Tuesday, August 22, 2017

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA SABA)

Image may contain: 1 person, text


Madhara ya Kiroho unapo angalia ponografia:
Ponografia husababisha madhara mabaya ya kiroho. Inaweza kuwa kizuizi kikubwa kwa mtu anayetaka kuwa na uhusiano na Mungu.* Biblia huhusianisha hamu ya ngono na tamaa na ibada ya sanamu. (Wakolosai 3:5) Mtu anayetamani kitu huwa na hamu kubwa sana ya kukipata hivi kwamba kinakuwa jambo kuu maishani mwake kuliko vitu vingine vyote. Kwa kweli, wale ambao wamezoea ponografia hutanguliza tamaa zao za ngono badala ya Mungu. Kwa hiyo wanazifanya kuwa sanamu yao. Amri ya Mungu inasema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.”—Kutoka 20:3.
Ponografia huharibu mahusiano yenye upendo. Mtume Petro, ambaye alikuwa amefunga ndoa, aliwahimiza waume Wakristo wawaheshimu wake zao. Mungu hatasikiliza sala za mume anayekosa kufanya hivyo. (1 Petro 3:7) Je, mtu anayetazama picha chafu za wanawake faraghani anamheshimu mke wake? Mke angehisije akigundua? Na Mungu ambaye “ataleta hukumuni kila kazi” na ambaye “huzipima roho” angeonaje? (Mhubiri 12:14; Mithali 16:2) Je, mtu anayetazama ponografia anaweza kumtarajia Mungu asikilize sala zake?
Ponografia hukazia kutosheleza tamaa za mtu binafsi kwa vyovyote vile. Kwa hiyo, kutazama ponografia ni kukosa upendo. Hudhoofisha uwezo wa Mkristo wa kudumu akiwa safi kiadili na kuwa mwadilifu mbele za Mungu. “Haya ndiyo mapenzi ya Mungu,” akaandika mtume Paulo, “kwamba mjiepushe na uasherati; kwamba kila mmoja wenu apaswe kujua jinsi ya kupata umiliki wa chombo chake mwenyewe katika utakaso na heshima, si katika hamu yenye tamaa ya ngono . . . , kwamba yeyote asifikie hatua ya kudhuru na kuziingilia haki za ndugu yake.”—1 Wathesalonike 4:3-7.
Ponografia huwatumia vibaya hasa wanawake na watoto. Huwavunjia heshima na pia huwashushia hadhi na kuwanyima haki zao. Yule anayetazama ponografia hushiriki na kuunga mkono matumizi hayo mabaya ya wanawake na watoto. ‘Hata mtu akijiona kuwa mwema kadiri gani,’ wasema watafiti Steven Hill na Nina Silver, ‘anapotazama au kukubali ponografia, anakuwa asiyejali au hata mwenye chuki kuelekea mtu anayedai eti anamjali.’
USIKOSE SEHEMU YA NANE
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW