KIMENUKA! Mzee wa Kiislam Fadhil Mshamu, mkazi wa Kibaha mkoani hapa anakula Krismasi na Mwaka Mpya wa 2018, akiwa na stresi kufuatia kusomewa shitaka la kumdhalilisha binti yake wa kumzaa jina linahidhiwa kwa sababu za kimaadili.
Kesi hiyo ilitajwa wiki iliyopita ambapo itaanza rasmi kusikilizwa mapema Mwezi Januari, mwakani katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Sheikh Mshamu alikutwa na kasheshe hilo baada ya miezi kadhaa kunaswa akiwa na binti yake wa kumzaa kwenye nyumba moja ya kulala wageni (gesti) huko Kibaha huku kukiwa na madai ya kumtaka kingono.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Sheikh Mshamu alinaswa akiwa na binti yake huyo baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa za kumsumbua kwa muda mrefu akidaiwa kumtaka kimapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya familia ya Sheikh Mshamu, baada ya kunaswa kwenye mtego huo uliowashirikisha polisi na ndugu wa familia hiyo, Juni 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi lilimfungulia Sheikh Mshamu jalada la uchunguzi ambalo lilipelekwa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) ambapo naye baada ya kuiona kesi hiyo, aliamuru ipelekwe mahakamani.
Ndugu huyo wa familia alilieleza gazeti hili kuwa, kufuatia sakata hilo, wiki iliyopita Sheikh Mshamu alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka la kutaka kumdhalilisha binti yake huyo ambaye ni mwanaye wa kumzaa kisha kutajwa tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa mahakamani hapo Januari 2, mwakani ambapo waandishi wetu wataendelea kufuatilia sakata hilo mahakamani hapo na kukuletea habari kamili.
Source Ijumaa
No comments:
Post a Comment