Tuesday, April 10, 2018

ETI, YESU ALIPOKUWA AMEKUFA DUNIA ILIKUWA INAENDESHWA NA NANI?

Image may contain: fire, text and food
Hili ndilo swali la wafuasi wa Muhammad kwa Wakristo na leo nitalijibu hapa.
Hili ni swali linalofaa kuulizwa juu ya kiumbe. Kama tungesema kuwa mwanadamu fulani alikuwa amekufa, ndipo kuna mantiki kuuliza kwamba, wakati amekufa nani alikuwa anatunza familia yake? Maana hili ni swali linalohusu tabia za kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuwa mahali kuwili au zaidi kwa pamoja. MUNGU SI MWANADAMU! ANAWEZA YOTE – NA HASA MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO, YAANI YESU KRISTO MUNGU MKUU. TITO 2:13!
Kwanza: Hili swali ni jibu tosha kuwa Allah anaye abudiwa na Waislam sio Mwenyezi Mungu na hana uwezo wa Kimungu. Kabla sijaweka jibu, ngoja nianze na swali kwa Waislamu: HIVI ALLAH ANAENDESHAJE DUNIA WAKATI HAJAWAI FIKA HAPA DUNIANI?
Sifa moja ya Mungu ambayo haipo kwa Allah ni ya kuwa kila mahali kwa wakati mmoja. Hii sifa ya kuwa kila mahali "omnipresent" ni ya Mungu peke yake. Je Yesu alipokufa aliwezaje kuendesha dunia kama wanavyo uliza hawa Waislam wanao mwabudu Allah asiye na uwezo wa kuwa kila mahali?
Yesu anaanza kukujibu kwa kupitia Injili ya Mathayo kama ifuatavyo:
Mathayo 18:20, Inasema: 20 Kwa maana wanapokutana watu wawili au watatu katika jina langu, hapo mimi nipo pamoja nao.”
Sifa ya kuwa kila mahali kwa wakati mmoja ni ya Mungu pekee, lakini Yesu anasema yeye hiyo sifa ni yake na anayo. Umesoma mwenye kwenye Mathayo hapo juu kuwa watu wawili au watatu wakikutana kwa jina lake yeye yupo, Haijalishi mpo nchi gani, yeye yupo. Mkitutana Johannesburg na wengine Capetown na wengine Texas yeye yupo. Hii ndio raha ya Yesu ambaye ni Mungu.
Tuendelee kumsoma Yesu kupitia Zaburi Mlango wa 139
aya 7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? 8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. 9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; 10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.
Tunamsoma Mfalme Daudi hapo juu akikiri kuwa, Mungu yupo kila mahali na huwezi kujificha kutoka kwake. Jambo la kutia aibu, Muislam anauliza, eti Yesu alipo kuwa amekufa nani alikuwa anaongoza dunia? Hivi kweli mtu mwenye akili anawezaje kuuliza swali la kitoto na la kidunia namna hii? Hivi unawezaje kulinganisha uwezo wa Mungu na binadamu ambaye ni dhaifu? Ndio maana huwa nasema Allah hawezi kuwa Mwenyezi Mungu hata mara moja, maana wafuasi wake hawana uelewo wa KIMUNGU kuwa Mungu yupo kila mahali?
SASA nawauliza Waislam: HIVI ALLAH ANAENDESHAJE DUNIA WAKATI HAJAWAI FIKA HAPA DUNIANI? Nijibuni kwa aya na sio matusi.
Leo nimeweka kwa kifupi tu kuwa Yesu yupo kila mahali, haijali wewe upo wapi au nchi gani, ukimwita anaitika na kuja kukusaidia. Ili kumfahamu Yesu zaidi soma kijarida cha http://www.maxshimbaministries.com/…/asilia-mbili-ya-yesu-k… kwa msaada zaidi. Yesu si nabii tu kama ambavyo Waislam nadai, bali ni zaidi ya hapo, maana yeye ni Mungu http://www.maxshimbaministries.com/…/uthibitisho-10-kuwa-ye…
Yesu alipo kuwa amekufa au alipo kuwa nje ya mwili wa kibinadamu bado alikuwa Mungu maana Mungu ni Roho na hafi. Kilicho kufa ni mwili na sio Roho ambaye bado ilikuwa inafanya kazi. Ndio maana Yesu alisema mnapo kuwa wawili au watatu katika jina lake yeye yupo.
Lakini utakuta Waislamu wanauliza maswali ya ajabu sana. Eti, kama Yesu ni Mungu, wakati amekufa, nani alikuwa anaangalia dunia?
Hili ni swali linalofaa kuulizwa juu ya kiumbe. Kama tungesema kuwa mwanadamu fulani alikuwa amekufa, ndipo kuna mantiki kuuliza kwamba, wakati amekufa nani alikuwa anatunza familia yake? Maana hili ni swali linalohusu tabia za kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuwa mahali kuwili au zaidi kwa pamoja. MUNGU SI MWANADAMU! ANAWEZA YOTE – NA HASA MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO!
YESU NI MUNGU MILELE NA MILELE!!
HALELUYA!!
Tafakari
Hoji mambo
Chukua hatua!
Katika huduma yake Max Shimba Ministries Org.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW