NILETEENI AYA ILI NISILIMU
Katika Surat al a naam Allah anasema yeye alitengeneza Giza na Mwangaza.
Sasa hili giza liliumbwa siku ya ngapi?
Waislam nileteeni aya.
HII AYA INASEMA ALLAH KAUMBA KWA SIKU MBILI (2)
Quran 41:9. Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote.
+
HAPA ALLAH ANAUNGANISHA MAWINGU NA ARDHI KWA SIKU NNE(4)
Quran 41:10. Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza 11. Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu.
+
HAPA ALLAH ANAZITENGENEZA MBINGU KWA SIKU MBILI (2)
Quran 41:12. Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua.
HIZI ZOTE KWA PAMOJA NI SIKU NANE (8)
Siku mbili kwa ajili ya viumbe wa dunia, basi siku nne kujaza ardhi na milima baraka, na chakula kwa ajili ya wakazi wake wote, na mwisho kwa siku mbili zaidi ili kujenga mbingu saba na kujenga nyota yao. Hii inaongeza hadi 2 + 4 + 2 = siku 8 kinyume na siku 6 zilizotajwa katika aya nyingine.
Giza liliumbwa siku ya ngapi? Waislam mbona mnakimbia mada? Nipeni aya ili nisilimu.
Shalom.
No comments:
Post a Comment