Monday, April 30, 2018
HAKUNA MABADILIKO KATIKA MANENO YA ALLAH
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.
Kwanza yanipasa nimshukuru Mola wetu mlezi ambaye ametupa uwezo wa kununa na kutumia karama ya fikra na kututenganisha na viumbe wengine wote. Baada ya kuipokea na kuikubali njia ya Bwana, na mwongozo wake, matokeo yake ni makuu na yametimizwa na ahadi ya uzima wa milele mbinguni. Kutakuwa na baraka tele na furaha kwani ALLAH amesema: ‘kwa wale wafuatao imani, kutakuwa na zawadi tele zaidi ya chochote chenye kufikiriwa, zaidi ya chochote kionekanacho au kinachosikika.’
Ebu tutumaini kuwa miongoni mwa hao watao bahatika.
Mola wetu aliyetupa akili timamu na fikra safi pia atatuongoza na kutuelekeza, kuona mwanga na kweli utakaotuongoza kwa usalama. Bwana uufanye mkono wetu unyoke kufikilia uwongofu.
Mungu mkuu amefanya tangazo hili:
“Msiliongeze neno niwaamuru wala msilipunguze, mpate
kusishika amri za BWANA, Mungu wenu mwaamuzi’ Kumb 4:2
Na mwishoni kwa injili tukufu, tunasoma onyo kali.
‘Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki,Mungu atamwondelea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.’ Ufunuo 22:18-19.
Baada ya amri hizi nzito namna hii, Je pana mtu yeyote mwaminifu atakayeleta changamoto kwa neno la Mungu au kulibadilisha neno la BWANA?
Imefikiriwa na baadhi ya Waisilamu wengi kwamba Biblia (Yaani Taurati, Zabur na Injili) imechafuliwa na kubadilishwa mara nyingi wakati tofauti tofauti , ima kwa kuongeza jambo ndani yake au kwa kuondoa jambo humo ndani. Kwa muda mrefu watu wenye mawazo haya wamejaribu kuleta hoja dhidi ya Biblia ijapo kwa kweli bado hawajafaulu kuleta ushindi kamilifu kwao basi ni wazi kwamba wamepoteza msingi wote kwa madai yao.
Ndungu yangu Muislamu,ni jambo la ajabu kwamba watu leo hii bado wangali wanadai kwamba Biblia (Taurati, Zaburi na Injili) imefanyiwa mabadiliko ambayo yanaleta utata kati ya Biblia halisi ya awali na Quran. Ni jambo lakusikitisha kwani Quran inashuhudia Biblia, kwamba Biblia kwa kweli ni maneno ya ALLAH, Yaliyoletwa na Mola wetu mwema kuwa nuru , muongozo na rehema. Biblia kwa kweli ni neno la ALLAH ambalo halijawahii kubadilishwa au kuletewa ushindani. Qurani inashuhudia ukweli huu, kwamba hapana mabadiliko katika maneno ya ALLAH.
Ushahidi wa kuunga mkono usahihi wa Biblia ni mwingi zaidi ya uvuli wowote wa shaka. Qurani inatupa ushahidi , Ndungu yangu Muislamu , unaushuhudia ukweli kwamba , Taurati ni kitabu kilicholetwa kutoka kwa Mola wetu mlezi kwa bwana wetu Musa, kuwa muongozo na rehema kwa walimwengu.
‘Hakika sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru…
Q 5:44
Ni wazi kuwa Taurati imetoka kwa BWANA:
‘Sema : Nani aliyoteremsha kitabu alicho kuja nacho Musa,
chenye nuru na uwongofu kwa watu.’ Q6:9
Pasi na shaka ni wazi kuwa Taurati tumepewa kutoka kwa BWANA wetu MLEZI. Mwenyezi .
‘Na hakika tulimpa Musa kitabu na tukafuatisha baada yake
Mitume wengine” Q 2:7
Ni vyema tukumbuke kwamba Taurati aliyokabitiwa Musa:imeitwa “kitabu”
‘Na tulipo mpa Musa kitabu na pambanuo (baina ya haki na
baatili) ili mpata kuongoka.’’ Q 2:53
Hapo pia pana kiashiria ina ukweli kwamba. Taurati alipewa Musa (kitabu na kipambanuzi) Al – Baidwawi anasema katika ufafanuzi wa aya hii:
(Yeye ni miongoni mwa wafafanuzi wazuri na wanaokubalika) kwamba pambanuo inamaanisha kwamba Taurati iljumuisha maana ya kitabu kilicho weka utofauti bayana baina ya halali na haramu, haki na baatili.
“Na kwa yaini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi na
mwangaza, na makumbusho kwa wachamungu” Q 21:48
Al – Baidwawi alisema katika ufafanuzi wake kwamba Taurati ni mwangaza, ni nuru ya kuwaongoza watu wafuate njia ya kheri kuwatoa kwenye kufa moyo na ujinga wa kutofahamu, kuwaongoza watu kwenye kweli ambao ndio utakaowaokoa.
MUKHUTASARI: Ni bayana kwetu , ndungu yangu Muislamu, kutokamana na ufafanuzi huu wote , kwamba Taurati ni kitabu alichopewa Musa na Mola mlezi kama mwongozo, nuru na rehema kwa ulimwengu. Kwa maana hiyo: kwa kuwa Taurati ililetwa na ALLAH.(Quran inapeana ushahidi wa kutosha). Basi ni wazi kuwa Taurati ni maneno ya ALLAH mtukufu.
“Na tulikwisha andika katika zaburi – nacho ni kitabu cha David baada ya Taurati kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema wapate kuitengeneza na kuusahilisha njia za maisha bora humo.”
(Bali wenye upole watairithi nchi.” Zaburi 37:11
wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.” Zaburi 37:29
Na sasa kwako ndungu yangu Muislamu, huu hapa ushahidi wa Qurani, unaoshuhudia kwamba zaburi alipewa Nabii Daudi.
‘Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa zaburi.’ Q 17:55
“Na hakika tulikwisha andika katika zaburi baada ya kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.’’21:105
MUKHTASARI: Ni wazi sasa kwako ndungu yangu Muislamu, kwamba Mwenyezi Mungu amepeana Zaburi kwa mja wake Daudi na ALLAH ( Qurani inashuhudia jambo ili) hivyo basi Zaburi ni neno la ALLAH.
Sasa ndungu yangu Muislamu, ukweli huko bayana kwamba injili pia ililetwa kutoka kwa ALLAH wa Bwana wetu Isa Massihi kuwa nuru mwongozo na mfano kwa wachamungu.
‘Na wahukumu watu wa injili kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu ndani yake.’ Q 5: 47
Na huu ndiyo ushahidi wa ukweli kwamba kila kilichomo ndani ya injili kilipeanwa na Bwana wetu.
“ Na sisi tuliwaamrisha wafuasi wa Isa yaani . Watu wa injili , wakristo, wahukumu kwa hukumu alizo teremsha mwenyezi Mungu. Na wasio hukumu kwa musibu wa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu basi hao wameiacha sharia ya mwenyezi Mungu, ni waasi.”
“Amekuteremshia kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo)”
Kutokamana na ushahidi huu, ni bayana kuwa injili imetoka kwa Bwana kuongoza ulimwengu wote kama vile Qurani ilivyotambua Taurati na Biblia kuwa kipambanuzi. Ni vyema pia kutambua usawa uliopo baina ya Taurati , Injili na Quran
“Enyi watu wa kitabu, mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake” Q3: 65
Twaweza kuona kwa uhakika, jinsi gain ilivyo bayana kwamba Taurati na Injili zote zilipeanwa na ALLAH.
“Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili ilyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo. Sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamungui.’’ Q 5:46
Kwa mara nyingine tena, twaona kuwa injili aliyopatiwa kwa bwana wetu Isa iwe muongozo na nuru.
‘Tena tukafuatisha nyuma yao mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na wengine tukampa injili. Na tukajaalia katika nyoyo za waliomfuatia upole na rehema.”
Tena kwa mara nyingine Quran inatuakikishia kuwa injili imetolewa kwa Allah kwa Bwana wetu Issa
MUKHUTASARI: Kutokamana na haya yote, ni wazi kwetu sote ndungu yangu Muislamu, kwamba injili imepeanwa na ALLAH mtukufu, kwa bwana wetu Issa kama mwongozo na nuru ya ulimwengu . Na hivyo basi kwa kuwa injili ni kitabu kilichopeanwa na ALLAH.( Quran inashuhudia hili) hivyo basi injili ni neno la Allah.
Ndungu yangu Muislamu, hapa pia utapata ushahidi mwingi zaidi kuhusu uhalali na usafi wa Biblia Tkatifu ( Taurati, Zaburi na injili katika sehemu zake zote.
“Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” Q 16:43
“ Tungependa tungeli wateremshia kutokamana na aya hizi mbili za Bwana wetu mlezi kwa yeyote yule muisilamu ni wazi kuwa:
1.Unabii wote kutoka kwa ALLAH ambao ulipewa kwa hao watu wa Mungu kabla ya Muhammad kwa kweli na bila shaka ulitoka kwake Allah. Mola wao. Zingatia neno,Kabla yako ewe Muhamad na vilevile neno ‘uliopewa wewe ewe Muhammad.
2.Kwa kuwa Musa na Daudi ni miongoni mwa manabii wakuu walioshi kabla ya Muhammad vitabu vyao vilitoka kwa Mola mlezi. Na kwa vile Musa alihubiri Taurati, Daudi Zaburi na Isa Injili , vitabu hivi vitatu vitakuwa vimetoka kwa ALLAH.
3. Neno “Alipewa” linammanisha kwamba yote waliyopewa yalikuwa ni maneno ya ALLAH kwa maana hiyo;Taurati Zaburi na Injili vyote ni maneno ya ALLAH mtukufu.
“Hakika sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Natulimpelekea wahyi Ibrahim na Ishmail na Is – haka, na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daudi tukampa Zaburi” Q 4 :163
Kutokamana na haya twaweza fikia hatima hii:
a. Maneno yaliyoshushwa kutoka kwa ALLAH kwa Muhamad yalikuwa sawa kama yale ya Nuhu na manabii wengine waliomfuata (kumbuka na zingatia neno uliyopewa ewe Muhammad)
b. Kwa vile Musa Daudi na Isa wote walikuja baada ya Nuhu, mafundisho yao yalitoka kwa Mola wao Mlezi .Ivyo pia vitabu vyao vyote (Taurati, Zaburi na Injili) yalitoka kwa Mola kulingana na uisilamu yalikuwa ni maneno ya ALLAH yaliyopewa kwa Musa , Daudi na Isa.
MUKHTASARI: Kutokamana na haya, ni wazi kwa Muisilamu yeyote kwamba Qurani kwa bayana inatangaza kwamba Biblia Takatifu (Taurati, Zaburi na Injili) imetoka kwa mwenyezi Mungu. Tazama (Q 26: 3:16:43, 4:163)
Ndungu yangu muisilamu haya ndiyo majina ya sifa ya Taurati na Injili kama yalivyotajwa ndani ya Qurani :
1. Qurani inavipa Taurati na Injili jina la “KITABU”
“Sema:Enyi watu wa kitabu! hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokamana na Mola wetu mlezi.” Q 5:68
“Ewe mtume! Waambie watu wa kitabu (yaani Biblia). Hakimka ninyi hamtakuwa mnafuata dini sahihi ila mtazitangaza hukumu zote za Qurani”
Q 25:63
“Wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa.”Q 29:46
“Enyi mlio pewa kitabu ! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo” Q:4:47
“Watu wa kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Q 4 : 153
Kutokamana na haya twaona wazi kuwa Qurani inaipa Taurati na Injili neno ‘kitabu” ushahidi huu unaungwa mkono pale Qurani inapowatambua wayahudi na wakristo kama “Watu wa kitabu” neno ambalo limerejelewa mara 20 ndani ya Qurani.
2. Qurani inaipa Taurati na Injili sifa ya kuitwa “Dhikr”(Ujumbe wa Mungu)
“Na kabla yako hatukuwatuma watu ila wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui” Q 21:7
Nukuu hii imetajwa katika ufafanuzi wa AL-Jalaleen (uk357) akihitimiza kuwa Qurani inatambua Taurati na Injili kama ‘Al-Dhikir’
MUKHUTASARI: Maneno haya “kitabu” na “Al-Dhikir” ni majina ambayo pia Qurani inajitambua kwao.Kwa kuwa Qurani inaipa Biblia Takatifu jina lilelile lake, huu ni ushahidi tosha kwamba Taurati na Injili vimetoka kwa Bwana Mungu.
“Amekuteremshia kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili. Q 3:3
Haya yote yana dhihirisha wazi kuwa Qurani inatambua Taurati na Injili kuwa na uongozi , nuru, Rehema na Ufunuo.Qurani pia inatuhakikishia kuwa Taurati na Injili vimetoka kwa Mola wetu mlezi
UHAKIKA KUTOKA KWA QURANI:
1. Taurati, Zaburi na Injili vyote ni vitabu vya kibinguni tulivyo pewa na Mola wetu mlezi (Q5:46,17:55,3:3)
2. Taurati, Zaburi na Injili vyote ni sawa sawa na Qurani. (Q 16: 43, 4:163)
3. Qurani vilevile inatambuliwa kwa majina yaleyale ya Taurati na Injili (“kitabu” na “Al – Dhikir) Taz Q 21: 7, 20:99,113
4. Qurani inaelezea kuwa Taurati na injili ni vitabu vitakavyostahiki kuwa vitabu vya mwenyezi Mungu.
Kutokamana na haya yote, Ndungu yangu muisilamu, twaona wazi kuwa Qurani inanakiri kuwa Biblia Takatifu ( Taurati, Zaburi na Injili) ni maneno ya Mungu mkuu.
Huenda kweli utakubali kuwa Biblia Takatifu (Taurati,Zaburi na Injili) ni neno la Mola mlezi kwa kuwa Qurani inashuhudia jambo hilo. Lakini unaweza kusema kwamba baadaye imefanyiwa mageuzi na kubadilishwa. Pia waweza kuwa na fikira kama za ndungu zetu wengine kuwa kweli Taurati ni kitabu kilichotoka kwa Mola wetu kwa kuwa Qurani inashuhudia hilo, lakini Taurati ilifanyiwa mageuzi baada ya Musa na kwa sababu hiyo Mola wetu akampa Injili bwana wetu Isa mwana wa Mariamu. Hata hivyo watu hawa husema pia kwamba injili nayo imefanyiwa mageuzi na ndio maana Allah akaleta Qurani kuwa ukurasa wa Mwisho wa ufunuo wake.
Ebu nikwambie ndungu yangu muisilamu , kwamba Qurani yenyewe inashuhudia ukweli kwamba hapakuwa na mageuzi au mabadiliko yoyote katika maneno ya ALLAH baada ya kupitiwa Musa , Daudi na Isa.
“Hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio tutaoulinda” Q 15:9
Nukuu hii inadhihirisha bayana kuwa Taurati na Injili vyote vimetoka kwa Allah na vimelindwa bila mabadiliko yoyote. Waweza ukadhani ndungu yangu muisillamu;kwamba Qurani ndiyo inayo ashiria kinapotajwa kitabu kitakatifu (Al – Dhikr) wala za Taurati na Injili. Lakini tukumbuke kuwa Qurani yenyewe ndio iliyo vipa kitabu hivi viwili sifa ya Al – Dhikr.”
“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema” Q 21: 105
Ni wazi kwako sasa kwamba kitabu kitakatifu (Al – Dhikr) kinamaanisha Taurati na wala sio Qurani: ushahidi ukiwa kwamba Zaburi imekuja baada ya Taurati, wala sio baada ya Qurani.
“Na kabla yako hatukuwatuma watu ila wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui.” Q 21: 7
Wataalamu na wanavyioni akiwemo Al – Jalaleen (uk 357) na Ibn Kathir (uk 502) wanashikilia maoni kuwa watu waliotajwa katika Al – Dhikr ni wayahudi na wakristo. Sasa utakubaliana nami, ndungu yangu muisilamu, kwamba Taurati na Injili vimetolewa kwa Allah na vyote vimelindwa kutokamana na mageuzi na mabadiliko yoyote yale.
MUKHTASARI: Sote twatambua wazi kwamba Qurani inashuhudia ukweli kwamba hapajakuwa na mabadiliko katika maneno ya Allah na kwamba Biblia ( yaani Taurati, Zaburi na Injili) ni neno la ALLAH kama tulivyotibitisha kwa aya mbalimbali za Qurani.
HATIMA:
Maneno ya Allah yaliyokuja katika Biblia yamesalia bila mageuzi au mabadiliko, kama vile kila muisilamu mwenye ujuzi wa kitabu awezavyo kuona. Kwa hivyo ndungu yangu muisilamu unaposema hata sasa kuwa Biblia ( Taurati, Zaburi na Injili) vimechafuliwa na kufanyiwa mabadiliko; kwa maneno mengine unasema hivi:
1. Qurani sio sahihi
Ni wazi kuwa Qurani inatuhakikishia kuwa maneno ya Mola wetu mlezi hayabadiliki ila bado wewe washikilia kuwa Biblia Takatifu imefanyiwa mabadiiko.
2. Allah anadhunishwa
Kwa kuwa unaashilia kuwa ALLAH alishindwa kuyalinda maneno yake, ingawaje Qurani imeshuhudia kwamba hapatakuwa na mabadiliko katika maneno ya Allah.
3. Qurani imefanyiwa mabadiliko
Ikiwa Biblia Takatifu (Yaani Taurati, zaburi na Injili vimewahi kubadilishwa; waeweze kufikria kinachoweza kufanyika kuhusiana na Qurani Takatifu.
Ebu nikuuleze swali ewe ndungu yangu muisilamu , ikiwa kweli iliwezekana Biblia Takatifu kufanyiwa mabadiliko: Je mabadiliko haya yalifanywa lini? Je ilikuwa kabla au baada ya kuja uisilamu? Ikiwa undisi kwa mageuzi haya yalifanywa kabla ya uisilamu; Je inakuwaje basi kwamba Qurani inashuhudia na kuisifu Taurati na Injili? Badala ya mashambulizi kutoka kwa Qurani kuhusu Taurati na Injili hapana chochote ila sifa na kuvitakasa.
Ndungu yangu Muisilamu, sote twaweza kuona wazi kuwa ni yule mtu asiyekuwa na ujuzi wa Qurani tu awezaye kuwa na mawazo kama hayo ; kwani pamekuwepo na ushahidi mwingi wa kuthibitisha kwamba Biblia Takatifu ilikuwepo kabla na hata baada ya kuja ka uisilamu na imebakia vile vile bila mageuzi au mabadiliko.
“Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za mwenyezi Mungu? Q 5:43
Utagundua kwamba kuna tukio la kiajabu lililotokea zamani za Nabii Muhammad ( Tazama Ibn Kathir, uk 517-518).
Inasemekana kwamba kundi la wayahudi walikuja kwa Mtume Muhammmad wakimtaka kuhukumu baina ya wawili mume na mwanamke walioshikwa katika tendo la zinaa. Mtume akawaamuru wairejelee Taurati. Walipojaribu kuificha sehemu iliyotaja kwamba adhabu ya wazinifu ni kuuwawa kwa kupigwa mawe , mtume Muhammad alitambua hiana zao na akawaingiza waifuate Taurati. Hivyo basi wale wazinifu wawili wakapigwa mawe hata kufa.Huu ni ushahidi bayana kwako ndungu yangu muisilamu, kwamba Taurati ilikuwa bado haijachafuliwa wala kufanyiwa mageuzi.
“Sema Enyi watu wa kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlioteremsiwa kutoka na Mola wenu mlezi.”Q 5:68
“Ewe mtume! Waambie watu wa kitabu (yaani Biblia) hakika nyinyi hamtakuwa mnafuata dini sahihi ila mtapo zitangaza hukumu zote za Taurati na Injili ni mkazitenda.”
Tazama Ibn Kathir, uk 535. Utaona kuwa Taurati na Injili sote zilikuwepo sawia na Qurani na bila mabadiliko yeyote.Laiti sivyo, basi Qurani isingeli wataka wayahudi na wakristo wote pamoja, waambatane, waishike na waifuate Taurati na Injili.
“Na wahukumu watu wa Injili kwa yale aliyoteremsha mwenyezi Mungu ndani yake na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha mwenyezi Mungu, basi hao ndio wapotofu.’
Tena tazama Ibn Kathir uk 523 utagundua kwamba Quraniiliwaamurisha wakristo wajihukumu kwa hukumu za Biblia maishani mwao. Litakuwa jambo lisilo wezekana kwa Qurani kuagiza jambo ili ikiwa Biblia yenyewe imefanyiwa mageuzi ya namna yeyote wakati wowote.
“Huwaoni wale waliopewa sehemu ya kitabu? Wanaitwa kukiende kitabu cha mwenyezi Mungu ili kuwahukumu baina yao; kasha baadhi yao wanageuka wanakikataa” Q3:23
Swali la muhimu hapa, ndungu yangu muisilamu ni hili: Inamkinikaje, inawezekanaje kwa Qurani kuwataka Wayahudi wairejee Taurati ili wapate hukumu ya Mumgu ? Lazima sote tukubaliane kwamba haiwezekani jambo ili ikiwa Taurati ingelikuwa kweli imegeuzwa na kwamba mabadiliko haya yalikuwepo hata zamani za uteremsho wa Qurani.
Ukweli kuwa Qurani inawaita wayahudi na wakristo kufuata hukumu za Taurati na Injili mtawalia , ni ishara na ushahidi mwingine kuonyesha kuwa Taurati na injili havijafanyiwa mabadiliko . Mwana historia Al – Badwawi amenakiri kuwa mtume Muhammad alikuwa na mazoea ya kutembelea shule za wayahudi ambamo Taurati ilifundishwa. Wakati mtufulani (Naiem bin Amir) alipomuuliza kuhusu, imani ipi aliyoishika alijibu “Mimi n ijitolea Ibrahimu na Taurati”
“Enyi mliopewa kitabu! Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha yale mlio nayo”
Q 4:47
Hapa utaona kuwa Ibn Kathir aliufikia ule uelekevu kwamba Qurani inaiunga mkono Taurati na injili.
“Na aminini ndiyo yateremsha ambayo yanasadikisha ndiyo nayo” Q 2: 41
“Kisha akakujieni mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo” Q 3:81
“Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha mwenyezi Mungu. Wao husema tunaamini tuliyo teremshiwa sisi na kuyakataa yasiyo kuwa hayo. Na hali yakuwa hii ndiyo haki inayo thibitisha yale waliyo nayo wao” Q 2:91
Kwa mara nyingine Ibn Kathir uk 89, utagundua kuwa Qurani inashuhudia ukweli na usafi na usahihi wa Taurati na injili jambo ambalo lisingeli wezekana ikiwa vingekuwa vimechafuliwa.
Pia pana maelezo mengi tofauti tofauti ya mwanawachuoni Ibn Kathir akipeana matukio kadhaa yanayoonyesha jinsi gain mtume Muhammad alivyoenzi na kuvutiwa na Taurati na Injili katika zama zake duniani.
“Na ukiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao kitabu kabla yako.”
Vilevile Al – Baidhawi alihitimshwa pale Qurani iliponakiri “ Na ukiwa unayo shaka (ewe nabii Muhammad) Waulize wale wasomao kitabu kabla yake (yaani wayahudi na wakristo)
Nasi pia twafika hatima hiyo kwamba Taurati na Injili vyote viwili vilijulikana na nabii Muhammad na vilikuwa salama kutokamana na mageuzi na mapinduzi , Natumai sasa, ndungu yangu muisilamu kwamba wakubaliana nami kwamba Taurati na Injili havijawahi fanyiwa machafuko, mageuzi au mapinduzi yoyote yale wakati wowote kabla ya uisilamu, zama za nabii Muhammad wala hata baada ya kuja kwa uisilamu duniani.
HATIMA YA UTAFITI
Taurati na Injili zote zilikuwepo ulimwnguni zamani zile alipokuwa analetewa mtume Muhammad Qurani tukufu na vilikuwepo bila ya mabadiliko ushahidi wa haya ni kama ufuatavyo:
1. Nabii wa Uisilamu (Muhammad) aliwataka Wayahudi wairejeree Taurati iwe kitabu cha kuhukumu baina ya wayahudi (Tazama Q 3:23) Ni wazi kuwa mtume asingeli pendekeza watu wairejeree Taurati na Injili ambavyo vimekorogwa.
2. Qurani inawangaa wayahudi ambao licha ya kutoiamini Quarini walijaribu kuitumia kama hakimu kwao. Niwazi kuwa mtume Muhammad aliwashangaa , na kwa kuwa alikubali Taurati basi aliwataka waitumie Taurati kama hakimu wao, kwani ndani yake mna uongofu na mwelekeo. Q: 47 – 52
3. Kwa kuwa nabii wa uisilamu aliwataka watu wa injili (yaani wakristo) waamini kila kitu kilichokuja ndani yake na waifuate (Qu 5:47) Na wazi pia kuwa mtume Muhammad asingali pendekeza wakristo wakirejeree kitabu kilicho korogwa na kubadilishwa. Huu ni ushahidi tosha wa kuthibitisha kuwa injili ilikuwa safi kipindi cha kuteremshwa Qurani.
4. Wakati Nabii wa uisilamu aliposisitiza ya kwamba wayahudi na wakristo wote waishike Taurati na Injili, kwa kuzingatia hukumu zilizokuja ndani yake (Tazama 54:5 2-52. Je wadhani hata kiufupi tu, kwamba mtume Muhammad angalifanya haya ikiwa Taurati au Injili zingelikuwa zimekorogwa na kubadilishwa?
5. Ukweli ni kwamba Qurani inatupa ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Taurati na Injili view safi na bila dosari yeyote. (Tazama Su 3:81, 5: 47 – 52, 4:47 na Qu 2: 89-91)
6. Qurani ilimshauri mtume wa uisilamu kutafuta msaada kutoka kwa watu wasomao Taurati na Injili wakati wowote akiwa na shaka yeyote katika maswali ya dini. (Ikiwa unayo shaka ewe Muhammad.)hauwezi kamwe kupendekeza kuwa Allah angemshauri mtume wake kwenda kwa watu wenye kitabu kilicho korogwa na kubadilishwa. Au jee waweza kupendekeza kinyume?Je angemrejesha katika Taurati na Injili zilizo badilishwa tayari?
7. Qurani yenyewe inawataka wayahudi na wakristo wawe na imani katika Taurati na Injili.
“Enyi mlio amini !Muaminini mwenyezi Mungu na mtume wake, na kitabu alicho kiteremsha juu ya mtume wake, na kitabu alichokiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa mwenyezi Mungu, na malaika wake, na vita vyake, na mitume wake, na siku ya kiyama, basi huyu amekwisha potelea mbai.” Q 4: 136
Ni jambo la kushangaza na wala haliingi akilini kwamba Qurani itawataka waislamu waiamini Biblia ilyoteremshwa kabla ya Qurani kama Biblia ingelikuwa sio kitabu chenye haki. Huu ni ushahidi kamili wa usafi na ukweli na uhakika wa Biblia, kwani Qurani isingeliwataka waislamu waiamini ikiwa ingelikuwa imebadilishwa na kugeuzwa
Sasa basi ni wazi kwako ndungu yangu muisilamu, baada ya utafiti huu wote na ushahidi huu kutoka kwa Qurani; ni dhahiri na zaidi ya uvuli wowote wa shaka kwamba Taurati na Injili vilihifadhiwa katika zama za kuteremshwa Qurani (kwa kuwa Qurani imetupa ushahidi huo) mageuzi yalifanywa baadaye wakati mwingine.Wacha nikwambie ndungu yangu, kwamba Qurani yenyewe inakanusha jambo hili kwa sababu zifuatazo.
1.Katika Su 5:48 inasaema:
“Na tumekuteremshia wewe wa haki, kitabu hichi nacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na kuyalinda”
Maana ya “kuyalinda” ni kuwa maandiko ya Mungu yatasalia na kuwa salama kutokamana na mabadiliko na mageuzi na kukologwa.Inamaana wazi kuwa ikiwa Taurati au injili vimebadilishwa baada ya Muhammad au Qurani ni kusema kuwa Qurani ilishindwa katika kazi yake kama “mlinzi” juu ya Taurati na injili kwa maneno mengine ikiwa Taurati na injili vilibadilishwa baada ya kuteremshwa Qurani, basi watu wa Qurani wameshindwa kuhifadhi kulinda na kuchunga angalau nakala moja au zaidi ya Taurati na injili safi kama mlinzi juu yake.
Wakati wakristo walipotambua kwamba Taurati ina aya nyingi zilizomhusu masihi Yesu, walichukua jukumu la kuwa walinzi wake, na wakaisambaza Taurati na injili kote ulimwenguni. Imekadiliwa kuwa Taurati imetafsiriwa karibuni lugha zote zinazo julikana na wanadamu.Kwa nini basi waisilamu hawakufanya kazi kama hii kwani waliamini kuwa Taurati na Injili ilikuwa na aya nyingi tu zinazo mhusu mtume Muhammad na Qurani?
2 Kwa kuwa tayari tumethibithisha ukweli kwamba Taurati na injili vilihifadhiwa safi kutokamana na mageuzi yeyote zamani za uteremsho wa Qurani: basi ili litatupeleka kufikia hatima hii:
3a) Wakristo wa kweli – zamani za uteremsho wa Qurani walihifadhi nakala ya Taurati maana ndani yake mlikuwepo maandiko mengi yaliyomhusu Yesu na injili.Zaidi ya hayo Yesu mwenyewe alishuhudia usafi na uhaki wa Taurati. Pia imenakiriwa ndani ya Qurani:
“Natuka wafuatisha haio Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili iliyomo ndani yake uwongofu na nuru na inayo sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachangamfu.’ Q 5:46
Hivyo basi ikiwa kuwa vyovyote vile wayahudi wahgelijaribu kubadilisha Taurati, wakristo wangegundua hilo na kutambua mageuzo hayo mara moja kwani walihifadhi nakala halisi ya Taurati.
b) Vilevile kwa mawazo yaleyale, ikiwa wakristo nao wangeli jaribu kubadili chochote ndani ya Taurati , wayahudi wasingeli
8. Qurani yenyewe inawataka wayahudi na wakristo wawe na imani katika Taurati na Injili.
“Enyi mlio amini !Muaminini mwenyezi Mungu na mtume wake, na kitabu alicho kiteremsha juu ya mtume wake, na kitabu alichokiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa mwenyezi Mungu, na malaika wake, na vita vyake, na mitume wake, na siku ya kiyama, basi huyu amekwisha potelea mbai.” Q 4: 136
Ni jambo la kushangaza na wala haliingi akilini kwamba Qurani itawataka waislamu waiamini Biblia ilyoteremshwa kabla ya Qurani kama Biblia ingelikuwa sio kitabu chenye haki. Huu ni ushahidi kamili wa usafi na ukweli na uhakika wa Biblia, kwani Qurani isingeliwataka waislamu waiamini ikiwa ingelikuwa imebadilishwa na kugeuzwa
Sasa basi ni wazi kwako ndungu yangu muisilamu, baada ya utafiti huu wote na ushahidi huu kutoka kwa Qurani; ni dhahiri na zaidi ya uvuli wowote wa shaka kwamba Taurati na Injili vilihifadhiwa katika zama za kuteremshwa Qurani (kwa kuwa Qurani imetupa ushahidi huo) mageuzi yalifanywa baadaye wakati mwingine.Wacha nikwambie ndungu yangu, kwamba Qurani yenyewe inakanusha jambo hili kwa sababu zifuatazo.
1.Katika Su 5:48 inasaema:
“Na tumekuteremshia wewe wa haki, kitabu hichi nacho sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu na kuyalinda”
Maana ya “kuyalinda” ni kuwa maandiko ya Mungu yatasalia na kuwa salama kutokamana na mabadiliko na mageuzi na kukologwa.Inamaana wazi kuwa ikiwa Taurati au injili vimebadilishwa baada ya Muhammad au Qurani ni kusema kuwa Qurani ilishindwa katika kazi yake kama “mlinzi” juu ya Taurati na injili kwa maneno mengine ikiwa Taurati na injili vilibadilishwa baada ya kuteremshwa Qurani, basi watu wa Qurani wameshindwa kuhifadhi kulinda na kuchunga angalau nakala moja au zaidi ya Taurati na injili safi kama mlinzi juu yake.
Wakati wakristo walipotambua kwamba Taurati ina aya nyingi zilizomhusu masihi Yesu, walichukua jukumu la kuwa walinzi wake, na wakaisambaza Taurati na injili kote ulimwenguni. Imekadiliwa kuwa Taurati imetafsiriwa karibuni lugha zote zinazo julikana na wanadamu.Kwa nini basi waisilamu hawakufanya kazi kama hii kwani waliamini kuwa Taurati na Injili ilikuwa na aya nyingi tu zinazo mhusu mtume Muhammad na Qurani?
2 Kwa kuwa tayari tumethibithisha ukweli kwamba Taurati na injili vilihifadhiwa safi kutokamana na mageuzi yeyote zamani za uteremsho wa Qurani: basi ili litatupeleka kufikia hatima hii:
3a) Wakristo wa kweli – zamani za uteremsho wa Qurani walihifadhi nakala ya Taurati maana ndani yake mlikuwepo maandiko mengi yaliyomhusu Yesu na injili.Zaidi ya hayo Yesu mwenyewe alishuhudia usafi na uhaki wa Taurati. Pia imenakiriwa ndani ya Qurani:
“Natuka wafuatisha haio Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati , na tukampa injili iliyomo ndani yake uwongofu na nuru na inayo sadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachangamfu.’ Q 5:46
Hivyo basi ikiwa kuwa vyovyote vile wayahudi wahgelijaribu kubadilisha Taurati, wakristo wangegundua hilo na kutambua mageuzo hayo mara moja kwani walihifadhi nakala halisi ya Taurati.
b) Vilevile kwa mawazo yaleyale, ikiwa wakristo nao wangeli jaribu kubadili chochote ndani ya Taurati , wayahudi wasingeli kubali na wangewazuia mara moja kwa tendo la kuleta nakala halisi ya Taurati.
c) Vilevile, kama wayahudi wangelijaribu kubadilisha injili, wakristo wangali wazima kwa kuileta nakala safi na halisi ya injili.
4. Ni –bayana kuwa uisilamu asilia kama ulivyo, umekuja karibuni miaka 570 baada ya ukristo. Wakati wa kabla ya uisilam, zama za ujinga, ukristo ulikuwa umezaenea takriban kote ulimwenguni ikiwemo Afrika , uabeshi, Irani, India na Uropa.
Hii ilipelekea ugumu kwa watu wa sehemu moja ulimwenguni kubadilisha injili kuwa kazi nzito na isiyo wezekana.
5. Na sasa ndungu yangu muisilamu, lazima tujiulize wenyewe basi: Ni lini ni wapi mageuzi hayo yalifanywa? Ni nani aliyeyafanya mageuzi hayo?Hakuna yeyote ambaye anaweza kutoa na kuthibithisha jina hata moja tu la mwana historia. Myahudi au mkristo anayeweza kudhihirisha jambo hilo.Tena kama basi mageuzi na mabadiliko yeyote yalifanywa kwa makubaliano ya makundi yote mawili, wayahudi na wakristo; basi itakuwa ina maana pana mgongano, kwani Qurani inashuhudia kwamba – Hapana mabadiliko katika maneno ya Allah.
“Nasoma uliyofunuliwa katika kitabu cha Mola wako mlezi. Hapana awezaye kubadilisha maneno haya.”Q 18 :27
Hapana shaka kwamba neno “kitabu” lililotajwa katika ayah ii inaashiria Qurani lakini tamko Maneno yake” Yanaashiria Biblia Takatifu (Yaani Taurati, Zaburi na injili). Vitabu hivi vyote ni maneno ya Allah na tunaamini hapana yeyote awezaye kubadilisha maneno yake.
“Hapana mabadiliko katika maneno ya mwenyeziMungu.” Q 10:64
“Na hakuna abadilishaye maneno ya mwenyezi Mungu.”
HITIMISHO:
1. Biblia (Taurati, zaburi na injili) ni neno la Allah alilopeana Allah kwa waja wake, mitume kabla yenu injili ni mwongozo, nuru na rehema kwa ulimwengu.
2. Qurani anajenga usawa baina yake na Biblia (Yaani Taurati, Zaburi na Injili) kwani zote zililetwa na Allah kwa wajumbe wake kabla yenu.
3. Qurani inajipa jina la sifa kama lile lile inaloipa Biblia – Yaani “kitabu”
4. Maneno ya Allah yaliyopeanwa kwa wajumbe wake yalisalia hivyo na wala bado hayajafanyiwa mabadiliko
“Hakika sisi ndio tulioteremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio tutao ulinda” Q 15 : 9
5. Biblia Takatifu ilikuwepo kipindi ambapo Qurani inateremshwa. Ushahidi ni kuwa , mtume Muhammad aliwataka wayahudi wailete Taurati kuwa hakimu katika mjadhalo baina yao.
6. Ni jambo la kustaajabisha kudhai kuwa kitabu chochote katika vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu mlezi viliwahi kufanyiwa mabadiliko kwani ukweli ni kwamba Taurati na injili vilikuwa vimekwisha tapakaa kote ulimwenguni katika lugha mbali mbali.
NDUNGU YANGU MUISILAMU:
Utafiti huu wote unaungwa mkono na maandiko na dalili kutoka kwa Qurani na pia unaungwa mkono na mabingwa miongoni mwa wanavyuoni wakubwa w kiislamu kama vile Ibn Kathir, Al – Baidhwawi, Al – jalaleen na Al – Bukhari.
Nimeenda umbali huu wote ili kumfanya kila muisilamu wa kweli atosheke kuwa utafiti huu ulifanywa katika uwazi na ukweli. Nimekuwa mwangalifu kutumia Qurani kama haswa kitabu rejeshi ili kukuhakikishia kwamba, wakati utakapokuwa umehitimisha kusoma utafiti huu ,utaweza kukubaliana nami kuwa, Biblia Takatifu (Yaani Taurati, zaburi na injili) vimehifadhiwa kutokamana na mageuzo yeyote au mabadiliko yeyote. Hivi vyote ni vitabu vya Allah nani maneno yake, na tunaamini hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno ya mwenyezi Mungu.
“ Hapana mabadiliko katika maneno ya mwenyezi Mungu” Q 10:64
“Hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu, na hakika sisi ndio tutaolinda.” Q 15:9
Ndungu yangu muisilamu, ikiwa una maswali yeyote kuhusu haya niliyoandika au ikiwa unatamani kupata nakala yako ya Biblia Takatifu, tafadhali niandikie kwa anwani zifuatazo:
Al Shaikh Muhammad Kamal
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "
JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment