Monday, March 19, 2018

KAMA MUNGU NI WA UPENDO, KWANINI KUNA MAJANGA NA UOVU?

Related image
Kwenye Mwanzo 1, kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu kikiwa kizuri, kwa nini radi, milipuko ya magonjwa na majanga mengine hutokea?

Kila kitu kilikuwa kizuri mwanzoni. Lakini katika Warumi 8:20-22 inaonyesha kuwa tokea wakati wa anguko, dunia "ilitiishwa chini ya ubatili" pia. Ulimwengu wote upo chini ya utawala wa mwovu (1 Yohana 5:19), na mkuu wa dunia hii ni Shetani kwa mujibu wa Yohana 12:31; 14:30.

Mungu wa kwenye Biblia hakuumba uovu, wala mwovu wala shetani. Kwamaana. Biblia inasema hivi: Mtume Paulo aliandika, “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu” (1 Korintho 14:33). Wakati MKANGANYIKO mkubwa umegubika utambulisho wa shetani, huhitaji kukanganyikiwa!

Paulo pia aliandika, “JARIBUNI mambo yote; lishikeni lililo jema” (1 The. 5:21), na “MPATE KUJUA hakika mapenzi ya Mungu, yaliyo mema, yakumpendeza, na ukamilifu” (Warumi 12:2).

Mungu hakuumba uovu, lakini uruhusu uovu uwepo. Kama Mungu hangeruhusu nafasi ya uovu, wote mwanadamu na malaika wengemtumikia Mungu kwa lazima, bali si kwa kuchagua. Mungu hakutaka “miigizo” kwa ufupi yenye ingefanya chenye aliwataka wafanye kwa sababu ya “ratiba” yao. Mungu aliruhusu jukumu la uovu ili tuwe na nia njema ya kweli na kuchagua ikiwa ama hatukutaka kumtumikia.

Shalom,



Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW