Sunday, April 1, 2018

KWANINI UISLAM UNAPOTEZA WAUMINI?

Max Shimba Ministries
Image may contain: text
KWANINI UISLAM UNAPOTEZA WAUMINI?
BIBLIA INASEMA NINI: Yesu Kristo alionya hivi kuhusu walimu wa uwongo: “Kwa matunda yao mtawatambua. . . . Kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini kila mti uliooza huzaa matunda yasiyofaa.” (Mathayo 7:15-18) “Matunda yasiyofaa” yanatia ndani kujihusisha na mambo ya kisiasa na kuunga mkono mazoea yanayomchukiza Mungu, kama vile ngono kati ya watu wa jinsia moja. (Yohana 15:19; Waroma 1:25-27) Pia, yanatia ndani kuacha kufundisha mafundisho yenye kunufaisha yaliyo katika Maandiko na badala yake kufundisha desturi na utamaduni usio na faida yoyote. (Mathayo 15:3, 9) Yesu alisema: “Lisha kondoo wangu wadogo.” (Yohana 21:17) Hata hivyo, leo watu wengi sana wana njaa ya kiroho.
BIBLIA INASEMA NINI: Paulo, aliyeandika vitabu fulani vya Biblia, alisema hivi: “Sisi si wachuuzi wa neno la Mungu.” (2 Wakorintho 2:17) Hata ingawa Paulo alikuwa mhudumu maarufu katika kutaniko la Kikristo la karne ya kwanza, mara nyingi alifanya kazi ya mikono ili asiwalemee wengine kifedha. (Matendo 20:34) Mtazamo wake ulionyesha kwamba alitii amri hii ya Yesu: “Mlipokea bure, toeni bure.”—Mathayo 10:7, 8.
JE, WEWE umekatishwa tamaa na dini? Watu wengi sana hawapendezwi na dini. Katika nchi nyingi, idadi inaongezeka ya watu wanaosema kwamba wao ‘si watu wa dini’—na jambo hilo linaonyesha kwamba hali ya dini inazidi kuwa mbaya. Baadhi ya nchi hizo zimeorodheshwa hapa.
TUNISIA
Katika mwaka wa 2013, karibu asilimia 60 ya watu waliohojiwa nchini Tunisia walisema kwamba hawaendi msikitini kusali bali wanasali nyumbani. Sababu iliyotolewa ilikuwa mafundisho yanayochochea jeuri yanayoendelezwa humo. Hii ni nchi ya Kiislam yenye asilimia 100 ya Waislam.
MISRI
Kati ya mwaka wa 2005 na 2012, idadi ya watu waliosema wanapendezwa na dini ilishuka kutoka asilimia 53 hadi asilimia 30. Hii ni nchi ya Kiislam na Uislam ni asilimia 100.
JAPANI
Ni asilimia 16 tu ya watu waliohojiwa nchini Japani waliosema kwamba wanapendezwa na dini; asilimia 62 walisema ama hawapendezwi na dini au hawaamini kwamba kuna Mungu. Hii ni yenye dini ya Shinto 54% na Buddhism 40%.
AFRIKA KUSINI
Kati ya mwaka wa 2005 na 2012, idadi ya watu nchini Afrika Kusini waliosema kwamba wanapendezwa na dini ilipungua kwa asilimia 3. Afrika ya Kusini ni 80$ Ukristo.
Takwimu za kila nchi isipokuwa Tunisia zimetolewa kwenye jarida Global Index of Religion and Atheism la 2012, linalochapishwa na shirika la Gallup International. Maoni yalikusanywa kutoka nchi 57 zinazowakilisha zaidi ya asilimia 73 ya idadi ya watu ulimwenguni.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW