Sunday, September 10, 2017

KWANINI ALLAH ANAOMBA MSAADA KWA MAKAFIRI?

Image may contain: one or more people, fire and text
Sura Al-Ankabut 29:6
Quran inasema:
Allah hahitaji kusaidiwa na viumbe wake. (bila shaka ni katika kutekeleza makusudi na mipango yake).
LAKINI QURAN HIYO HIYO INAWAAMBIA WAISLAMU:
Sura Muhammad 47:7
Kama mkimsaidia Allah, yeye naye atawasaidia na kuwafanya kuwa imara.
Maswali:
1. Umesema huhitaji msaada, kisha unasema tena unahitaji msaada! Je, Mungu anaweza kufanya jambo kama hilo?
2. Aya hizi zinafanana au zinapingana?
3. Je, hii si ishara kuwa aya hizi zilisemwa tu ili kukidhi mahitaji ya wakati fulani, lakini msemaji alipoona anahitaji kuwafanya watu watende kinyume chake, akajikuta amesema tofauti na alivyosema siku za nyuma?
Na tena quran inasema katika sura Al-Baqara 2:244
Fanyeni vita kwa ajili ya Allah na mkumbuke kwamba anaona yote na anajua yote.
Maswali:
1. Kama kweli Allah hahitaji msaada wa viumbe wake; na kama kweli aliumba ulimwengu wote kwa NENO TU, iweje NENO hilo hilo lisiweze kuwabadilisha wanadamu hadi alazimike kuliingiza ndani yao kwa nguvu, kwa vitisho na kwa ukali namna hiyo?
(Ukristo unashinda na kufanikiwa kwa NENO tu. Maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu wetu. Yeye aliumba kwa Neno; na sisi watoto wake, tunaumba kwa Neno hilo hilo. Tunahubiri tu na watu wanaokolewa, wanaponywa, wanalindwa na kusimama na Mungu wa kweli. Huoni kwamba hii hasa ndiyo maana ya nguvu ya Mungu? Hatuhitaji kuchinja au kupiga watu ili wampende Mungu!! Unawezaje, hata tu wewe mwenyewe, kumfanya mwanao au mkeo akupende kwa njia ya vipigo na kulazimisha? yaani, ukitaka mwanao au mkeo akupende utamshikia rungu au panga au bunduki? Je, hiyo si ishara kwamba wewe huna nguvu ndiyo maana unalazimisha? je, huko si kujikanganya maana umetuambia kuwa wewe ni Mungu unayeweza yote?)
2. Je, Allah anapotaka wanadamu wanaomwamini wafanye vita ili kuwalazimisha wasioamini wamwamini, huko si kutaka msaada kwa viumbe wake?
Ndio maana watu wenye kujitambua wanaukimbia Uislam.
Shalom
Max Shimba Ministries

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW