Tamaa ya asili hutimizwa na kitu halisi:
Kila hitaji asilia hutimizwa na kitu halisia. Njaa huzimwa na chakula. Upweke humalizwa na mpenzi. Kwa kila haja ya kimambile lipo jibu nje ya maumbile husika. Lakini ipo tamaa ya kibinadamu isiyoweza kutoshelezwa na mazingira ya mwanadamu. Elimu ya kidunia na ajira mali na madaraka na mapenzi haviwezi kukidhi haja hiyo. Nani asiyetamani kufurahia ua lisilonyauka, muziki usiochuja, na upendo usiopoa. Nani hana hamu ya kukutana na rafiki pasipo kuagana, kucheka pasipo kulia, na kuzaliwa pasipo kufa? Nani asiyependa kuongea na kusikilizwa, kugusa na kuguswa, kujua na kujulikana, na kupenda na kupendwa. Shauku ya kufaidi uzima katika ukamilifu wake ni kiu halisi ya ulimwengu huu na utimizo wake hupatikana katika uhalisia wake nje ya ulimwengu. Zaidi ya ulimwengu upo uhalisia, Mungu Baba halisi, utimilifu wa tamaa ya vizazi vyote. "Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga,...” (Yakobo 1:17)
BIBLIA NA MATAIFA
Unabii wa Daniel unao mpango wa kuvutia unaohusu kukua na
kuanguka kwa dola, na hali ya mataifa ya kile kilichokuwa kikiitwa 'Dunia iliyostaarabika,' yaani mataifa ya Ulaya, Mashariki ya Kati, Misri na pwani ya kaskazini mwa Afrika, yote yanayoizunguka Bahari ya Kati (Mediterranean sea). Unabii huu ulitolewa wakati Daniel alipokuwa mateka katika boma Babeli karne ya 6 K.K. Ukweli wake umejidhihirisha katika historia tangu siku hizo hadi sasa.
kuanguka kwa dola, na hali ya mataifa ya kile kilichokuwa kikiitwa 'Dunia iliyostaarabika,' yaani mataifa ya Ulaya, Mashariki ya Kati, Misri na pwani ya kaskazini mwa Afrika, yote yanayoizunguka Bahari ya Kati (Mediterranean sea). Unabii huu ulitolewa wakati Daniel alipokuwa mateka katika boma Babeli karne ya 6 K.K. Ukweli wake umejidhihirisha katika historia tangu siku hizo hadi sasa.
Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akiwa amejaa kujikinai na ufahari, aliona katika ndoto sanamu moja kubwa sana ya mtu, yenye sehemu tano (tazama uk. 16,17):
1. Kichwa cha sanamu kilikuwa cha dhahabu.
2. Kifua chake na mikono kilikuwa cha fedha.
3. Tumbo lake na mapaja lilikuwa la shaba.
4. Miguu yake miwili ilikuwa ya Chuma.
5. Lakini nyayo na vidole zilikuwa mchanganyiko wa chuma na udongo wa mfinyanzi.
2. Kifua chake na mikono kilikuwa cha fedha.
3. Tumbo lake na mapaja lilikuwa la shaba.
4. Miguu yake miwili ilikuwa ya Chuma.
5. Lakini nyayo na vidole zilikuwa mchanganyiko wa chuma na udongo wa mfinyanzi.
Kisha jiwe likatokeza 'lililokatwa kutoka mlimani bila kazi ya mikono.' Likaangukia nyayo za sanamu ile, likaiangusha yote chini, na kuzisaga sehemu zake kuwa unga, kiasi kwamba upepo ukaupeperushia mbali. Baada ya hapa lile jiwe likakua kuwa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.
Nebukadreza alisumbuliwa sana na hatima ya sanamu ile, kwa sababu hakuna kati ya watu wake wajuzi aliyeweza kumwambia ilikuwa na maana gani. lakini Daniel, nabii wa Israel alimwambia "kuna Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho "Dal. 2:28
Kwa hiyo Daniel alielezea maana ya sanamu ile. Kichwa cha dhahabu kiliwakilisha utawala wa Nebukadreza mwenyewe. Ulikuwa ufuatiwe na mwingine, wa hali ya chini zaidi (kifua na mikono ya fedha); na baada ya huo wa tatu (wa shaba); alafu wa nne (miguu ya chuma) ambao ungekuwa na nguvu na kishindo, lakini nyayo na vidole viliwakilisha falme zilizogawanyika, nusu nguvu na nusu dhaifu". (Ms. 37 - 42)
Kitu kimoja ni wazi: Sanamu hii iliwakilisha makabidhiano ya falme zenye nguvu, na sio vigumu kuzitambua. Wa kwanza tunafahamu; ulikuwa ni dola ya Babeli. Katika kifungu cha 8 (Mstari wa 20 - 21) tunaambiwa afuataye angekuwa Mwajemi na Myunani. Dola ya nne, ' kuu na inayotisha', haikutajwa wazi wazi katika unabii wa Daniel. Historia inathibitisha tabiri hizi kwa wingi. Kama 530 K.K. mamlaka ya Babeli iliangushwa na Wamedi na Waajemi, ambao mwishoni walianzisha dola ya kiajemi. Ilidumu miaka 200, na baadaye kuangushwa kama 330 K.K. na Aleksanda Mkuu (Alexander the Great) aliyesimamisha dola ya Kiyunani.
Ni dola gani kubwa iliyofuata falme za mrithi wa Aleksanda? Hakuna mashaka juu ya jibu: ilikuwa dola ya Rumi. Warumi walivamia maeneo ya iliyokuwa dola ya Kiyunani kuanzia karne ya 2 K.K. na kuendelea. Kwa miaka 500 iliyofuata, Rumi ilikuwa mamlaka kuu kuliko zote duniani. Dola yake ilitanda kama sehemu yote ya dola zile tatu, na kuenea mbali ndani ya Ulaya, Mashariki ya Kati na nchi zote zinazozunguka Mediterranean. Walifanikisha uvamizi wao kwa ukatili mwingi kama ilivyodokezwa na maneno "nguvu kama chuma." Katika karne zake mbili za mwisho za kuwepo kwake, iligawanyika sehemu mbili: ya magharibi makao yake makuu yakiwa Rumi, na ya mashariki makao yake makuu yakiwa Constantinople - miguu miwili ya ile sanamu.
Mungu anayefunua siri
Lakini ni nini kilichotokea baada ya dola ya Warumi kuvunjika katika karne ya 5 B. K. Haikufuatiwa na dola nyingine yoyote kuu, na kwa kweli haijakuwapo dola ya tano ya kulinganishwa kimamlaka, pamoja na kuwepo jitihada kubwa za watu wenye tamaa kuunda nyingine. Maeneo ya dola ya Kirumi yalimeguka kutokana na uvamizi wa makabila jeuri ya Kihan, Kigoti, Kivisigoti na Kivandali, yaliyoanzisha tawala zao wenyewe tofauti. Mataifa ya sasa ya Ulaya yametokana na falme hizo. Katika kipindi chote cha historia ya miaka 1500 mpaka sasa, mataifa hayo yamebakia katika mgawanyiko, kama ilivyoashiriwa na nyayo za ile sanamu - nusu chuma na nusu udongo: " nusu una nguvu, na nusu yake umevunjika ... hawatashikamana. "(Dan. 2:42-43)
Angewezaje Daniel kujua kuwa mamlaka ile kuu ya Nebukadreza ingefuatiwa na zingine tatu, ya nne ikiwa na nguvu zisizo za kawaida, ambayo kamwe isingelifuatiwa na ya tano? Angejuaje kuwa baada ya ile ya nne kuanguka, watu wake wangesambaratika kuwa nchi zilizomeguka, zisizo na umoja kati yake? Kwa vyovyote, kwa yeye mwenyewe asingeweza kujua kitu, wala yeyote mwingine. Lakini Daniel hatuachi bila maelezo:
"Yupo Mungu mbinguni afunuaye siri.. Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye, na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti." (Ms. 28,45)
"Yupo Mungu mbinguni afunuaye siri.. Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye, na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti." (Ms. 28,45)
Unawezaje kuuelezea uwepo wa unabii wa Daniel 2, karne kadhaa K.K, na bado kuwa na mtizamo sahihi wa madola na mataifa mpaka hivi leo, baada ya zaidi ya miaka 2000? Kama kweli kuna 'Mungu mbinguni,' unaweza kuelewa. Kama Hayupo, hakuna maelezo yanayoridhisha.
Tutatoa maoni katika sehemu ya hitimisho, juu ya jiwe linaloigonga ile sanamu miguuni na kuiangusha yote chini. Kwa ajili ya mfano wetu wa mwisho wa kinabii tuone kwanza.
====USIKOSE SEHEMU YA KUMI ==== NYAKATI TULIZO NAZO
Ingawa unabii tuliouzingatia mpaka sasa umeendelea kutimia hadi hivi leo, ulihusu zaidi matukio ya siku nyingi za nyuma (ukiacha urudishwaji upya wa Waisraeli hivi karibuni katika ardhi yao ya kale).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment