Monday, March 19, 2018

SHETANI NI NANI NA AMETOKA WAPI?

Image result for WHO IS SATAN
Hivi shetani ni nani? Biblia humwita “mungu wa ulimwengu huu.” Lakini alitoka wapi? Je Mungu alimuumba kama alivyo? Je, yeye ni roho aliyeanguka? Haya hapa ni majibu kutoka katika Neno la Mungu!

Mwanzoni Mungu aliumba makerubi watatu: Lusifa au Nyota ya Alfajiri (aliyegeuka kuwa Shetani), Mikaeli na Gabrieli. Kila mmoja alitawala theluthi ya mamia ya mamilioni ya malaika (Ufunuo 5:11). Nyota ya Alfajiri na theluthi yake walitawala ulimwengu uliokuwa kabla ya Adamu. Yeye, pamoja na malaika zake, waliasi serikali ya Mungu, na leo anawaongoza malaika hawa walioanguka, au mapepo, kama mungu wa dunia hii.

Shetani amekuwa somo lenye shauku kubwa kwa maelfu ya miaka. Amedhaniwa kuwa kama jini, mzuka, na zimwi. Ama kama mtu mwenye sura nzuri ya “kishetani” aliyevalia suti nyekundu, mwenye pembe na uma ya nyasi. Shetani hata amesimuliwa kuwa kama kitu kisicho dhahiri “aliye muhtasari wa maovu yote.” Au kama chanzo cha kila kitu kibaya watendacho watu. Huenda wengi wanaufahamu usemi “shetani alinifanya nitende.” Ingawa fikira hizi ni za kawaida, zote SI SAHIHI! Hata zinapojumuishwa pamoja, kwa kiwango kikubwa zinamwakilisha isivyo roho huyu mkuu aliyeanguka!

Shetani yuko hai na halisi. Biblia inamuita “mungu wa ulimwengu huu” (2 Korintho 4:4). Ufunuo 12:9 husema kwamba “audanganyaye ulimwengu wote.” Kwa hakika hii hujumuisha ukweli juu ya utambulisho wake. Lakini je wakati wote amekuwa shetani? Wakati wote amekuwa yule mwovu, muuaji, mwongo, mkuu wa giza mharabu? Je aliumbwa jinsi hiyo?

Ufunuo 12 husema juu ya Shetani na pepo wake wabaya “walitupwa katika nchi” (fu. 13). Kwa hakika sura hii imepachikwa katikati ya kitabu cha Ufunuo, na ni muhtasari mfupi wa historia ya Kanisa la Agano Jipya.

Fungu la 3 linamwelezea Shetani kama “joka” aliye “kokota theluthi ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika nchi” (fu. 4). Kumbuka kwamba “nyota” hizi zilikuwa ni theluthi ya malaika wote waliokuwa chini ya Nyota ya alfajiri kabla hajaasi.

2 Petro 2:4 hutoa kiashiria kingine juu ya huku “kutupwa chini” kwa Shetani na malaika zake “aliowakokota pamoja” naye. Angalia: “Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa [Shetani hakuwa malaika pekee aliyeasi], bali aliwatupa shimoni.” (Neno la Kigiriki hapa ni tartaros na linamaanisha aidha “gerezani” ama “kizuizini”—hii ni dunia yenyewe.) Pepo hawa wabaya pamoja na Shetani “wanalindwa hata ije hukumu,” wakiisha “kutiwa…katika vifungo vya giza.” Hii inafunua kwamba Mungu aliwatia katika gereza hili la giza pepo wengine wengi walioanguka waungane na “mkuu wa giza.”

Ufunuo 12:7-9 hueleza, kwa undani, lini Shetani na pepo wake wabaya watatupwa hata nchi kwa mara ya mwisho wasipate tena kibali cha kuingia mbinguni. Mafungu ya 12-14 yanaonyesha kwamba mwitikio wa ibilisi ni hasira kuu. Wakati huu wa kutisha unakuja kwa ulimwengu mzima hapo mbeleni kidogo!

Hatima ya Shetani
Lakini kitatokea nini kwa Shetani mara baada ya Kurudi kwa Kristo? Je, ataachwa huru kurandaranda duniani, akiendelea “kudanganya” (Ufu. 12:9) na “kudhoofisha” (Isa. 14:12) mataifa? Je, ataruhusiwa kubakia kuwa “mungu wa ulimwengu huu” (2 Kor. 4:4) milele? Hatima yake ni nini?

Ufunuo 20 huelezea Kristo akisimamisha utawala wa milenia kwa miaka-1000 (fu. 4) na kuzileta “sura za mwisho” katika kisa cha Shetani. Fungu la 2 husema kwamba malaika mwenye nguvu (fu. 1) anamfunga hakika kwa “miaka elfu” na “kumtupa katika kuzimu,” mahali “anapofungwa.” Kisha malaika huyu “[hu]tia muhuri juu yake, kwamba asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie: na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.”

Paulo alitaja wakati wa Shetani kufungwa aliposema, “naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi” (Rum. 16:20). Hii ni ahadi ya Mungu kwa Wakristo wote wa kweli na wanadamu wote, kwa sababu Shetani amewatesa Wakristo na kawadanganya wanadamu kwa maelfu ya miaka!

Mtume Yuda alisema kwamba Shetani na pepo wake wabaya watatupwa nje ya mifumo ya sayari kwenda mahali ambapo Biblia hupafafanua kuwa hapana nuru. Fungu la 13 huwaongelea viumbe hawa wenye kudhalilika kama “nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliyowekewa milele.” Yule “mkuu wa giza” na malaika zake watapata kile wanachostahili—kile walichojiletea wao wenyewe. Yule ambaye hapo awali alijulikana kama “aletaye nuru” alichagua giza. Mungu atampatia giza kamili kwa muda wote utakaofuata!

“Kwa hiyo Mungu HAKUUMBA ibilisi. Aliumba kerubi, Nyota ya alfajiri—mkamilifu katika njia zake, lakini akiwa na nguvu ya uchaguzi huru—na Nyota ya alfajiri alijigeuza mwenyewe akawa shetani kwa kuasi Serikali ya Mungu!’



Shalom

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW