Ndugu yangu msomaji, Hija ni Ibada kubwa kabisa kwa Muislamu ambayo hutakiwa kuifanya angalu mara moja katika maisha yake kwa mwenye uwezo (fedha) na kwa kawaida Hija hii hufanywa katika nchi ya Saud Arabia katika mji wa Makka ambao waislamu wanaitikadi kuwa ndio mji wao mtakatifu. Mwislamu anapokuwa Hija kuna Ibada ya kutoa Kafara (kuchinja) wanyama k.m Ngamia, Kondoo, Mbuzi ili iwe kama fidia ( ransom) kwa dhambi alizofanya.
Katika kitabu kiitwacho “VIPI UHIJI” kilichoandikwa na A.Suleiman uk 22 kinaelezea kafara anayopaswa kuifanya Muhirim anayehiji kwa kufanya mapenzi akiwa Makka,
“Kafara ya Mhirim kwa kufanya Mapenzi ni kuchinja (bila kuchelewa katika siku za hija) Ngamia mwenye umri wa miaka mitano. Ikiwa hutapata Ngamia utachinja ng’ombe, ikiwa hatapata ng’ombe basi kondoo au mbuzi saba, ikiwa hawatapatikana basi atakisia dhamani ya ngamia na kwa dhamani hiyo atanunua ngano na kuwagawia maskini wa Maka. Ikiwa yote hayo hakuweza basi itampas afunge siku moja kwa kila lita 0.51 za ngano ambazo zingeweza kununuliwa katika dhamani ya ngamia”
Hivi ndivyo anavypaswa kutoa kafara Mwislamu akiwa Hija huku akiamini kuwa dhambi alizofanya kwa kufanya Mapenzi zitasamehewa kwa kutoa kafara ya wanyama au ngano (unga) lakini tusomapo Biblia katika
Amosi 5:21,26 Inasema
Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini naam ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, SITAZIKUBALI wala sitaziangalia sadaka zenu za amani na wanyama walionona. Naam mtamchukua Sikuthi mfalme wenu, na Kiuni sanamu zenu, nyota ya mungu wenu mliojifanyizia wenyewe.
Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini naam ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, SITAZIKUBALI wala sitaziangalia sadaka zenu za amani na wanyama walionona. Naam mtamchukua Sikuthi mfalme wenu, na Kiuni sanamu zenu, nyota ya mungu wenu mliojifanyizia wenyewe.
Mwislamu huyu anapokuwa hija pamoja na kuiita kuwa ile ni ibada takatifu ,lakini maneno anayoyatamka siku hiyo ya mwisho wa hija ni maneno ya kukatisha tama sana , kwa sababu yanadhihirisha kuwa pamoja na mambo yote anayoyafanya huyu Mwislamu lakini bado hajapata uhakika wa msamaha wa dhambi zake.
Tunasoma katika kitabu kiitwacho VIPI UHIJI ule Uk.66-67
“Ee Mola nyumba ni yako, mja wako mwana wa waja wako wawili. Umenileta juu ya kiumbe uliyemfanya anitii, kunileta mji wako kunionyesha neema yako ili niweze kutimiza amal zako. Ikiwa umependezwa na mimi, basi zidi zaidi kupendezwa nami.
Ikiwa hujapendezwa nami nibariki hivi sasa kabla nyumbani kwangu na kwahala ninakokwenda hakujawa mbali na nyumba yako. Sasa hivi wakati wa kuondoka umewadia ukiniruhusu. Sitafuti chochote isipokuwa ridhaa yako na nyumba yako. Ewe Mola nipe afya ya kiwiliwili na unihifadhi katika dini yangu. Ifanye hali yangu kuwa bora na unidumishe katika utiifu kwako kwa muda wote utakao niweka hai. Nipe yaliyo bora katika huu ulimwengu na katika akhera kwani wewe ni muweza wa kila kitu”
Rafiki yangu mpendwa Mwislamu napenda nikujulishe kuwa Yesu kama kafara ya Mungu mwenye haki alalipia dhambi zako msalabani. Mkristo ameondolewa na kuwekwa huru katika Hukumu ya Mwisho.Yesu ametufanya tuhesabiwe haki kutoka na mashtaka na lawama aya shetani, Mkristo haishi tena chini ya sheria (sharia) bali anaishi katika neema ya Mungu.
Hawasumbuki kujiokoa wenyewe kwasababu wanae Mwokozi kwa bahati mbaya neno upatanisho (atonement) au wazo linalohusika na wokovu wa neema halimo katika Qur’an na Uislmau kwa ujumla.
Na Mwalimu Chaka wa Musa
For Max Shimba Ministries Org.
No comments:
Post a Comment