Saturday, May 26, 2018

MUHAMMAD ALITAMKA AYA ZA SHETANI KWENYE QURAN


KWANINI MUHAMMAD ALISHINDWA KUTOFAUTISHA KATI YA ALLAH NA SHETANI?
KWANINI MUHAMMAD ALISHINDWA KUTOFAUTISHA KATI YA AYA ZA MASHETANI NA AYA ZA JIBRIL?
Moja ya matukio yenye kuaibisha zaidi kwenye maisha ya Muhammad lilitokea wakati Shetani alipoweka maneno yake kwenye mdomo wa Muhammad. Muhammad alisema maneno ya Shetani kama neno la Mungu. Tukio hili limethibitishwa kwa maandishi na waandishi kadhaa wa Kiislam wa kale na limeongelewa kwenye Hadithi na Kurani. Waislam wa miaka iliyofuata, kwa kujisikia aibu kuwa nabii wao aliyejitangaza mwenyewe amesema maneno ya Shetani, walikana kuwa tukio hili lilitokea. Visingizio na kukana kwingi vimekuwa vikitolewa na hawa Waislam wa miaka iliyofuata ili kulifunika kosa lenye kuhusisha dhambi la Muhammad.
Ni muhimu ikafahamika tena kuwa tukio la ‘Aya za Shetani’ si jambo ambalo limetungwa na watu wasiokuwa Waislam. Tukio hili limerekodiwa na vyazo vya kale zaidi vya Kiislam vilivyokuwepo wakati wa uhai wa Muhammad. Mtu yoyote asifikiri kuwa jambo hili ni hadithi iliyotungwa na watu wenye kuupinga Uislam. Ni kisa kinachopatikana moja kwa moja kwenye rekodi za kale za Kiislam.
Hili moja ya masomo yenye kubishaniwa zaidi kwenye Uislam. Shetani alimsababishia Muhammad kunena maneno yake (Shetani) kama maneno ya Mungu."
Je Kurani Ilisema Nini Mwanzoni?
Sura ya Nyota (Sura 53) mistari ya 19-20 inasema, "Je umemwona Lat, na ‘Uzza, Na mwingine, (mungu mke) wa tata, Manat?"
Allah alikuwa maarufu huko Arabia kabla ya kuja kwa uislam, kama mungu aliyekuwa na mabinti watatu: al-Lat, al-Uzza, na Manat. (Kumbuka kuwa al- inamaanisha ‘yule’, kwa Kiingereza "the".)
Waandishi wanne wa mwanzo wa maisha ya Muhammad waliandika kuwa awali aya hizi zilifuatwa na:
"Hawa ni mawinchi (wasuluhishi) ambao maombi yao yanapaswa kutumainiwa"
Tafsiri: Mabinti wa Allah walifikiriwa kuwa viumbe wa mbinguni wenye kuomba kwa ajili ya wengine. Mawinchi marefu ya Kinumidia ilikuwa ni sitiari yao. Maneno mbadala ya "inatakiwa kutumainiwa" (turtaja) ni "imekubaliwa kwa kuthibitishwa" (turtada). (Kutoka kwenye tafsiri ya Alfred Guillaume ya The Life of Mohammed, iliyoandikwa na Ibn Ishaq, uk.166.
Baadaye, kifungu hiki kiliondolewa na kifungu kifuatacho kiliwekwa badala yake:
"Nini! Kwako wewe mwenye jinsia ya kiume, Na kwake (mwanaume), mwanamke? Tazama, hakika mgawanyo huu hautakuwa wa haki kabisa." (aya za 53:21-22 leo)
Tafsiri: Wale wanaoamini kuwa Allah alikuwa na mabinti watatu hawakuntendea haki Allah, kwa sababu walipendelea watoto wa kiume ingawa walisema kuwa Allah alikuwa na wasichana tu.
Hizi ndizo ambazo zimeitwa "Aya za Shetani." Katika nyakati za sasa Salmon Rushdie alitumia msemo huu tu kwenye kichwa cha riwaya yake ya kubuniwa na isiyohusika na aya hizi, na andiko hili halikiongelei kisa hiki cha kisasa. Kwa upande wa Aya za Sheatani za asili, Muislam au mtu mwingine asiyekuwa Muislam mwenye kutazama jambo hil bila upendeleo anawezaje kujua aya ambazo zilikuwemo toka awali? Sehemu iliyobaki ya andiko hili inatoa ushahidi wa moja kwa moja na ule usio wa moja kwa moja kuwa Aya za Shetani zilikuwemo asilia, na mapingamizi tisa ya Kiislam.
Kama Muhammad alikuwa mtume wa Mungu, kwanini alishindwa kumtambua Shetani alipo weka aya zaje kwenye mdomo wa Muhammad?
Tutamwamini vipi Muhammad kuhusu aya zingine za Quran kuwa sio za Shetani?
Natanguliza pole kwa muhammadans kwa kuingizwa mjini na Muhammad na kulishwa aya za Shetani.
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW