Je, wewe ni tawi la Mzabibu unao zaa?
Watu tuliookolewa, ni matawi ya Mzabibu wa Kweli. Yesu Kristo ndiye mizizi na shina. Kutoka kwake tunapata uzima. Chakula, maji na madini mengine hutoka chini kwenye mizizi na kupanda juu kwenye matawi. Uzima au uhai wetu unatokana na Yesu. Wokovu wetu hutoka kwake. Ikiwa tawi linaonekana kijani kibichi linapendeza, kupendeza huko hutokana na mizizi.
Yohana 15:1-8:
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.

Mtu yeyote anayedai kwamba ameokoka, lakini hazai matunda tuliyojifunza; huyu ni tawi lisilozaa. Hukatwa na kuondolewa, na kutupwa motoni. Ili tupate uzima wa milele, hatuna budi kuishi wakati wote maisha yanayoonyesha matunda.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.
No comments:
Post a Comment