Thursday, March 22, 2018

KUMBE BIBLIA ILIKUWEPO WAKATI WA YESU



Wapinga Biblia, huwa wanasema eti, Biblia ni kitabu kilicho tengenezwa na Binadamu. LA HASHA.

Hebu tuanze kuthibitisha haya kwa kutumia aya za Biblia Takatifu.

YESU ANANUKUU BIBLIA:

Katika Mathayo 22:23-33, twaona mfano jinsi Yesu alivyotumia maandiko. Alitumia sarufi ya aya ili kuthibitisha anachomaanisha. Yesu alikuwa anakabiliana na fundisho potofu lililokuwa limeenea. Masadukayo waliokuwa wanaunga mkono fundisho hili , walimtega Yesu mbele ya umati wa watu kuhusiana na ndoa, kifo, na kiyama.

YESU ALINUKUU KITABU CHA "KUTOKA":

Yesu alinukuu Kutoka 3:6 ambapo Mungu alimwita Musa ili awaongoze watu wake watoke utumwani. Mungu akajitambulisha kama Mungu wa Amram, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo huku akitumia kitenzi cha wakati uliopo. Maana yake ni kwamba Mungu alikuwa anasema hawa watu wanne walikuwa hai, hata ingawa Ibrahimu alikuwa amekufa mamia kadhaa ya miaka nyuma.

Naye Yesu katika Mathayo 22:32 alikubaliana kwa kusema walikuwa bado hai. Ndipo Masadukayo wakatambua kuwa njama yao imefeli. Lakini makutano wakabaki waduwazwa na Mwalimu mahiri (Mathayo 22:33).

Kama Yesu, nasi lazima tusome maandiko kwa makini na tuelewe kuwa sarufi ni muhimu ili kukitumia vyema kitabu. Mathalani, twaweza kusoma kuhusu “ubatizo mmoja” katika Waefeso 4:5 na tukaelewa kuwa ubatizo mmoja ndiyo unaokubalika na Mungu. Twaweza kusoma katika Mathayo 16:18, ambapo Yesu alisema “na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu” na kwa kutumia sarufi twaweza kuelewa kuwa kuna Kanisa moja. Kanisa hilo moja ni la Kristo, na kuwa Kanisa la Kristo.

Yesu aliyachukukulia maandiko kwa uaminifu na maarifa. Fanya hili liwe kusudi lako. Soma, jifunze na tumia maandiko kwa halali kwa kufuata mfano wa Yesu. Tena, la muhimu zaidi ya yote, unapowasikiliza wahubiri na walimu, wianisha wanavyoyatumia maandiko na namna Yesu alivyoyatumia maandiko.

HEBU TUSOME TENA JINSI YESU ANANUKUU MAANDIKO "BIBLIA" WAKATI ANAJARIBIWA NA SHETANI.

“Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, haya yote nitakupa, ukianguka kunisijudia. Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani; maana (NUKUU) imandikwa Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake” Matthew 4:9-10.

Shetani kwa mara ya pili alishindwa kumshawishi Yesu atende dhambi dhidi ya Babaye. Sasa katika Mathayo 4:8-10, Shetani anamjaribu Yesu kwa mara ya tatu, na tena Yesu anajibu kwa kutumia maandiko kwa kutupa sisi tafsiri ya kimaandiko tunayotakiwa kuiga na kufuata.

YESU ANANUKUU "KUMBUKUMBU LA TORATI":

Kisha shetani akamchukua Yesu mpaka kwenye mlima mrefu na akamshawishi kwa kumuahidi heshima ya kidunia na tunu, kwa msingi wa gharama ya Kristo kuinama kumsujudu Shetani. Kama alivyofanya awali, Yesu ALINUKUU ANDIKO kutoka katika Kumbukumbu la Torati 6:13 na kumwambia shetani kuwa tunatakiwa kumsujudia na kumtumikia Mungu peke yake.

NAAM, NDIO MAANA NAMPENDA SANA YESU ALIYE TUPA BIBLIA AMBAYO YEYE MWENYEWE ALIINUKUU.

Shalom



Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW