Swali la kujiuliza, kati ya Yesu na Allah ni nani alikuwa wa kwanza kujiita AL BAETH? Maana wa kwanza kujiita Al Baeth basi yeye ndie mwenye haki ya hilo jina, na anaye mfuata ni mkopiaji tu na kamwe si Al Baeth.
Yesu anakujibu miaka 632 kabla ya Muhammad na Quran kuwa yeye ni wa kwanza kujiita AL BAETH:
Yohana 11: 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo (Al Baeth الباعث ), na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Moja ya majina ya Allah wa Waislam ni Al Baeth ikimaanisha Ufufuo. Kumbuka jina la Allah ni Allah mwenyewe, nikimaanisha kuwa hakuna tofauti kati ya Allah na majina yake 99. Allah = Al Baeth.
Surat Al-Haj 22: 5. Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, 7 Na kwamba hakika Saa itakuja hapana shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.
Hii aya ya 5 katika Suratul Al Haj inathibitisha watu walikuwa na SHAKA ya kufufuliwa na Allah kwasababu hawakuona kabla ya hapo Allah akimfufua mtu yeyote yule. Sasa, Allah atajiitaje Al Baeth bila ya kufufua mtu?
Ushahidi thabit wa tukio ni ule wa kwanza na ulichukuliwa wakati wa tukio. Yesu ni wa kwanza kujiita AL BAETH na alijiita AL BAETH wakati wa tukio la kumfufua Lazaro lililo tokea miaka 632 kabla ya kuzaliwa Muhammad na kuteremshwa kwa Quran. Tusome kwa undani zaidi hili tukio Yohana 11:23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. 24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. ENDELEA AYA YA 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Lakini nilipo isoma Quran kwa undani, hakuna sehemu Allah anamfufua mtu au kiumbe, bali alijipachika jina la AL BAETH bila ya muujizo huo na au kumfufua angalau kipenzi chake Muhammad. Allah yeye anawaaminisha watu tu kuwa eti, ata wafufua lakini hakuwai fanya hivyo hata mara moja na wala hana uwezo huo.
Sasa, kati ya Yesu na Allah nani ni AL BAETH?
Yesu aliyeweza kufufua watu au Allah aliyejipachika jina bila ya kufufua watu au kiumbe chochote?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
No comments:
Post a Comment