Waislamu katika mitandao ya kijamii wamebainisha ghadhabu na hasira zao dhidi ya Utawala wa Saudia kufuatia kitendo cha wanadiplomasia wake kuonyesha kutoheshimu hata kidogo nakala za Qur'ani Tukufu.
Gazeti la Ajel la Saudi toleo la Jumapili limeandika kuwa, kufuatia mvua kali na kuharibika mahala panapowekwa nakala za Qur'ani na vitabu vingine vya kidini, wakuu wa ubalozi waliwaamuru wafanyakazi wachukue vitabu vyote hapo na kuvipeleka sehemu maalumu kwa ajili ya kuviteketeza moto.
Imearifiwa kuwa, vibarua katika ubalozi huo walivipeleka vitabu hivyo, ikiwemo Misahafu, katika eneo la kutupa takataka lakini wakakaidi amri ya wanadiplomasia wa Saudia ya kuviteketeza moto. Ubalozi wa Saudia umewatuhumu wafanyakazi hao kuwa walilenga kuiharibia Saudia jina kwa kusambaza picha hizo katika mitandao ya kijamii.
Tukio hilo la Ubalozi wa Saudia nchini Morocco kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu linaajiri katika hali ambayo nchi hiyo ni mwenezaji mkuu wa itikadi potovu za Kiwahhabi, Kitakfiri na kigaidi duniani. Uwahhabi ni dini rasmi Saudia na kawaida hueneza tafsiri potovu za Uislamu jambo ambalo limepelekea Saudia kuchukiwa na Waislamu wengi duniani.
Mwezi Agosti, zaidi ya wasomi na maulamaa 100 wa Kiislamu kutoka maeneo yote ya dunia walikutana Grozny, mji mkuu wa Jamhuri ya Chechenia na kutangaza kuwa, pote la Uwahhabi si la Kiislamu kama linavodai.
Kikao hicho kilidhudhuriwa na wanazuoni wa ngazi za juu wa Ahul Sunna akiwemo mkuu wa Chuo cha Al Azhar cha Misri Sheikh Ahmad Tayyib, Mufti wa Misri Sheikh Shouqi Alam.
Mkutano huo uliowachukiza sana watawala wa Saudia pia ulihudhuriwa na Maulamaa wa Ahul Sunna kutoka nchi kama vile Syria, Jordan, Sudan, Pakistan, Indonesia, Malaysia na nchi kadhaa za Ulaya.
No comments:
Post a Comment