Thursday, May 10, 2018

ALLAH HAKUMUUMBA IBILISI BALI YEYE NI IBILISI

Image result for ALLAH SI MUNGU
Tuanze na madai ya Allah ya kumhukumu Ibilisi kuhusu kumsujudia Adam.

Surat Al Baqara 34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Ibilis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.

Allah anadai kuwa Ibilisi alipo ambiwa amsujudie Adam alikataa. Je, Ibilisi alikosea kukataa kumsujudia Adam? Je, Ibilisi ni Malaika kutokana na Quran?

Kumbua Allah kawaamrisha Malaika wamsujudie Adam.

Surat Al Araaf 11. Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.
12. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.


Ibilisi anamjibu Allah kuwa mimi umeniumba kwa moto, ndio maana sikumsujudia Adam. Je, Malaika waliumbwa kwa moto kama Ibilisi?

Uislam unadai kuwa: Malaika waliumbwa kwa mwanga.

Nabii wa Allah alisema: Malaika waliumbwa kutoka mwanga, kama ambavyo majini yaliumbwa kutoka moto usio na moshi na binadamu aliumbwa kama mlivyo fundishwa. Sahih Muslim

MASWALI:

1. Kwanini Allah alimhukumu Ibilisi huku akijua kuwa alio waamrisha wamsujudie Adam ni Malaika?

2. Je, Ibilisi sasa ni Malaika na aliumbwa kwa mwanga?

3. Kama Allah ni Mungu, kwanini asahau kuwa Ibilisi sio Malaika?

HAKIKA ALLAH SIO MUNGU

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kriso Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW