Bibilia inatuamuru kuwa tusihiruhusu miili yetu “itawaliwe” na kitu cho chote. (1 Wakorintho 6:12). Uvutaji bila kukana ni mazoea. Baadaye kwa ujumbe huo huo tumeambiwa, “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:19-20). Uvutaji bila shaka unadhuru afya yako. Uvutaji umethibitishwa kuwa unaharibu mapafu na moyo.
Acheni tuchunguze madhara matatu yanayojulikana sana ya kuvuta sigara na tuone maoni ya Biblia.
HUSABABISHA URAIBU
Tumbaku ina kemikali iitwayo nikotini ambayo husababisha uraibu haraka zaidi. Nikotini husisimua na vilevile kutuliza hisia. Kuvuta sigara hupeleka nikotini haraka kwenye ubongo tena na tena. Mvuto mmoja wa sigara ni sawa na dozi moja, hivyo mvutaji wa kawaida anaweza kuvuta dozi 200 kwa siku, ambacho ni kiwango cha juu kuliko dawa yoyote ile. Ndiyo maana nikotini husababisha uraibu mkubwa sana. Mtu aliyezoea kuvuta sigara hujihisi vibaya anapokawia kuvuta.
Biblia inatusaidia kuelewa jambo hilo inaposema hivi: “Je, hamjui kwamba ikiwa mnaendelea kujitoa wenyewe kwa yeyote kuwa watumwa ili kumtii yeye, ninyi ni watumwa wake kwa sababu mnamtii yeye?” (Waroma 6:16) Mtu anapofikiria kila mara kuhusu kuvuta sigara, anakuwa mtumwa wa tabia chafu. Hata hivyo, Mungu, ambaye jina lake ni Yehovana sio Allah, anataka tuwe huru, si uhuru tu wa kuepuka madhara ya kimwili bali pia madhara ya kiroho, yaani, mtazamo wetu wa akili. (Zaburi 83:18; 2 Wakorintho 7:1) Hivyo, mtu anapojifunza kumpenda na kumheshimu Mungu, anatambua kwamba Mungu anastahili kilicho bora na kwamba hawezi kumtumikia Mungu huku akiwa mtumwa wa tabia inayodhuru. Mtu akitambua ukweli huo atachochewa kuepuka tamaa mbaya.
Olaf, anayeishi Ujerumani alianza kuvuta sigara alipokuwa na umri wa miaka 12, na alifanikiwa kushinda zoea hilo lililodumu miaka 16. Alisema hivi: “Nilipovuta sigara mara ya kwanza sikuona ubaya wowote. Lakini baada ya miaka kadhaa ikawa vigumu sana kuacha. Siku moja sikuwa na sigara, nilikata tamaa hivi kwamba nikakusanya vipande vya mabaki ya sigara na kutengeneza sigara kwa kutumia karatasi. Ninapokumbuka jambo hilo ninaaibika sana.” Aliachaje kuvuta sigara? Anasema hivi, “Jambo lililonisaidia ni tamaa yangu ya kumpendeza Yehova. Niliacha kabisa baada ya kujifunza kuhusu upendo wa Mungu kwa wanadamu na tumaini la wakati ujao.”
USIKOSE SEHEMU YA PILI === KUVUTA SIGARA HUHARIBU MWILI===
Jarida The Tobacco Atlas linasema hivi: “Kuvuta sigara . . . kumethibitishwa kisayansi kwamba kunadhuru karibu viungo vyote mwilini na husababisha magonjwa na kifo.”
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.
No comments:
Post a Comment