Wednesday, March 28, 2018

KWANINI MUNGU ALIMRUHUSU LUCIFER/SHETANI KUTENDA DHAMBI?



Hili ni swali la kutatanisha na kutetemesha akili.

Shetani Alitoka Wapi? Lakini je wakati wote amekuwa shetani? Wakati wote amekuwa yule mwovu, muuaji, mwongo, mkuu wa giza mharabu? Je aliumbwa jinsi hiyo?

Maswali haya yanahitaji ufafanuzi. Yale ambayo utayasoma yatakusaidia uione picha kamili.

Mwanzoni Mungu aliumba Makerubi watatu: Lusifa au Nyota ya Alfajiri (aliyegeuka kuwa Shetani), Mikaeli na Gabrieli. Kila mmoja alitawala theluthi ya mamia ya mamilioni ya malaika (Ufunuo 5:11). Nyota ya Alfajiri na theluthi yake walitawala ulimwengu uliokuwa kabla ya Adamu. Yeye, pamoja na Malaika zake, waliasi serikali ya Mungu, na leo anawaongoza malaika hawa walioanguka, au mapepo, kama mungu wa dunia hii.

Nyota ya alfajiri (Lucifer) alikuwa ni kiumbe mwenye akili sana—“malaika wa nuru,” kama walivyo “watumishi wake” (2 Korintho 11:13-15). Jina Nyota ya alfajiri lina maana ya “mwenye kuleta nuru.” Kiumbe huyu aliyekuwa mkamilifu hapo awali alileta nuru ing’arayo kwa wote waliokuwa wakimzunguka. Lakini aliasi na kutenda dhambi—na hivyo kuwa “mkuu wa giza.” Uasi wake ukamgeuza kuwa kiumbe aliyepinda, aliyepotoka. Japokuwa ni mwenye akili nyingi, kwa hakika amekuwa malaika kichaa aliyeanguka, asiyejua kutofautisha jema na baya!

Je, Mungu Aliumba Shetani? na:

“Mungu alimweka kerubi mkuu, Nyota ya alfajiri, lakini Nyota ya alfajiri yaani Lucifer alikataa kutekeleza mapenzi ya Mungu, amri za Mungu, serikali ya Mungu. Alitaka kuibadili na iwe yakwake mwenyewe. Hivyo akajiondolea sifa yeye mwenyewe.

Wakati Biblia haitoi maelezo mengi kuhusu uasi wa Shetani na malaika walioanguka, inaonekana kwamba Lucifer kama Kerubi wa malaika (Ezekieli 28:12-18 ) - katika kiburi aliamua kuasi dhidi ya Mungu ili kutafuta kuwa mungu wake mwenyewe. Shetani (Ibilisi) hakutaka kuabudu au kumtii Mungu; alitaka kuwa Mungu (Isaya 14:12-14). Ufunuo 12:4 inaeleweka kuwa maelezo ya kimfano ya thuluthi moja ya malaika kuchagua kufuata shetani katika maasi yake, kuwa malaika walioanguka - mapepo.

Tofauti na binadamu, hata hivyo, uchaguzi malaika waliamuwa na kumfuata Shetani au kubaki waaminifu kwa Mungu ni uchaguzi wa milele. Biblia haitoi nafasi kwa malaika walioanguka ya kutubu na kusamehewa. Wala Biblia haionyeshi kwamba kuna uwezekano zaidi wa malaika kutenda dhambi. Malaika ambao hubaki waaminifu kwa Mungu wameelezwa kuwa "malaika wateule" (1 Timotheo 5:21). Shetani na malaika walioanguka walimjua Mungu katika utukufu wake wote. Wao kuasi, licha yao kujua kuhusu Mungu, ulikuwa uovu mkubwa. Matokeo yake, Mungu hawapi Shetani na malaika wengine walioanguka nafasi ya kutubu. Zaidi ya hayo, Biblia haitupi sababu kuwa wengeamini na kutubu hata kama Mungu angewapa nafasi (1 Petro 5:8). Mungu aliwapa Shetani na malaika uchaguzi huo aliowapa Adamu na Hawa, wa kumtii au kuasi. Malaika walikuwa na uhuru wa uchaguzi wa kufanya; Mungu hakuwalazimisha kwa nguvu au kuhimiza malaika yeyote kutenda dhambi. Shetani na malaika walioanguka walitenda dhambini kwa hiari yao wenyewe na kwa hiyo wanastahili hasira ya Mungu wa milele katika ziwa la moto.

Kwa nini Mungu alimpa malaika uchaguzi huu, wakati Yeye alijua matokeo yake itakuwa namna?

Mungu alijua kwamba theluthi moja ya Malaika wataasi na kwa hiyo kulaaniwa kwa moto wa milele. Pia Mungu alijua kwamba Shetani atazidisha uasi wake zaidi na kumjaribu binadamu katika dhambi. Kwa hivyo, ni kwa nini Mungu alirumhusu? Biblia inatuambia kuwa Mungu ametupa uhuru wa kuchagua. Mwandishi wa Zaburi anatuambia, "Kama kwa Mungu, njia yake ni kamilifu" (Zaburi 18:30). Kama njia za Mungu ni "kamili," basi tunaweza kuamini kwamba lolote afanyalo - na chochote Yeye anaruhusu - ni kamilifu pia. Hivyo mpango kamili kutoka kwa Mungu wetu mkamilifu ulikuwa wa kuruhusu uhuru wa kuchagua ambao Lucifer alichagua kutenda kinyume na mapenzi ya Mungui. Akili zetu si mawazo ya Mungu, wala ni njia zetu njia zake, kama Anavyotukumbusha katika Isaya 55:8-9.

Kwa hiyo Mungu HAKUUMBA ibilisi. Aliumba kerubi, Nyota ya alfajiri—mkamilifu katika njia zake, lakini akiwa na nguvu ya uchaguzi huru—na Nyota ya alfajiri alijigeuza mwenyewe akawa shetani kwa kuasi Serikali ya Mungu!

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW