Sunday, May 20, 2018

ETI, USIKU NA MCHANA NI ISHARA NA MIUJIZA YA ALLAH




JE HII NI KWELI AU NI UKOSEFU WA ELIMU?
Baadhi ya Waislam wanasema Kurani ina ukweli wa kisayansi kuhusu mizunguko ya jua, mwezi, (na nyakati nyingine sayari). Ninapenda kuchunguza jambo hili, na tutazunguka pande tofauti tofauti kabla ya kufikia uamuzi.
وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ آيَتَيْنِ ۖ فَمَحَوْنَا آيَةَ اللَّيْلِ وَجَعَلْنَا آيَةَ النَّهَارِ مُبْصِرَةً لِتَبْتَغُوا فَضْلًا مِنْ رَبِّكُمْ
{12}
“Na tumeufanya usiku na mchana ni ishara mbili, kisha tukaifuta ishara ya usiku na tukaifanya ishara ya mchana ya kuonea ili mtafute fadhla itokayo kwa Mwenyezi Mungu.” (17:12)
Ishara maana yake nini?
Alama yenye kuwakilisha au kuashiria kitu fulani.
Hivyo basi, kama Usiku na Mchana ni ishara za Allah kama Quran inavyo dai, swali la msingi ni hili: Hii ishara ya usiku inamaana gani na au Allah anaashiria nini kwa binadamu au ni alama ya kuwakilisha au ashiria nini? Hii ishara ya mchana ina maana gani na au Allah ana ashiria nini kwa binadamu au ni alama ya kuwakilisha au ashiria nini?
Sura 36:37-40 inasema, "Na ishara yao ni usiku: Tulijitoa pale toka mchana, na tazama wakazamishwa kwenye giza; 38 na jua linafuata mkondo wake wa kawaida kwa muda liliopangiwa; hii ni amri yake (yeye), aliyeinuliwa kwenye nguvu, yeye ajuaye vyote. 39 Na mwezi-tumeupimia majumba makubwa (kupita toka upande mmoja hadi mwingine) hadi unabadilika kuwa kama sehemu ya chini ya kikonyo cha mtende kilichozeeka (na kunyauka). 40 Jua haliruhusiwi kuukuta mwezi na usiku hauwezi kwenda haraka hata kuupita mchana: Kila kimoja huelea tu kwenye mkondo wake wenyewe (kwa mujibu wa sheria)." (Tafsiri ya Yusuf Ali, toleo la kwanza) [Maneno yaliyo kwenye mabano yamo katika mabano kwenye tafsiri.]
Baadhi ya Waislam wanasema kuwa "jua hufuata njia yake kwa muda ambao limepangiwa" na neno "mkondo" likiwa limewekwa mwishoni. Hata hivyo, hatuwezi kusema vitu vingi sana kuhusu "mkondo" wa jua kwa sababu tafsiri ya Yusuf Ali ina rejeo (la 17) chini ya ukurasa linalohusiana na neno hili likisema "mzunguko, njia." Pia, toleo la Yusuf Ali lililofanyiwa marekebisho linasema "mahali pa kupumzika" badala ya "kipindi."
Je, ni kweli JUA linazunguka kama wanavyo dai Waislam na Allah wao?
SASA TURUDI KWENYE SAYANSI YA DARASA LA TANO
Usiku na mchana unapatikanaje?
Dunia (kutoka neno la Kiarabu; wakati mwingine pia: ardhi na kwa neno asili la Kibantu nchi) ni gimba la angani ambapo juu yake tunaishi sisi binadamu na viumbe hai wengine wengi, tukipata mahitaji yetu, kuanzia hewa ya kutufaa na maji.
Dunia ni mojawapo ya sayari zinazoelea katika anga ya ulimwengu. Kuna sayari nane zinazolizunguka jua, dunia yetu ikiwa sayari ya tatu katika mfumo wa jua na sayari zake.
Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au kizio astronomia 1. Dunia huchukua siku 365.256 kulizunguka jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake na upana wake ni kilomita 12,756.
Siku ni muda wa wakati wa saa 24 ambamo tunaona vipindi viwili; kile cha mwanga wa mchana na kile cha giza la usiku
Mchana na usiku unapatikanaje?
Mabadiliko haya ya mchana na usiku husabibishwa na mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake. Upande wa dunia unaotazama jua unapata mwanga wa mchana lakini upande mwingine usiotazama jua unakuwa gizani.
Sisi pamoja na vitu vyote vilivyo juu ya uso wa dunia, yaani majengo, barabara, bahari, mito, milima, binadamu, misitu, majangwa na kila kitu unachoweza kuwaza kuwa kipo kwenye uso wa dunia, basi vyote huwa katika mwendo kadri dunia inavyojizungusha kwenye mhimili wake. Hivyo basi, wakati upande ule wa uso wa dunia tulipo unapogeukia au kutazamana na jua, basi kwetu inakuwa mchana, pale ambapo upande huo hatutazamani na dunia, basi tunapata usiku, yaani tunakuwa kwenye giza.
LAKINI, MADAI HAYA YA KISAYANSI YANAPINGWA VIBAYA SANA NA MUHAMMAD PAMOJA NA WAISLAM WOTE.
Al-Tabari juzuu ya 1 uk.234 pia inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi yenye matope. Msemo "yenye matope" ni hami’ah, unaomaanisha udongo mweusi wa mfinyanzi, lakini hamiyah ni neno lenye kufanana nalo linaloweza kumaanisha kitu cha moto. (Tazama rejeo la 442 chini ya uk.234).
" [Muhammad] Aliendelea. Wakati jua linachomoza, linainuka juu ya kibandawazi (kinachokokotwa na farasi) toka kwenye moja ya chemchemi hizo likiwa pamoja na malaika 360 …. Wakati Mungu anataka kuvijaribu jua na mwezi, ili kuwaonyesha watumishi wake ishara na kwa njia hiyo kuwataka waache kutokumtii Yeye na kuanza kutii, jua huporomoka ghafla toka kwenye kibandawazi na kuanguka kwenye kina cha bahari, ambacho ni cha mduara. Wakati Mungu anataka kuongeza umuhimu wa ishara kuwatisha zaidi watumishi wake, jua lote huanguka, na hapawi na sehemu yake yoyote inayobaki kwenye kibandawazi. Huko ndiko kupatwa kukamilifu kwa jua, wakati ambapo mchana hujiwa na giza na nyota hutokeza." al-Tabari juzuu ya1 uk.236.
Je, ni kweli jua huzama kwenye chemchem yenye matope, ndio maana tunapata USIKU kama Uislam unavyo dai, au ni kwasababu ya Dunia inavyo zunguka kwenye mhimili wake?
Je, Usiku ni ishara na miujiza ya Allah au ni matokea ya mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake?
Je, mchana ni ishara na miujiza ya Allah au ni matokea ya dunia inapo zunguka kwenye mhimili wake?
Naam kwa elimu hii inathibitisha kuwa Allah sio Mungu na hakuumba chochte kile.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW