Thursday, August 17, 2017

YESU MAANA YAKE NI MUNGU MWOKOZI



Jina takatifu la Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yēšū́aʿ, 'Yeshua; yaani "YHWH anaokoa", hivyo "Mungu Mwokozi")
Yesu maana yake ni “Mungu Mwokozi”: alichaguliwa jina hilo kabla hajazaliwa, akitabiriwa kuwa “yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21). “Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12).
Kumbe ndio maana hata kwenye Tito 2:13 “Tukilitazamia tumaini lenye mafunuo ya KRISTO YESU MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU”.
Unaona raha ya kumfuta Mwokozi na Mungu Mkuu?
Mhalifu msalabani alimwita YESU Mungu na kumuomba YESU atakapokuwa katika ufalme wake amkumbuke mharifu huyo”. Luka 23:39-43. Yesu hakukataa kuwa SI MUNGU bali alisema, Amini nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponi.
Ndio maana tutaendelea kusema kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, na Mwokozi wetu maana hayo yote yanawezekana kwa Yesu Pekee.
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW