Sunday, September 10, 2017

ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO

Image may contain: fruit, text and food
Katika Wagalatia 5:22-23, tunajifunza juu ya tunda la Roho. Katika lugha ya asili, yote katika mistari hii yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu, Upendo. Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu katika tabia na matendo kama furaha, amani, uvumilivu, utu wema,f adhili, imani, upole, na kiasi. Ni pale tu tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo, ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
Pasipo upendo, tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao, tunakuwa si kitu. Lolote jingine tunalolifanya linakuwa halina faida (1Wakorintho 13:3). Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8) Sasa basi , ni muhimu kufahamu kwamba upendo ni tunda la Roho, tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.
Tukilipokea tunda hili, na kukua kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12), Kama matunda yanavyokua, ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli. Tukiwa na tunda la Roho la upendo, tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa lolote la kimwili (Yakobo1:2). Tutakuwa na amani ipitayo fahamu zote (Wafilipi 4:7) inayotuwezesha kuwa na amani na watu ambao tusingeweza kuwa na amani nao.
Tutakuwa na lengo la kutafuta amani na watu wote wakati wote (Waebrania 12:14) Tutakuwa na uvumilivu wa kipekee katika mateso, makwazo kutoka kwa watu n.k Tutakuwa na utu wema kwa watu wengine hata wale ambao hawajaokoka (Marko 10:17). Tutakuwa na fadhili yaani hali ya kutaka wakati wote watu wanaotuzunguka wawe na furaha.
Tutakuwa watu tuliojaa imani,tusiotetereka kirahisi.Tutakuwana upole yaani unyenyekevu (Mathayo 11:29; Wafilipi2:5-8) Na pili tutakuwa na kiasi (self-control) yaani uwezo wa kukataa kufanya lile ambalo Yesu hataki, kwa gharama yoyote.
Je, unataka kuwa na tunda la Roho katika maisha yako?Mwambie Roho Mtakatifu, naye atafanya.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW