Friday, May 18, 2018

JE, KUFUNGA KUPI KUMEKUBALIWA NA MUNGU?

Image may contain: one or more people and text
Kufunga maana yake nini?
Kufunga ni hali ya kuunyima mwili chakula, vinywaji, na starehe kwa muda fulani uliotengwa. Tena ni hali ya kuutesa mwili katika kawaida yake kwa ajili ya Mungu.
“Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.”Zaburi 109:24. Pia Zaburi 35:13c “… Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga;…”
Nyakati za Biblia, watu walifunga kwa sababu mbalimbali zilizokubaliwa na Mungu. Baadhi yao walifunga kwa sababu ya huzuni au toba (1 Samweli 7:4-6), wengine walifunga ili kuomba mwongozo wa Mungu au ili wapate kukubaliwa naye (Waamuzi 20:26-28; Luka 2:36, 37), au ili kukaza fikira walipotafakari.—Mathayo 4:1, 2.
Hata hivyo, Biblia inataja pia visa vya kufunga ambavyo Mungu hakuvikubali. Mfalme Sauli alifunga kabla ya kwenda kumwona mwanamke aliyewasiliana na pepo. (Mambo ya Walawi 20:6; 1 Samweli 28:20) Watu waovu, kama vile Yezebeli na watu washupavu ambao walitaka kumuua mtume Paulo, waliamua kufunga au kuwaamuru wengine wafunge. (1 Wafalme 21:7-12; Matendo 23:12-14) Mafarisayo walijulikana sana kwa kufunga kwa ukawaida. (Marko 2:18) Hata hivyo, Yesu aliwashutumu na hawakumpendeza Mungu. (Mathayo 6:16; Luka 18:12) Yehova alikataa vilevile kufunga kwa Waisraeli fulani kwa sababu ya mwenendo na nia zao mbaya.—Yeremia 14:12.
Visa hivyo vinaonyesha kwamba si tendo la kufunga hasa linalompendeza Mungu. Hata hivyo, watumishi wengi wa Mungu waliofunga kwa moyo mweupe walikubaliwa naye. Basi, je, Wakristo wanapaswa kufunga?
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW