POKEA UKOMBOZI WAKO SASA KWA JINA LA YESU
Fahamu kwamba magonjwa na umasikini siyo mapenzi ya Mungu kwako:
Magonjwa na umasikini au kutofanikiwa, ni sehemu ya LAANA juu ya mtu asiyetaka kuisikiliza sauti ya BWANA Mungu na kufanya maagizo yake [KUMBUKUMBU 28:15-28]. Yesu alifanyika laana kwa ajili yetu kwa kupigiliwa msalabani ili baraka zitufikie [WAGALATIA 3:13-14]. Kwa kupigwa kwake Yesu na hatimaye kusulubishwa msalabani, alitukomboa kutoka katika:-
(a) Dhambi [MATHAYO 26:28; 1 PETRO 2:24].
(b) Magonjwa na udhaifu wote [MATHAYO 8:14-17; ISAYA 53:4-5;
1 PETRO 2:24].
1 PETRO 2:24].
(c) Umasikini [ 2 WAKORINTHO 8:9].
Magonjwa na udhaifu wote, umasikini na dhambi; zote ni kazi za Ibilisi ambazo zilivunjwa na Mwana wa Mungu [1YOHANA 3:8].
Watu tuliookolewa, hatuko tena chini ya laana. Hivyo kama unavyozikataa na kuzipinga dhambi,vivyo hivyo inakupasa kuyakataa na KUYAPINGA MAGONJWA na Udhaifu wote, na kuukataa umasikini. Hivyo usiseme “Labda ni mapenzi ya Mungu niugue” au “Huenda anataka kunifundisha kwa ugonjwa”. Ni mapenzi ya Mungu UWE MZIMA WA AFYA – Yeye anaitwa YEHOVA-RAPHA AU “BWANA NIKUPONYAYE” [SOMA KUTOKA 15:26; YEREMIA 30:17; YEREMIA 33:6; ZABURI 103:3; YOHANA 10:10; 3 YOHANA 1:2].
Mungu ana njia nyingi za kukufundisha. Hakufundishi kwa kumruhusu shetani akuletee magonjwa!
Mungu ana njia nyingi za kukufundisha. Hakufundishi kwa kumruhusu shetani akuletee magonjwa!
Ukisema ni mapenzi ya Mungu uugue, basi ujue unazidi kumpa nafasi shetani akutese zaidi. Mapenzi ya Mungu, ni Neno la Mungu.
Shetani akijua kwamba hulijui neno lililoandikwa, atakutesa! Usimpe nafasi Ibilisi kwa kuzungumza yaliyo kinyume na Neno la Mungu.
Mara zote, yapinge magonjwa ukijua kwa kufanya hivyo unampinga shetani; naye atakimbia. Shetani ndiye mleta magonjwa yote. Shetani ndiye aliyeleta magonjwa juu ya Ayubu na kutofanikiwa kote. Ayubu hakujua akasema ni Mungu! Usiwe kama Ayubu. Mjue mbaya wako Shetani! [Angalia WAEFESO 4:27; YAKOBO 4:7; AYUBU 1:12-16; AYUBU 2:2,7].
Hivyo kumbuka kwamba usitumie “Ikiwa ni mapenzi yako” katika kuomba juu ya ugonjwa.
Tunatumia maneno haya pale tu tusipokuwa na uhakika wa jambo. Uhakika juu ya ugonjwa uko tayari katika Neno. Ni mapenzi ya Mungu uwe mzima.
Shalom
No comments:
Post a Comment