Sunday, September 10, 2017

ROHO MTAKATIFU YUPO KILA MAHALI

Image may contain: sky, ocean, cloud, text and nature
Hebu tuangalie kama Roho Mtakatifu ana adhama za Mungu aliye hai. Sifa, moja ya Mungu ni kuwa, yeye yupo kila Mahali. Je, Roho Mtakatifu anayo hii sifa ya kuwa kila mahali? Fungua Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” Daudi anatuambia kwa kupitia Zaburi kuwa, huwezi kumkimbia Mungu.
Daudi anamtaja Mungu na au anamwita Mungu kuwa ni Roho. Hii sifa ya kuwa kila mahali ni ya Mungu pekee, na katika Zaburi 139: 7-8, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu yupo kila mahali. Tuendele na ushahidi zaidi wa kuwa kila mahali; katika Wakorintho wa Kwanza, hapa Mtume Paulo anasema yafuatayo 1 Wakorintho 2 aya ya 10 Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu.
Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake?
Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.” Kama Roho Mtakatifu anafahamu kila kitu kilicho ndani ya Binadamu, ambao wametapakaa Duniani kote, basi kitendo cha kuwa kila mahali kwa wakati mmoja ni Mungu pekee ndie aliye na huo uwezo. Tuendelee kwa Ushihidi mwingine katika aya hiyo hiyo ya 10 ya Wakorintho wa kwanza Sura ya 2. Roho Mtakatifu ni Mungu kwasababu ana akili, hisia, na mapenzi yake. Katika Wakorintho wa kwanza 2:10 tumesoma kuwa Roho Mtakatifu hufikiria na hujua siri iliyo ndani yako. Hii sifa ya kufikiria na kujua, inavunja hoja ya Mashahidi wa Yehova kuwa Roho Mtakatifu ni “Nguvu”. Nguvu haina uwezo wa kufikiria wala kufanya maamuzi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW