VINASABA (DNA) NI NINI?
DNA Ni kifupi cha neno (Deoxyribonucleic
Acid). Hizi ni chembechembe asili za urithi
au viini tete ambavyo hupatikana katika
kila kiumbe hai.
Nasaba hupatikana katika kiini cha seli hai na huwa na taarifa za urithi kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto. Taarifa za nasaba ndizo pekee zenye kutoa ukweli usiopingika kuhusu uzao wa mtoto.
Msingi wa Uchunguzi wa DNA
(Vinasaba)
Kila Binadamu ana mpangilio wa
chembechembe asili za urithi aliyorithi
kutoka kwa wazazi wote wawili (Baba na
Mama). Mpangilio wa chembechembe
asili za urithi hurithiwa nusu kutoka kwa
baba na nusu kutoka kwa mama.
Hivyo basi ili kutambua uhalali wa
mzazi kwa mtoto ni lazima mtoto awe
na chembechembe asili za urithi nusu
zinazooana na za baba na nusu nyingine
zinazooana na za mama.
ZIMEANDIKWA KWA NJIA AMBAYO TUNAWEZA KUELEWA
Bila shaka! Ikiwa Mungu ndiye aliyeumba uhai, basi Mungu ndiye anayestahili kusifiwa wala si mageuzi. (Ufunuo 4:11) Pia, ikiwa sisi tumeumbwa na Muumba mwenye hekima, basi tupo hapa kwa kusudi fulani. Hali isingekuwa hivyo ikiwa uhai ulijitokeza wenyewe.
Habari yoyote iwe ni picha, sauti, au maandishi, inaweza kuhifadhiwa na kushughulikiwa kwa njia nyingi. Kwa mfano, kompyuta hufanya hivyo kielektroniki. Kwa kutumia DNA, chembe hai huhifadhi na kushughulikia habari kwa njia ya kikemikali. DNA hupitishwa wakati chembe zinapogawanyika na viumbe vinapozaliana—uwezo unaoaminika kwamba ndiyo unaofafanua maana ya uhai.
Chembe hutumia habari jinsi gani? Hebu wazia kwamba DNA ni kama kitabu cha mapishi chenye maelekezo na hatua mbalimbali, na kila hatua imeandikwa kwa umakini na utaratibu maalumu. Hata hivyo, badala
Habari zilizo kwenye chembe ya urithi huhifadhiwa mpaka zitakapohitajiwa, labda ili kubadili chembe zilizochakaa au zilizo na ugonjwa kwa kutokeza chembe mpya au kupitisha tabia kwa mtoto.
Kufafanua habari zilizo katika DNA kama “lugha ya molekuli ya chembe za urithi hakutoshi,” anasema Küppers. Anaendelea kusema hivi: “Kama tu ilivyo katika lugha za wanadamu, lugha ya molekuli ya chembe za urithi ina utaratibu maalumu.” Kwa ufupi, DNA ina “sarufi,” au kanuni, zinazoongoza kikamili jinsi maagizo yanavyotolewa na kutekelezwa.
“Maneno” na “sentensi” katika DNA huunda “maagizo” mbalimbali ambayo huongoza kutokezwa kwa protini na viini vingine vinavyojenga chembe mbalimbali zinazounda mwili. Kwa mfano, “maagizo” hayo yanaweza kuongoza kufanyizwa kwa chembe za mifupa, misuli, neva, au chembe za ngozi. Mwanabiolojia wa mageuzi, Matt Ridley aliandika hivi: “Uzi wa DNA una habari au ujumbe ulioandikwa kikemikali, na kila herufi moja inawakilisha kemikali moja.” Akaongezea hivi: “Ni jambo la kushangaza kwamba alama hizo au utaratibu huo hubadilika na kuwa maandishi tunayoweza kuelewa.”
Mwandikaji wa Biblia Daudi alisali kwa Mungu hivi: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa.” Zaburi 139:16) Daudi alitumia lugha ya kishairi. Hata hivyo, kulingana na kanuni, alikuwa sahihi kabisa akiwa mwandishi wa Biblia. Hakuna mwandishi yeyote wa Biblia aliyeathiriwa hata kidogo na hekaya au mapokeo ya watu wa kale.—2 Samuel 23:1,2; 2 Timotheo 3:16.
Wanasayansi wengi husema nini?
Wanabiolojia
wengi na wanasayansi fulani
hufikiri kwamba DNA pamoja na maagizo
yake yaliyopangwa vilitokana na matukio
yaliyojitokeza yenyewe ambayo yalifanyika
kwa kipindi cha mamilioni ya miaka.
Wanasema kwamba hakuna uthibitisho wa
ubuni katika maumbile ya molekuli hiyo
wala katika habari inayobeba na kuituma
wala jinsi inavyofanya kazi.
Biblia inasema nini?
Biblia inasema kwamba
kufanyizwa kwa sehemu mbalimbali
za mwili wetu—hata wakati zitakapofanyizwa—kunahusisha
kitabu cha mfano ambacho
chanzo chake ni Mungu. Ona jinsi
Mfalme Daudi alivyoongozwa na roho kueleza
mambo, akisema hivi kumhusu Mungu:
“Macho yako yalikiona kiini-tete changu,
na katika kitabu chako sehemu zake
zote zilikuwa zimeandikwa, kuhusiana na
siku ambazo zilifanyizwa na hakukuwako
hata moja kati ya hizo.”—Zaburi 139:16.
Uthibitisho unafunua nini?
Ikiwa fundisho
la mageuzi ni la kweli, basi inapaswa
angalau kuonekana kwamba huenda DNA
ilijitokeza yenyewe kupitia mfuatano wa
matukio. Ikiwa Biblia inasema kweli, basi
DNA inapaswa kutoa uthibitisho wenye
kusadikisha kwamba inatokana na Muumba
mwenye utaratibu na akili.
Shalom
Max Shimba Ministries
No comments:
Post a Comment