Huu ni mwendelezo wa sehemu ya 1 na 2. Aisha anamuuguza Mohammad na Jibril anamuombea kwa Allah amnusuru na sumu aliyoila.
KUMBUKA: Imenukuliwa kutoka kwa Ibn Sa’d (ukurasa 250) Mohammad alijaribu kujitibu kutokana na sumu aliyotiliwa kwenye chakula.
Kutoka kwa Ibn Sa'd, ukurasa 263
Hakika, wakati wa ugonjwa wake, mtume alisoma "al-Mu'awwadhatayn" [Sura 113, and 114], na kujipulizia hewa huku akisugua uso wake (hii ilifanyika kwa nia kuwa apone).

Kutoka kwa Sahih Muslim Juzuu 3, # 5440
Aisha alisimulia kuwa mtume wa Allah alipougua, aliswali Mu’awwidhatan kwenye mwili wake na ugonjwa ulipozidi nilimswalia na kumkanda nikitumai kuwa atapona.

Kutoka kwa Ibn Sa'd, ukurasa 265
Mtume wa Allah aliugua na Jibril akamswalia akisema, “Kwa jina la Allah naomba kila kitu kinachokudhuru akizuie mwenye wivu na kijicho, na Allah atakuponya.”

Aisha, mke wa mtume alikuwa akisema, “Mtume wa Allah alipougua, Jibril alimswalia akisema, ‘Kwa jina la Allah ambaye atakuponya katika maradhi yote na kukuepusha na macho mabaya ya ibilisi mwenye wivu.’

Bukhari's Hadith 5.713:
Amesimulia Aisha; mtume akiwa anaumwa, kabla ya kufa, alisema, “Ewe Aisha! Ninahisi maumivu yanayosababishwa na chakula nilichokila kule Khaibar, na wakati huu, ninahisi ni kama mshipa wa moyo wangu unakatwa na hiyo sumu.”

Kisha ugonjwa wa mtume ukawa mbaya zaidi na akateseka kwa maumivu makali. Akasema, “Nimwagilie mwilini ngozi saba za maji kutoka kwa visima tofauti ili niende kwa wafuasi wangu na niwape maagizo.” Tukamfanya akae kwenye karai la Hafsa d. Umar na tukamwagilia maji haki akasema, “imetosha, imetosha!”
Kutoka kwa Ibn Sa'd ukurasa 322:
Huku siku za mwisho za mtume zikikaribia, alikuwa akivuta shuka na kufunika uso wake; lakini alipohisi vibaya, alijifunua na kusema: “Hukumu ya Allah iwe juu ya Wayahudi na Wakristo ambao walifanya makaburi ya mitume yao sehemu za ibada.”

Kutoka kwa Ibn Sa’d ukurasa 239
Siku ya kifo cha mtume ilikuwa imekaribia na aliamriwa aswali akirudiarudia ‘tasbih’ (utukufu) na amwombe Allah msamaha.

TATHMINI:
Aisha alimuuguza Mume wake huku akimwombea kwa Allah apone kutokana na kula nyama ya mbuzi (vitabu vingine vinasema ni kondoo) iliyotiwa sumu. Malaika Jibril pia alimwombea kwa Allah. Alitumia madawa ili apone lakini yote hayo hayakufua dafu. Huku siku zake za mwisho zikikaribia, Mohammad alijawa na uchungu mwingi. Aliwalaani Wayahudi na Wakristo na kumwomba Allah awaadhibu.
***SEHEMU YA NNE ITAKUJA HIVI KARIBUNI***
No comments:
Post a Comment