Wednesday, August 16, 2017

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: text
Nini maana ya ponografia?
Neno “ponografia”—linalotokana na maneno ya Kigiriki pornē na graphos yanayomaanisha “kuandika kuhusu makahaba.” Leo ponografia inafafanuliwa kuwa kuonyesha tabia za kimahaba katika vitabu, picha, sanamu, sinema, na kadhalika, kwa kusudi la kuamsha nyege.”
Ingawa watu wengi hawaoni kosa lolote au hatari ya kutazama ponografia, Biblia haiungi mkono maoni hayo. Inasema waziwazi kwamba matendo yetu yanaongozwa sana na mambo tunayojaza akilini mwetu. Mwanafunzi Mkristo Yakobo anaonyesha kwamba “kila mmoja hujaribiwa kwa kuvutwa na kutongozwa na tamaa yake mwenyewe. Kisha tamaa, wakati imetungika mimba, huzaa dhambi.” (Yakobo 1:14, 15) Yesu alisema: “Kila mtu ambaye hufuliza kumtazama mwanamke ili kuwa na harara kwa ajili yake tayari amefanya uzinzi pamoja naye moyoni mwake.”—Mathayo 5:28.
Kufikiria mambo ya kingono isivyofaa kunaweza kuathiri ibada yetu kwa Mungu. Hiyo ndiyo sababu Paulo aliandika hivi: “Kwa hiyo, fisheni viungo vya mwili wenu . . . kwa habari ya uasherati, ukosefu wa usafi, hamu ya ngono, tamaa yenye kuumiza, na tamaa, ambako ni ibada ya sanamu.”—Wakolosai 3:5.
Katika andiko hilo Paulo alionyesha kwamba hamu ya ngono inahusiana na tamaa, ambayo ni kutaka sana kuvipata vitu usivyokuwa navyo. Tamaa ni namna ya ibada ya sanamu. Kwa nini? Kwa sababu yule anayetamani huweka kitu anachotamani mbele ya mambo mengine yote, hata Mungu. Ponografia huamsha tamaa kwa ajili ya kitu ambacho mtu hana. “Unatamani maisha ya kingono ya mtu. . . . Huwezi kuwa na jambo jingine akilini ila tu kutamani kile ambacho huna. . . . Kile tunachotamani, tunakiabudu,” akasema mwandishi mmoja wa mambo ya kidini.
USIKOSE SEHEMU YA PILI.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW