Wednesday, March 21, 2018

JE, YOHANA MBATIZAJI ALITIMIZAJE UNABII WA ELIYA?

Image result for Was John the Baptist really Elijah?

JE, YOHANA MBATIZAJI ALITIMIZAJE UNABII WA ELIYA?

Kwenye Mathayo 17:12 na Mark 9:11-13, Yohana Mbatizaji alitimizaje unabii wa Eliya? Je alikuwa ni Eliya aliyezaliwa upya katika mwili wa Yohana?

Katika ujio wa kwanza wa Yesu, Yohana alikuwa na lengo na makusudio ya Eliya. Kwa kweli, Eliya (si Yohana) mwenyewe alitokea kwa muda mfupi wakati wa kubadilika kwa sura ya Yesu. Watu wengi wanadhani kuwa Eliya atakuwa mmoja wa mashahidi wawili watakaotokea kabla ya baragumu ya saba kupigwa kulingana na Ufunuo 11:3-12.

Mwandishi wa kwanza anayefahamika kuongelea aya hii ni Justin Martyr (aliyeishi karibu mwaka 138-165 BK), aliyesema kuwa dhana ya mtu kuwa na roho ya mwingine haipo kwa Eliya na Yohana Mbatizaji tu. Mungu aliahidi kuwa Yoshua atakuwa na roho ya Musa (Dialogue with Trypho the Jew sura ya 49, uk.220). Pia Elisha alikuwa na sehemu maradufu ya roho ya Eliya kulingana na 2 WaFalme 2:9-10.

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW