Thursday, March 22, 2018

BIBLIA ILIANDIKWA NA MUNGU MWENYEWE


Najua teyari watu wameasha anza kuweweseka maana wamezoea kuaminishwa uongo. Biblia imekamilika, na inajibu madai potofu ya kuwa eti, Biblia sio maandiko ya Mungu na haikutoka kwa Mungu.

Haya tuanze kufikicha akili na Max Shimba Ministries.

UTHIBITISHO 1:

Kutoka 31: 18 Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.

Biblia inatuthibitishia kuwa Maandiko ambayo Musa alipewe yaliyo kuwa kwenye "TABLETS" yaani mbao mbili za Mawe, yalikuwa maandiko ya Mungu na yaliandikwa na Mungu Mwenyewe.

UTHIBITISHO 2:

Kutoka 32: 15 Basi, Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake; mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa. 16 Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao.

Kutoka 32 inaendelea kututhibitishia kuwa Mungu alindika Biblia na kumkabidhi Musa.

BAADA YA MUNGU KUANDIKA SHERIA, TUNASOMA NA MUSA NAYE ANAKUKUU ALICHO ANDIKA MUNGU, NA KUWAPA WANA WA ISRAEL:

Kumbukumbu la Torati 31: 9 Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la agano la Bwana, na wazee wote wa Israeli.

JE, MUSA ALIANDIKA KWA MUONGOZO WA NANI?

2 Petro 1: 20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. 21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

YESU NDIE ALIRUHUSU WAANDISHI WA AGANO JIPYA:

Mathayo 23:34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

Naam, leo nimewathibitishia kuwa Biblia yote imetoka kwa Mungu na MWANDISHI WA KWANZA NI MUNGU MWENYEWE, NA BAADA YESU MUNGU MKUU ANAKUJA KUWARUHUSU MANABII WENYE HEKIMA KUANDIKA BIBLIA KWA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Krsito Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW