Usemi wenyewe hudai uwepo wake:
Usemi wowote uletao maana hupangika kisarufi bila kugongana kimantiki. "Duara ni pembe tatu" Sarufi? Sawa. Maana? Hakuna. “Mungu hayupo” huangukia hukumu hiyo hiyo. Vichwani mwetu, "Mungu" ni Yeye astahiliye kuabudiwa kwa kuwa ni Mkamilifu katika uweza na uadilifu. “Mungu” ataitwa Mungu kwa kuwa yupo. Mrembo aliyeko kwenye jeneza si mrembo, na “Mungu” asiyekuwepo si “Mungu.” Kusema, ‘"Mungu” hayupo’ ni kumhesabu Aliye hai miongoni mwa wasio hai. Mtu huthubutu vipi kusema “Mungu hayupo” kama hajateleza ulimi pasipo kujitambua? (Zaburi 51:1-2;14:1-2). “Duara ni nyuzi 360” na “Mungu yupo” ni tungo mbili sahii kwa muundo na maana zake.
HATIMA YA MISRI
Misri iliwahi pia kuwa dola yenye nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati. Ukubwa wake ulikuwa kama 1600 (K.K) wakati majeshi ya Mafarao wavamizi walipojisogeza kusini ndani ya Sudani, Magharibi kuambaa pwani ya Afrika ya kaskazini, kaskazini kupita ardhi ya Kaanani (baadaye Israeli), na ndani ya Syria. Uvumbuzi kaatika baadhi ya Mahekalu ya kale, minara na makaburi umedhihirisha utukufu wa Mafarao ulivyokuwa katika kilele cha kuu wao.
Lakini ilipofikia miaka ya 1400 K.K nguvu ya Misri ilianza kurudi nyuma kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukua kwa Ashuru, na baadaye Babeli. Hata hivyo katika kipindi Waisraeli walipokuwa wakiikalia Kanaani, 1400-600 K.K, Wamisri waliingilia kati kwa nyakati mbalimbali siasa za Mashariki ya Kati, kwa mafanikio fulani. Waisraeli, walipokuwa wakiogopa uvamizi kutoka Ashuru na Babeli mara kwa mara walishawishika kutafuta msaada Misri badala ya kumtumainia Mungu wao.
Sasa manabii wa Israeli walikuwa na kitu maalum sana kusema juu ya hatima ya Misri. Nabii Ezekiel, ambaye matamko yake yalitolewa katika siku za Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kuanzia kama 600 K.K, alitangaza kwamba kutokana na hukumu ya Mungu, Misri ingekuwa upweke kwa miaka 40. Baada ya hapo kungekuwa na uamsho, lakini usiofikia ukuu wa nguvu zake za awali.
"Maana Bwana MUNGU aseme hivi; Mwisho wa miaka arobaini
nitawakusanya Wamisri, na kuwatoa katika hizo kabila za watu, ambazo walitawanyika kati yao; nani nitawarudisha hata nchi ya Pathrosi, hata nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni (ufalme wa chini).

Utakuwa duni kuliko falme zote; wala hatajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza ili wasitawale tena juu ya mataifa... Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu (Memphis), wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri. Ezk. 29:13-15; 30:13
Hapa napo maana ya unabii huu inaeleweka: Misri ingekabiliwa na matatizo ya uvamizi na watu kuchukuliwa mateka. Ingawa hakuna kumbukumbu halisi zilizobakia za matukio hayo, lazima yatakuwa ni matokeo ya uvamizi wa Wababeli kwa Misri, kama Ezekiel mwenyewe alivyotabiri (tazama Ezek: 30:17-20). Lakini huo usingekuwa mwisho wa Misri. Maana baada ya miaka 40, mateka wangerudi tena katika nchi yao wenyewe. Misri, kama ufalme usingeangamizwa: ungedumu lakini nguvu yake ingeshushwa sana - "Ufalme mdogo," usioweza kutumainia nguvu zake kukabili mataifa yanayopakana nayo tena.
Ufalme mdogo
Na ndivyo ilivyotokea. Tangu kama mwaka 600 K.K, Misri aliangukia chini ya watawala wa kivamizi, kwanza wa Wababeli katika karne ya 6 K.K; kisha Waajemi kati ya karne ya 6 na 4; alafu Wayunani katika karne ya 4; wakifuatiwa na Warumi karne ya kwanza K.K mpaka karne ya 5 B.K. Walifuatiwa na Waarabu na Waturuki kutoka karne ya 7 B.K na kuendelea. Hata Waingereza wameitawala Misri kwa kipindi katika karne ya 19. Kwa miaka 2500, Misri imebakia kama alivyotabiri Ezekiel kuwa ingekuwa, "Ufalme wa chini," wakati wote ikikaliwa na wengine. Lakini Misri na Wamisri hawakutokomea. Bado wapo, na wameponea uhuru kiasi miaka ya karibuni, washukuru misaada mikubwa ya fedha wanayopata kutoka Marekani na Saudi Arabia.

Tuweke pembeni kidogo mawazoni swala la Misri wakati tukiangalia mfano wa tatu wa utabiri wa Biblia wa matukio ya mbele, kwa kutazama.
==== USIKOSE SEHEMU YA SABA==== UNABII KUHUSU ISRAELI
Huu ndio uliojaa kuliko wote, kimaelezo ya utabiri wake, na pia katika wingi wa thibitisho zihusuzo ukweli wake kimatukio kihistoria.
Huu ndio uliojaa kuliko wote, kimaelezo ya utabiri wake, na pia katika wingi wa thibitisho zihusuzo ukweli wake kimatukio kihistoria.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment