Kama ambavyo Mungu anafahamu mambo yote na anaweza yote, vivyohivyo Roho mtakatifu ni Mungu na anauwezo wa huohuo wa kufahamu yote. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu Kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26). Yohana 14:26 Neno: Bibilia Takatifu (SNT) 26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Katika Yohana hapo juu, tunajifunza kuwa, Roho Mtakatifu yupo nasi kila siku na anaishi ndani yetu. Huu uwezo wa kuishi ndani yetu na kuwa kila mahali, na kufahamu yote ambayo Yesu aliyo tuambia na kutukumbusha, huu uwezo ni wa Mungu na unamfanya Roho Mtakatifu kuwa Mungu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.
No comments:
Post a Comment