafanya waone Ukristo kuwa ni dini ya uongo kiasi cha wao kuamua kungia kwenye Uislamu – kumbe wasijue kuwa wanatoka uzimani na kutumbukia mautini. Uongo wa namna hii ni mwingi mno miongoni mwa Waislamu na unaenezwa kupitia intaneti, mihadhara, mabishano ya ana kwa ana, vitabu na kadhalika. Kuna mamia ya aya za Biblia ambazo wamezipotosha na ndizo watakazozitumia kukuondoa Yerusalemu Mpya. Je, wewe ni mmoja wa waliodanganywa na kunaswa?
Baada ya kuanguka kwa Babiloni mwaka wa 539 K.K., Foinike yawa koloni la Milki ya Umedi na Uajemi. Mtawala Mwajemi, Koreshi Mkuu, ni mtawala anayetoa uhuru zaidi. Chini ya utawala wake mpya, Tiro litaanza tena utendaji wake wa awali na kujitahidi sana kupata umaarufu wake wa kuwa kituo cha kibiashara—kama vile kahaba ambaye amesahauliwa na kupoteza wateja wake atafutavyo kuvutia wateja wapya kwa kutembea jijini, akipiga kinubi chake na kuimba nyimbo zake. Je, Tiro litafanikiwa? Ndiyo, Mungu atalipatia mafanikio. Baada ya muda, jiji hilo la kisiwani litapata ufanisi mwingi sana hivi kwamba mwishoni mwa karne ya sita K.K., nabii Zekaria atasema: “Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu.”—Zekaria 9:3.
NUKUU YA AYA:
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.”—Isaya 23:17.
Unaposoma aya hizi, kwa harakaharaka utadhani kana kwamba maneno NAYE na ATAFANYA yanamwongelea Bwana – yaani kwamba Bwana atakapoizuru Tiro basi atapata ujira wake na pia atafanya ukahaba.
Lakini hii ni kwa sababu katika Kiswahili hayabainishi jinsi ya kike au ya kiume. Ukisoma kwa Kiingereza imeandikwa hivi:
And it shall come to pass after the end of seventy years, that the LORD will visit Tyre, and SHE shall turn to her hire, and shall commit fornication with all the kingdoms of the world upon the face of the earth. And her merchandise and her hire shall be holiness to the LORD: it shall not be treasured nor laid up; for HER merchandise shall be for them that dwell before the LORD, to eat sufficiently, and for durable clothing.
Katika Biblia YOTE Bwana huwa anatajwa kama HE na sio SHE. Tazama mfano ufuatayo kutoka Zaburi 147:12-20.
Praise the LORD, O Jerusalem; praise thy God, O Zion.
For he hath strengthened the bars of thy gates; he hath blessed thy children within thee.
He maketh peace in thy borders, and filleth thee with the finest of the wheat.
He sendeth forth his commandment [upon] earth: his word runneth very swiftly.
He giveth snow like wool: he scattereth the hoarfrost like ashes.
He casteth forth his ice like morsels: who can stand before his cold?
He sendeth out his word, and melteth them: he causeth his wind to blow, and the waters flow.
He sheweth his word unto Jacob, his statutes and his judgments unto Israel.
He hath not dealt so with any nation: and as for his judgments, they have not known them. Praise ye the LORD.
Kwa hiyo, tunaposoma andiko hilo la Isaya kwa Kiingereza, tunakuta kuwa linaongelea Tyre (yaani Tiro) na linasema: “and SHE(TYRE) shall turn to her hire” na sio “and HE(LORD) shall turn to her hire”! Pia linasema: “And her merchandise and her hire…” na sio “And HIS merchandise and HIS hire…”
Maneno ya unabii yanayofuata yanavutia kama nini! “Biashara [“faida,” “NW”] yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.” (Isaya 23:18) Faida ya mali ya Tiro yapataje kuwa wakfu? MUNGU aongoza mambo ili itumiwe kulingana na mapenzi yake—ili watu wake wapate kula na kushiba na kuvaa. Hayo yatokea baada ya kurudi kwa Waisraeli kutoka uhamishoni Babiloni. Watu wa Tiro wawasaidia kwa kuleta mbao za mierezi kwa kujenga hekalu upya. Pia waanza tena kufanya biashara na jiji la Yerusalemu.—Ezra 3:7; Nehemia 13:16.
Licha ya hayo, MUNGU apulizia ufunuo mwingine dhidi ya Tiro. Zekaria atoa unabii juu ya jiji la kisiwani ambalo sasa lina mali nyingi: “Tazama, Bwana atamwondolea mali zake, naye ataupiga uwezo wake alio nao baharini, naye mwenyewe atateketezwa kwa moto.” (Zekaria 9:4) Hayo yatimizwa Julai 332 K.K. wakati Aleksanda Mkuu abomoapo jiji hilo maarufu la baharini.
Hitimisho
Andiko la Isaya 23:17-18 limepotoshwa na ‘wahubiri’ wa kiislamu na kupewa maana ua UONGO isiyokuwapo kwenye Biblia. Mungu wetu si kahaba!
Kwa hiyo, ni wazi kuwa aliye kahaba hapa ni mji wa Tiro. Ukahaba unapotajwa kwenye Biblia kuhusiana na nchi au watu wote kwa ujumla, ina maana kumwacha Mungu aliye hai na kwenda kutafuta msaada ama kwa miungu mingine au kwa nchi nyingine. Tazama Ezekieli 16:1-16. Je, Wialsam, bado mnadhani Mungu wetu ni kahaba?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW