Baada ya kuokolewa, tunahitaji pia kutakaswa. Bila utakaso, tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi za ndani katika mawazo, na moyoni, ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda. Dhambi za ndani , ni kama hasira, wivu ,chuki, masengenyo, kugombania ukubwa, kiburi, majivuno, kutokusamehe, kinyongo, kupenda udunia n.k.
Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa: Mawazo yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23), kugombania ukubwa (Luka 22:24-26; Mathayo 20:20-22,25-28; Marko 9:30-37), hasira (Mathayo 20:24) wivu, fitina, ugomvi (Marko 9:38-39; Luka 9:49-50; 1Wakorintho 3:3-5), faraka na matengano (1Wakorintho1:10-13), umimi (Mathayo 28:6-13), kutokusamehe (Mathayo 18:21-35), chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani (Luka 9:51-56; 1Wakorintho 6:1-8); Warumi 7:15 n.k . Mambo haya huondolewa kwa utakaso.
Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka (Yohana 17:14-19).
Roho mtakatifu ndiye atupaye Utakaso (1Wakorintho 6:11; 1Petro1:2)
Je, hujatakaswa, mwambie Roho Mtakatifu akutakase, yeye ni waminifu, atafanya (1Thesalonike 5:23-24)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.
No comments:
Post a Comment