Thursday, May 24, 2018

ALLAH ANADAI ETI DUNIA INA MASHARIKI MBILI NA MAGHARIBI MBILI?

AIBU YA MWAKA KWA MUHAMMAD NA ALLAH


ALLAH ANADAI ETI DUNIA INA MASHARIKI MBILI NA MAGHARIBI MBILI?
Je, nikweli Dunia tunayo ishi ina mashariki mbili na magharibi Mbili, au ni UKOSEFU WA ELIMU?
Tuanze kusoma aya kutoka Quran inayodai hivyo:

Sura Ar-Rahman, Ayah 17-Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.

HAYA TUTAZAME SAYANSI YA DUNIA INASEMA NINI KUHUSU MIELEKEO YA DUNIA

Mashariki ni wapi?
Mashariki ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande jua linapochomoza asubuhi.
Jina "mashariki" limetokana na neno la Kiarabu مشرق mashriq linalomaanisha "mahali jua linapokucha".
Mashariki kawaida huwa upande wa kulia kwenye ramani.

Magharibi ni wapi?
Magharibi ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande wa machweo ya jua.
Magahribi ni pia neno la kutaja saa ya sala ya jioni ya Waislamu na sala hii yenyewe.

Jina "magharibi" limetokana na neno la Kiarabu مَغْرِب maghrib linalomaanisha sehemu upande wa machweo.

Magharibi kawaida huwa upande wa kushoto kwenye ramani.

DIRA NI NINI?
Dira ni kifaa cha kutambua mwelekeo. Ni chombo muhimu kwa kutafuta njia baharini au kwenye ardhi pasipo na alama zinazoonekana kama vile jangwani.

Dira huwa na mielekeo mikuu 4 ambayo ni Kaskazini, Mashariki, Kusini na Magharibi.

Mielekeo ya kati hutajwa kama kaskazini-mashariki / kaskazini-magharibi na kusini-mashariki / kusini-magharibi (kwa Kiingereza Northeast NE/ Northwest NW na Southeast SE/ Southwest SW).

Inawezekana kutaja mieleko makini zaidi kwa mfano Kusini-kusini-magharibi (South-south-west SSW) au Magharibi-kusini-magharibi (west-south-west WSW).

-Sura Al-Ma'arij, Ayah 40-Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza.
Hapa Muhammad ambaye sie msemaji wa Quran anapingana na madai yake ya kwanza kuwa kuna Sura Ar-Rahman, Ayah 17-Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.

Mbali na pande hizi nne, kunazo pande nyingine.

Tazama dira ifuatayo, pande a - h hutamkwa vifuatavyo;
1) Kaskazini
2) Kaskazini kaskazini mashariki
3) Kaskazini mashariki
4) Mashariki kaskizini mashariki
5) Mashariki
6) Mashariki kusini mashariki
7) Kusini mashariki
8) Kusini kusini mashariki
9) Kusini
10) Kusini kusini magharibi
11) Kusini magharibi
12) Magharibi kusini magharibi
13) Magharibi
14) Magharibi kaskazini magharibi
15) Kaskazini magharibi
16) Kaskazini kaskazini magharibi

Ili kukumbuka kwa urahisi dhania kuwa unasema,
“Kaskazini ya kaskazini mashariki kaskazini ya kaskazini mashariki n.k”
Jua huchomoza upande wa mashariki na hutua/huzama upande wa magharibi.
Jua linapochomoza twasema Kumekucha au Kumepambazuka au mawio.

Ni vizuri kuelewa uhusiano wa upande wa jua, wakati na upande wa kivuli k.v: Asubuhi Jua huwa upande wa mashariki. Kivuli huwa upande wa magharibi.

Alasiri Jua huwa upande wa magharibi. Kivuli huwa upande wa mashariki.
Jua linapotua au linapozama husemwa kumekuchwa au kumekutwa. Wakati huo ni machweo au machwa au magharibi.

Kaskazini ndio utosi wa dira. Yaani dira huanzia Kaskazini.
Jina jingine la Kaskazini ni Shimali au Shemali na Matlahi ni jina lingine la Mashariki.
Jua huwa mkabala na kivuli, yaani iwapo jua li kusini, kivuli kitakuwa kaskazini.

ZOEZI A
a) Asubuhi moja nikielekea shuleni, kivuli changu kilikuwa mbele yangu.
Je, shule ilikuwa upande upi? __________
Nyumbani kwangu kulikuwa upande upi?_______
b) Jioni moja nikitoka machungani, kivuli changu kilikuwa upande wangu wa kulia, Je nilikuwa nikielekea upande upi?
c) Juma anaishi kusini mashariki ya Fatuma. Kwa hivyo Fatuma anaishi upande gani wa Juma?
d) Jua huzama upande upi?

ZOEZI B
a) Ni upande upi unaopatikana katikati ya kusini na magharibi?
b) Ni upande upi ulio katikati ya magharibi na mashariki?
c) Ni upande upi ulio katikati ya kaskazini mashariki na kaskazini?
d) Ni upande upi unaopatikana katikati ya kusini magharibi na magharibi?
e) Ni upande upi unaopatikana katikati ya kaskazini na mashariki?

NDIO MAANA NAENDELEA KUSEMA ALLAH SIO MUNGU.
Shalom,

Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu 2:13

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW