Saturday, April 14, 2018

UTABIRI KUHUSU SYRIA NDANI YA BIBLIA

Image may contain: outdoor
Macho ya ulimwengu hivi sasa yapo juu ya Syria. Maafa yanayojitokeza huko sasa hivi, na mbaya zaidi ni kwamba siku za mbeleni inaweza kuwa mbaya zaidi.
Manabii walishatabiri anguko la Dameski-Syria zaidi ya miaka 2500 iliyopita.
Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake... Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi. Yeremia 49:24,26
Katika kituo cha matukio, Syria na mji mkuu wake Damascus. Mji huu ni Mkongwe duniani kuendelea kukaliwa. Imetajwa tayari katika kitabu cha kwanza katika Biblia. Katika kutoka kwanza 14:15, 15: 2, unaweza kusoma kuhusu Damascus.
Mji Umetajwa mara 50 katika Biblia. Pia kuna unabii kuhusu Damascus katika Isaya 17: 1: Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa chungu ya magofu. "
Je, vita vinavyo endelea hivi sasa vya ISIS vinaweza timiza unabii huu wa Damascus kuwa mji wa gofu?
Urusi ni kama simba hasiye na meno anaunguruma lakini mawindo yake yanapokonywa. Taifa lolote linalotegemea Urusi litakuwa limeshika mwanzi unaomchoma mwenyewe. Sadam alitegemea Urusi mwisho wake Urusi ikaishia kumtazama kitanzini.
Watu wengi wanajua kuwa Urusi imefanikiwa kumsaidia Assad lakini hali ni tete uko Syria, maana Marekani ana mkono mrefu hapo, na Syria na Urusi wameshindwa kuhimili mkono wake. Urusi amechanganyikiwa na kuishia kushambulia wapinzani wa Assad ovyo ovyo kwa ndege, kiasi cha UN kumuonya hasitishe mashambulizi yanayoua raia wengi.
Syria itaanguka tu ingawa mpaka sasa imeshapoteza nguvu kwa asilimia kubwa imebakia kusaidiwa tu.
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW