Tuesday, April 10, 2018

JE, MKRISTO ANAWEZA KUINGIWA NA PEPO?


Muumini wa Yesu Kristo, ambaye amezaliwa mara ya pili na kuokoka anaweza kuingiwa na pepo?

Tuanze kwa kusoma aya hii:

Mathayo 16: 23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

Hili ni somo gumu sana, lakini linaweza kuw rahisi sana kama tukifuata aya za Biblia na kutoa "Doctrines" za kanisa.

Petro ambaye alikuwa anatembea na Yesu, aliwezaje kuingiwa na SHETANI?

Zaidi ya hapo, Shetani aliwezaje kukaa ndani ya Petro aliye kuwa kwenye huduma ya Yesu?

Ndugu zanguni, pepo anaweza kuiingia na kuharibu maisha yako. Wakristo huwa wana sema hivi: Wakristo wanaitwa watoto wa Mungu na Roho Mtakatifu yuko ndani mwa kila muumini. Mapepo hayawezi kuingia sehemu ambayo kuna Mungu na Roho Mtakatifu kwa sababu Mungu ni Mkuu kuliko roho zote chafu kwa kuwa ndiye Muumbaji wa vyote wakiwemo malaika.

Hayo naweza kuyaita madai na sio facts:
1. Kama kweli Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako hauwezi ruhusu pepo, kuingia ndani yako, IWEJE, wewe huyo huyo unaweza umwa? Je, hapa Roho Mtakatifu ameshindwa kazi au amepungua nguvu?

2. Dai la pili tunasema, pepo hawezi kuingi au kaa sehemu alipo Roho Mtakatifu, Je, IWEJE, basi Petro aingiwe na pepo, huku akiwa na Yesu wakati wote?

Yesu anatoa onyo juu ya roho wachafu katika Mathayo 12:43-45 anaposema, Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kibaya.

Shetani ameshika pabaya sana Wakristo kwa kuwaaminisha kuwa, eti hawawezi kupagawa na pepo au ingiwa na pepo.

Swali la kujiuliza, ni wapi, pepo anakaa ndani ya Mwili?

Hebu tumsome Mtume Paulo katika Warumi 7: 15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

Mtume Paulo anatufamisha katika aya ya 17, kuwa DHAMBI INAKAA NDANI YANGU, sasa tujiulize, KIVIPI dhambi ikae ndani ya Nabii Paulo huki akiwa na Roho Mtakatifu ndani yake kwa wakati huohuo?

Aya ya 18, inasema ndani yako halikai neno jema, sasa, Roho Mtakatifu anakaa wapi?

Hata wewe unayo soma mada hii na kukataa, kivipi utende dhambi huku ukiwa umejazwa na Roho Mtakatifu?

Nafsi na roho ni sehemu mbili muimu za mwili wa ndani ambazo Bibilia yaamini ni tabia kamili za mwanadamu. Inaweza tatanisha kujaribu kutambua kabisa tofauti ilioko kati ya hayo mambo mawili. Neno “roho” laashiria mwili wa ndani pekee wa mwanadamu.

Wanadamu wako na roho, nafsi na mwili. “… nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.” 1 Wathesalonike 5:23

Ingawa katika maandiko ni waumini wanatambulika kuwa hai kiroho (1 Wakorintho 2:11; Waebrania 4:12; Yakobo 2:26), bali wasio amini wamekufa kiroho ( Waefeso 2:1-5; Wakolosai 2:13). Paulo katika uandishi wake, roho ni kitu cha maana katika maisha ya Mkristo (1 Wakorintho 2:14; 3:1; Waefeso 1:3; 5:19; Wakolosai 1:9; 3:16). Roho ni kitu katika maisha ya mwanadamu ambacho kinampa uwezo wa kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu. Popote neno “roho” limetumika, linaashiria sehemu ya ndani ya mwanadamu ambayo “yakutanika” na Mungu, ambaye Yeya mwenyewe ni Roho (Yohana 4:24).

ROHO NA NAFSI:
Hivi viwili hushindana kila kimoja. Kwa maana kila kimoja chaweza kuwa mkuu wa mwili. (Kwa maana mwamini aweza akaongozwa kwa roho akawa rohoni au akaongozwa na nafsi yake akawa mwilini). Hivyo huu ni uhusiano wa ndani. Dhambi ndio adui wa roho ya mwamini kufanya kazi ya Mungu katika utimilifu, hivyo roho ya mtu isipookoka haiwezi kutenda mambo ya Mungu/kumlingana Mungu bali nafsi ataitawala kuamuru mwili ufuate matendo yake(matendo ya mwilini)

Nafsi ikiisha kupokea taarifa,hufikiri na kufanyia maamuzi lakini ikiwa roho ya mtu ikiwa imepokea Yesu,maamuzi yale ya nafsi yanaweza kubatilishwa na roho pamoja na Roho (Roho wa Bwana uleta maamuzi mengine.

Mwanadamu Ni roho, Ana Nafsi na Anakaa Ndani Ya Mwili.
Ukisoma 1Wathesalonike 5:23 Inatusaidia Kuona Maeneo Yote Matatu Ya UTU Wa MTU;


"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU Mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo"
Hapa Unaona Nafsi, Roho Na Mwili Vimetajwa.

ROHO YAKO
Hii Ndo Sehemu Ya Uhai Wako Ulipo. Hii Ndiyo Iliyo Chanzo Cha Uhai Wako. Hii Ndiyo Wewe Halisi. Ikitoka Kwenye Mwili Wanakuita MAREHEMU..."MWILI WA MAREHEMU FULANI" Hii Ni Kwa Sababu "ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA"
Soma Ayubu 32:8, Ayubu 33:4, Mithali 20:27

NAFSI YAKO
Hii Nayo Imebeba Sehemu Kuu Tatu; NIA/ AKILI (Mind), HISIA (Emotions And Feelings) Na UTASHI (Will).
Soma Mathayo 11:28-29, Zaburi 103:1-2, Mithali 23:7a

MWILI WAKO
Ni Nyumba Yako Inayohifadhi Roho Na Nafsi Yako.
Soma Mwanzo 2:7, Mwanzo 3:19b, Wagalatia 5:17-21, 24, 1Thesalonike 4:4.

Utendaji Wako Kama Mtu Unategemea Na "UZIMA ULIONAO ROHONI"

Aliyekombolewa Kwa Damu Ya Yesu [ALIYEOKOKA] na kujaa Neno la Mungu; Huwa anaanza kufanya chochote toka ROHONI- NAFSINI- MWILINI.

Lakini yule ambaye "AMEKUFA ROHONI" Kwa Sababu Ya Dhambi Na Kutokuwa Na Ushirika Na Mungu; Anaishi kinyume chake. Anaishi toka MWILINI- NAFSINI- Na Roho haina kazi maana Imekufa "KIUTENDAJI" Imebakiza tu "UHAI WA KUWA NDANI YA MWILI" Lakini Haina Uwezo Wa KUSHIRIKI MICHAKATO YA KIMAAMUZI NA UTENDAJI!

Mtu ambaye HAJAOKOKA "ALIYEKUFA KIROHO" Anaweza "KUZINI NA KAHABA" Huku "ANAJUA KABISA NI MWATHIRIKA WA VVU", Hajali maana "ANAENDESHWA TOKA MWILINI" Na kwenye NAFSI anachukua tu Uamuzi wa kutenda Hiyo Dhambi.

Mtu ambaye "AMEKUFA KIROHO" anaweza kwenda kumchukua Mme/ Mke Wa Rafiki yake au hata ndugu yake wa damu, japo anajua HAIPENDEZI KWA WANADAMU NA NI DHAMBI KWA MUNGU lakini kwakuwa "ROHO YAKE HAIFANYI KAZI" Bado anajikuta ametenda ingawa anajua ubaya na madhara ya hilo.

NINI KINATOKEA UNAPOOKOKA?

Unapookoka, "MUNGU ANAUMBA ROHO NYINGINE MPYA NDANI YAKO" Maana Ile Ya Kwanza "ILISHAKUFA KWA SABABU YA DHAMBI" Na Hapa Ndipo Ilipo Ile 2Wakorintho Isemayo "HATA IMEKUWA MTU AKIWA NDANI YA YESU KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA; YA KALE YAMEPITA, NA TAZAMA! YOTE YAMEKUWA MAPYA"

Unapookoka "ROHO YAKO INAUMBWA UPYA" Ndo Maana "UNAANZA KUICHUKIA DHAMBI" Utajikuta tu "KIU YA DHAMBI IMEONDOKA" Halafu "KIU YA KUMPENDA MUNGU NA KUTAKA KUMPENDEZA MUNGU INARUDI"

NINI HUFUATA BAADA YA KUOKOKA?

Unapookoka, "MUNGU ANAKUUMBA UPYA ROHO YAKO-Yaani anaingia ndani ya Roho Yako na kuisafisha" Lakini nafsi yako inaendelea kuwa Ileile; Utakuwa unakumbuka dhambi zako, matendo yako maovu, maisha yako yasiyompendeza Mungu nakadhalika lakini tofauti Iliyopo ni hii, "ROHO YAKO ITAKUWA HAI KUKUKUMBUSHA KUWA UMEOKOKA" Kukujulisha kuwa "WEWE NI MWANA WA MUNGU SASA" Na Hivyo kukunyima "UJASIRI NA NGUVU YA KUIENDEA DHAMBI KUITENDA KAMA KABLA YA KUOKOKA"

Hii Sehemu ya nafsi yako inaendelea "KUBADILISHWA NA KUJENGWA KUWA SAWA NA MUNGU APENDAVYO KUTEGEMEA JUHUDI YAKO YA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU NA KULITENDA"

Hivyo basi, kumbe unapo okoka, ni ROHO YAKO inayo okoka na sio nafsi au mwili wako. Hivyo, Shetani bado anaweza kuinfluence nafsi yako na akakaa huko, lakini roho yako imesha okoka. Ndio maana Mtume Paulo anasema kwenye Warumi 7 kuwa, dhambi inakaa ndani yake, yaani dhambi bado ipo kwenye nafsi yoke na nasfi yoke bado inataka kuendesha mwili wako.

Naamini Mungu amekusaidia kujifunza kitu hapa; Yapitie maandiko yote niliyokuwekea hapa Ili kupanua kiasi na wigo wa NENO ndani yako, usiishie kusoma tu.


Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mung Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW