Tuesday, August 22, 2017

JE, MUNGU ANATAKA NINI KUTOKA KWAKO? SEHEMU YA KWANZA

Image may contain: one or more people and text
Ukisoma kitabu cha Mika, unaweza kufikiri mwanzoni kwamba ni orodha ndefu ya mashtaka dhidi ya Waisraeli walioasi. Bila shaka, Mungu aliona kuzorota kwa maadili ya watu wake waliokuwa wamejiweka wakfu, kutia ndani watu aliowaita: ‘Wanaochukia yaliyo mema na wanaopenda ubaya.’ (Mika 3:2; 6:12) Hata hivyo, mbali na kuwashutumu waziwazi, alitoa mojawapo ya mahimizo yenye kugusa moyo na yenye kuchochea zaidi katika Biblia. Mika anakazia uangalifu Chanzo cha viwango vya uadilifu, kisha anauliza swali hili lenye kuchochea fikira: “Mungu anataka nini kutoka kwako ila kutenda haki na kupenda fadhili na kuwa na kiasi katika kutembea na Mungu wako?”—Mika 6:8.
Je, unaona jinsi Muumba wetu anavyotusihi katika andiko hilo?
Anatukumbusha kwa upendo mambo yanayofaa tunayoweza kufanya badala ya kujiruhusu tukengeushwe na uovu uliopo.
Mungu anajua kwamba ushikamanifu wetu hutuchochea kusitawisha sifa kama zake, naye ana hakika kwamba tunaweza kufanya hivyo.
Ungejibuje kama ungeulizwa hivi: ‘Mungu anataka nini kutoka kwako?’
Je, unaweza kutaja mambo fulani maishani mwako yanayoongozwa au yanayopasa kuongozwa na viwango vya Mungu vya maadili?
Uhusiano wako na Mungu na maisha yako yatakuwa bora zaidi ukiendelea kufuata viwango hivyo. Unapoendelea kutazamia paradiso duniani, himizo hili na likutie moyo: “Mjipandie mbegu kwa uadilifu; mvune kulingana na fadhili zenye upendo. Mjilimie udongo unaofaa kwa kilimo, kukiwa kungali na wakati wa kumtafuta Mungu mpaka atakapokuja na kuwatolea ninyi mafundisho kwa uadilifu.” (Hosea 10:12) Hebu sasa tuchunguze mambo fulani makuu kutokana na shauri zuri la Mika 6:8.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: text
Leo, ponografia imeenea sana na kukubaliwa na watu wengi katika jamii ya kisasa. Wakati mmoja ponografia ilipatikana katika sinema fulani tu za kimahaba na katika mitaa ya makahaba, lakini sasa imeenea kwa wingi katika jamii nyingi. Nchini Marekani pekee, ponografia ni biashara inayochuma zaidi ya dola bilioni kumi kila mwaka!
Biblia inatuhimiza hivi: “Mambo yoyote yaliyo safi kiadili, mambo yoyote yaliyo ya kupendeka, mambo yoyote yaliyo ya kusemwa vema, wema wa adili wowote ulioko . . . endeleeni kufikiria mambo haya.” (Wafilipi 4:8) Mtu anayetazama ponografia na kuijaza akilini mwake analikataa himizo la Paulo. Ponografia haina kiasi kwa sababu inafunulia watu wote mambo ya siri na ya faragha. Ni tendo la kipumbavu kwa sababu linamshusha mhusika na kushusha heshima. Hilo si tendo la upendo kwa kuwa halichangii hali ya kuwajali wengine. Hilo hukazia tu tamaa ya mtu binafsi.
Kwa kuonyesha matendo yasiyo ya kiadili na yaliyopotoka kingono, ponografia hudhoofisha na kuharibu jitihada ya Mkristo ya ‘kuchukia mabaya.’ (Amosi 5:15) Ponografia huwatia watu moyo kufanya dhambi na ni kinyume kabisa cha himizo la Paulo kwa Waefeso la kuacha ‘uasherati na ukosefu wa usafi wa kila namna au pupa hata visitajwe hata miongoni mwao, kama vile ifaavyo watu watakatifu; wala mwenendo wa aibu wala kufanya mzaha wenye aibu, mambo yasiyofaa.’—Waefeso 5:3, 4.
Kwa kweli ponografia haikosi kuleta madhara. Hiyo hutumikisha na kufisidi. Inaweza kuharibu mahusiano mazuri, na kupotosha njia ya kiasili ya kuonyesha ukaribu wa kingono kuwa uraibu wa kutazama picha za kiponografia. Hiyo huharibu akili na hali ya kiroho ya mraibu. Hiyo hukuza ubinafsi, pupa na kumfanya mtu kuwaona wengine kama vyombo tu vya kutosheleza tamaa zao. Hiyo huharibu jitihada ya mtu ya kufanya mema na kuwa na dhamiri safi. Jambo baya hata zaidi, ponografia inaweza kuathiri vibaya au hata kuharibu kabisa uhusiano wa mtu wa kiroho pamoja na Mungu. (Waefeso 4:17-19) Kwa kweli, ponografia ni janga linalopasa kuepukwa.—Mithali 4:14, 15.
USIKOSE SEHEMU YA TATU
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

KILA MUISLAM ANA JINI KATIKA MWILI WAKE

Image may contain: 1 person, beard and text
MUHAMMAD AKIRI KUCHEZEWA NA SHETANI
Abu Huraira alisema, "nilimsikia Nabii wa Allah akisema, Hakuna kiumbe ambaye hakuguswa na Shetani, ndio maana mtoto hulia kwa sauti kubwa wakati wa kuzaliwa kwasababu Shetani anakuwa amemgusa, ISIPOKUWA Mariyam na Mwanae Yesu, wao hawakuguswa na Shetani. Kisha Abu Huraira akasema : " Na najikinga na Wewe kwa ajili yake na kwa ajili ya watoto wake kutoka kiwa Shetani" (3.36)
Ndugu zanguni, Muhammad leo amekiri kuwa, YESU hakuwai kuguswa na Shetani lakini yeye na Waislam wote wameguswa na kuchezewa na Shetani.
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa "Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa na shetani tangu alipozaliwa, (Fat'hul Baary Juzuu ya 6 Uk. 389).
Je, kuna ushahid wowote ule kuwa Muhammad alitolewa Shetani? Kama upo Basi Waislam, tuleteeni tuuone.
BAADA YA KUTOKA PANGONI,
Basi Mtume akafanya khofu, akarejea kwa mkewe, akamhadithia, na pale pale homa kubwa kabisa, ikampanda, akataka afunikwe maguo, akawa anatetemeka kwa ngerema, na kuweweseka, na kusema, "Najikhofia nafsi yangu, kuchezewa na mashetani, na kuniharibu akili yangu na kunizuga"(Kitabu cha maisha ya Nabii Muhamaad s.a,uk.17 kilichoandikwa na Sheiky A.Farsy).
KUFUATANA KITABU CHA MAISHA YA NABII MUHAMMAD, tunajifunza kuwa Muhammad kwa mara ya kwanza kabisa alipata utume wake pangoni baada ya NAFSI YAKE KUCHEZEWA NA MASHETANI.
MASWALI:
(i). Kama Jibril ndie alitumwa na Allah, na huyo Allah ni Mungu, kwanini Muhammad alisema kuwa nafsi yake imechezewa na MASHETANI baada ya kukutana na Jibril?
(ii). Kama Jibril alitoka kwa Allah, kwanini Muhammad alipo toka pangoni alisema kuwa Jibril AMEMZUGA AKILI YAKE?
Majini wamepewa ruhusa ya kukaa katika mwili wa Muislam yeyote, hivyo kila Muislam ana Jini kuanzia moja na kuendelea. Vile vile Majini wameruhusiwa kukaa katika nyumba za Waislam. Katika nyumba yoyote ya Muumini wa dini hiyo, kuna Jini au Majini wanaokaa humo. Ni ukweli usiopingika kuwa bila Majini hakuna Uislamu kama vile pasipo Roho Mtakatifu hakuna Ukristo. Majini ndiyo yaliyomchukua mtume Muhammad kwa muda wa siku 40 akiwa Mabondeni walikompeleka na kuanza kumuagiza kuhusiana na kuanzisha imani hiyo ya Kiislamu.
Pia hiamini kuwa Majini wana uwezo wa kuzaa na Wanadamu. Soma Quran 17:64. Waislamu huamini kwamba mtu anauwezo wa kuoa au kuolewa na Jini bila kujua, na mwanadamu anauwezo wa kumuua Jini. Soma Quran 57:14-15
Suratul Jinn
Ndani ya QURAN pia imo sura inayoitwa Suratuljinn (QURAN 72). Sura hiyo huitwa hivyo kwa sababu ni sura ya Majini (Mapepo).
Kwa nini wanatajwa Majini katika imani ya Kiislamu?
SASA WAISLAM, NIONYESHENI, wapi kwenye Taurat, au Zaburi au Injili kama kuna Mtume aliye na sifa za ajabu kama za Muhammad.
Karibuni kwa Yesu ambaye ndie Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni.
SHETANI ANAWAPULIZA WAISLAM MSIKITINI
Kasema Mtume (s.a.w) “Anamwijia mmoja wenu shetani katika sala, basi anapuliza (anampuliza) katika matako yake, basi yule mtu inamwijia fikiria ya kuwa umemtoka upepo (kajamba) nae haukumtoka, basi akiona hali hiyo asiondoke kwenye sala mpaka asikie sauti ya kumtoka huo upepo au anuse harufu yake”. (KITABU CHA MKWELI MWAMIU, JUZUU YA 1 -2 HADITHI NA. 74, UK 42)
Muhammad anasema: Shetani anaingia msikitni na kuwachezea Waislam kama ushahidi unavyo sema hapo juu.
Kwanini mfuate dini ambayo inaongozwa na MASHETANI Msikitini?
Kwanini Shetani ana mamlaka ya kuwapuliza Waislam matako yao tena wakiwa Msikitini?
Karibuni kwa Yesu ambaye hakuwai guswa na Shetani kama alivyo kiri Muhammad.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries Org,

YESU MAANA YAKE NI MUNGU MWOKOZI



Jina takatifu la Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yēšū́aʿ, 'Yeshua; yaani "YHWH anaokoa", hivyo "Mungu Mwokozi")
Yesu maana yake ni “Mungu Mwokozi”: alichaguliwa jina hilo kabla hajazaliwa, akitabiriwa kuwa “yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21). “Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12).
Kumbe ndio maana hata kwenye Tito 2:13 “Tukilitazamia tumaini lenye mafunuo ya KRISTO YESU MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU”.
Unaona raha ya kumfuta Mwokozi na Mungu Mkuu?
Mhalifu msalabani alimwita YESU Mungu na kumuomba YESU atakapokuwa katika ufalme wake amkumbuke mharifu huyo”. Luka 23:39-43. Yesu hakukataa kuwa SI MUNGU bali alisema, Amini nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponi.
Ndio maana tutaendelea kusema kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, na Mwokozi wetu maana hayo yote yanawezekana kwa Yesu Pekee.
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: one or more people and people standing
TAFADHALI SOMA KISA HIKI CHA KUSISIMUA
Mara nyingi Waislam wamekuwa wepesi kuwaambia watu wengine kuwa Mungu ameruhusu Biblia kupotoshwa. Kitu wanachodokeza ni kuwa Kurani leo hii ni neno la Mungu lenye kuaminika wakati ambapo Biblia sivyo. Biblia ina maandiko yanayotofautiana mengi yenye tofauti ndogo, lakini ushahidi wa mabadiliko ya mafundisho hauna uzito. Kurani ina ushahidi mkubwa zaidi wa kupotoshwa kwa mujibu wa Ubai, aya zilizobatilishwa‘Uthman, na matatizo mengine ya Kurani. Hata hivyo, tofauti kubwa zaidi ya mafundisho ya Kurani, iliyoletwa na Waislam wenyewe, ni "mabinti wa Allah."
Muhtasari
Tovuti ya Kikristo http://answering-islam.org/Responses/Saifullah/sverses.htm inasema, "Moja ya matukio yenye kuaibisha zaidi kwenye maisha ya Muhammad lilitokea wakati Shetani alipoweka maneno yake kwenye mdomo wa Muhammad. Muhammad alisema maneno ya Shetani kama neno la Mungu. Tukio hili limethibitishwa kwa maandishi na waandishi kadhaa wa Kiislam wa kale na limeongelewa kwenye Hadithi na Kurani. Waislam wa miaka iliyofuata, kwa kujisikia aibu kuwa nabii wao aliyejitangaza mwenyewe amesema maneno ya Shetani, walikana kuwa tukio hili lilitokea. Visingizio na kukana kwingi vimekuwa vikitolewa na hawa Waislam wa miaka iliyofuata ili kulifunika kosa lenye kuhusisha dhambi la Muhammad.
Ni muhimu ikafahamika tena kuwa tukio la ‘Aya za Shetani’ si jambo ambalo limetungwa na watu wasiokuwa Waislam. Tukio hili limerekodiwa na vyazo vya kale zaidi vya Kiislam vilivyokuwepo wakati wa uhai wa Muhammad. Mtu yoyote asifikiri kuwa jambo hili ni hadithi iliyotungwa na watu wenye kuupinga Uislam. Ni kisa kinachopatikana moja kwa moja kwenye rekodi za kale za Kiislam.
Hili moja ya masomo yenye kubishaniwa zaidi kwenye Uislam. Shetani alimsababishia Muhammad kunena maneno yake (Shetani) kama maneno ya Mungu."
Je Kurani Ilisema Nini Mwanzoni?
Sura ya Nyota (Sura 53) mistari ya 19-20 inasema, "Je umemwona Lat, na ‘Uzza, Na mwingine, (mungu mke) wa tata, Manat?"
Allah alikuwa maarufu huko Arabia kabla ya kuja kwa uislam, kama mungu aliyekuwa na mabinti watatu: al-Lat, al-Uzza, na Manat. (Kumbuka kuwa al- inamaanisha ‘yule’, kwa Kiingereza "the".)
Waandishi wanne wa mwanzo wa maisha ya Muhammad waliandika kuwa awali aya hizi zilifuatwa na:
"Hawa ni mawinchi (wasuluhishi) ambao maombi yao yanapaswa kutumainiwa"
Tafsiri: Mabinti wa Allah walifikiriwa kuwa viumbe wa mbinguni wenye kuomba kwa ajili ya wengine. Mawinchi marefu ya Kinumidia ilikuwa ni sitiari yao. Maneno mbadala ya "inatakiwa kutumainiwa" (turtaja) ni "imekubaliwa kwa kuthibitishwa" (turtada). (Kutoka kwenye tafsiri ya Alfred Guillaume ya The Life of Mohammed, iliyoandikwa na Ibn Ishaq, uk.166.
Baadaye, kifungu hiki kiliondolewa na kifungu kifuatacho kiliwekwa badala yake:
"Nini! Kwako wewe mwenye jinsia ya kiume, Na kwake (mwanaume), mwanamke? Tazama, hakika mgawanyo huu hautakuwa wa haki kabisa." (aya za 53:21-22 leo)
Tafsiri: Wale wanaoamini kuwa Allah alikuwa na mabinti watatu hawakuntendea haki Allah, kwa sababu walipendelea watoto wa kiume ingawa walisema kuwa Allah alikuwa na wasichana tu.
Hizi ndizo ambazo zimeitwa "Aya za Shetani." Katika nyakati za sasa Salmon Rushdie alitumia msemo huu tu kwenye kichwa cha riwaya yake ya kubuniwa na isiyohusika na aya hizi, na andiko hili halikiongelei kisa hiki cha kisasa. Kwa upande wa Aya za Sheatani za asili, Muislam au mtu mwingine asiyekuwa Muislam mwenye kutazama jambo hil bila upendeleo anawezaje kujua aya ambazo zilikuwemo toka awali? Sehemu iliyobaki ya andiko hili inatoa ushahidi wa moja kwa moja na ule usio wa moja kwa moja kuwa Aya za Shetani zilikuwemo asilia, na mapingamizi tisa ya Kiislam.
Waandishi Wanne wa Maisha ya Muhammad: Ushahidi wa Moja kwa Moja
Ingawa si kila kitu Waislam wa kale walichosema kuhusu Muhammad kilikuwa kweli, wanazuoni wa kiislam wana uwezekano mkubwa zaidi wa kukubali mambo ambayo Muhammad aliyasema ambayo yameshuhudiwa na vyanzo vitatu au zaidi. Tunajua kuwa Aya za Shetani hazikutokana na vyanzo visivyokuwa vya kiislam, lakini kutoka wanazuoni wanne tofauti wa kale wa kiislam ambao walikuwa waandishi wa maisha ya Muhammad. Kumbuka kuwa watatu kati ya waandishi hawa walisimulia maisha ya Muhammad hata kabla ya mkusanyiko mashuhuri wa Hadithi ambao dhehebu la Kiisuni limejengeka juu yake.
Al-Wahidi/Wakidi (aliyekufa mwaka 207/823 BK) aliandika Asbab al-Nozul. "Kwenye siku fulani, wakuu wa Maka, walikusanyika kwenye kundi pembeni mwa Kaaba, walijadili kama ilivyo kawaida ya mambo ya mji wao; wakati Muhammad alipotokea na, kukaa karibu yao kwa namna ya kirafiki, alianza kusema sura 53 huku wakimsikia…. ‘Na usimwangalie Lat na Ozza, na Manat wa tatu zaidi?’ Alipofika kwenye aya hii, mwovu alipendekeza njia ya kujieleza mawazo yake ambayo iliitawala nafsi yake kwa siku nyingi; na aliweka mdomoni mwake maneno ya upatanisho na masikilizano, ufunuo aliokuwa anausubiri kwa hamu kubwa sana toka kwa Mungu, yaani; ‘Hawa ni wanawake waliotukuka, na hakika maombezi yao yanatakiwa kutumainiwa. ’ Wakoreish walishangazwa na kufurahishwa na kukubaliwa huku kwa miungu yao; na kama Mahomet alivyoimalizia Sura kwa maneno ya hitimisho ‘Kwa hiyo inama mbele ya Mungu, na mtumikie’ kusanyiko zima lilijiinamisha kwa moyo mmoja chini na kuabudu. … Jioni Gabriel alimtembelea; na nabii aliisema Sura hiyo kwake. Na Gabriel alisema, ‘Umefanya kitu gani? Umeyarudia mbele ya watu maneno ambayo sikuwahi kukupa’. Kwa hiyo Muhammad alisononeka zaidi …"
Ibn Sa’ad/Sa’d (aliyekufa mwaka 230/845 BK), aliifahamu kazi ya al-Wahidi lakini yeye mwenyewe alikuwa mwandishi wa habari za maisha ya watu aliyeandika kitabu chenye juzuu 15 kiitwacho Kitab al Tabaqat al Kabir.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Shalom,

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA TATU)


UASHERATI NI NINI?
“Uasherati” ni nini, na ni kwa njia gani wale walio na mazoea ya kufanya uasherati huvuna kile wanachopanda?
Katika Biblia, neno “uasherati” (Kigiriki, por·neiʹa) linahusu mahusiano haramu ya ngono nje ya ndoa ya Kimaandiko. Linatia ndani uzinzi, ukahaba, ngono kati ya watu ambao hawajaoana, ngono ya kinywa, ufiraji au ulawiti, na kusisimua kingono viungo vya uzazi vya mtu mwingine ambaye si mwenzi wako wa ndoa. Pia linatia ndani mazoea kama hayo kati ya watu wa jinsia moja au kati ya mtu na mnyama. *
Maandiko yanataja waziwazi: Walio na mazoea ya kufanya uasherati hawawezi kuendelea kuwa katika kutaniko la Kikristo na hawatapata uzima wa milele. (1 Wakorintho 6:9; Ufunuo 22:15) Pia, wanajiletea wenyewe madhara makubwa hata sasa. Wanakuwa watu wasiotumainika, wanajidharau, wanakuwa na mizozo katika ndoa zao, wanakuwa na dhamiri chafu, wanapata mimba zisizotakikana, magonjwa, na hata kifo. (Wagalatia 6:7, 8) Kwa nini uanze kutembea katika barabara hiyo yenye hatari nyingi? Inasikitisha kwamba wengi hawafikirii madhara yanayoweza kutokea kabla ya kuchukua hatua ya kwanza isiyofaa, ambayo mara nyingi hutia ndani ponografia.
MADHARA YA PONOGRAFIA—HATUA YA KWANZA
Je, ni kweli kwamba ponografia haina madhara yoyote kama wengine wanavyodai?
Katika nchi nyingi, ponografia hupatikana katika magazeti, muziki, televisheni, na imejaa katika Intaneti. Je, ni kweli kwamba haina madhara yoyote kama wengine wanavyodai?
Sivyo hata kidogo! Mara nyingi wale wanaotazama ponografia husitawisha mazoea ya kupiga punyeto na kukuza “hamu za ngono yenye kufedhehesha,” mambo ambayo yanaweza kusababisha pupa ya ngono, tamaa potovu, matatizo mazito katika ndoa, na hata talaka. (Waroma 1:24-27; Waefeso 4:19) Mchunguzi fulani analinganisha pupa ya ngono na ugonjwa wa kansa. Anasema: “Hukua na kuenea daima. Uwezekano wa kupungua ni mdogo sana nayo haitibiki wala kupona kwa urahisi.”
Fikiria maneno haya yaliyo katika andiko la Yakobo 1:14, 15: “Kila mtu hujaribiwa kwa kuvutwa na kushawishiwa na tamaa yake mwenyewe. Kisha tamaa, wakati imetunga mimba, huzaa dhambi; nayo dhambi, wakati imetimizwa, huleta kifo.” Kwa hiyo tamaa mbaya ikiingia akilini mwako, iondolee mbali mara moja! Kwa mfano, ukiona bila kukusudia picha zenye kuamsha hamu ya ngono, angalia kando haraka, au uzime kompyuta, au ubadili stesheni ya televisheni. Fanya yote unayoweza ili kuepuka kulemewa na tamaa zilizopotoka kabla hazijaenea sana na kupita mipaka!—Mathayo 5:29, 30.
USIKOSE SEHEMU YA NNE
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

MAADUI ZAKO WOTE WAMESHINDWA KWA JINA LA YESU.

Image may contain: 1 person, text
Ni amri kuliamini Jina la Yesu Kristo – sio ombi
“Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.” (1 Yohana 3:23)
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. (Yohana 3:18)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

JE, MUNGU ANATAKA NINI KUTOKA KWAKO? SEHEMU YA PILI

Image may contain: 2 people, child and outdoor
DUMISHA VIWANGO VYA JUU VYA MAADILI
Umejionea mambo gani kuhusiana na maadili ya ulimwengu leo?
Maadili ya Kikristo muhtasari wake umetolewa na Wakolosai 3:1-6 : "Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkon wa kuum wa Mungu.
Roho Mtakatifu hukaa ndani ya kila muumini, na sehemu ya majukumu yake ni kufundisha jinsi ya kuishi: "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia,"(Yohana 14:26). "Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yankaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama matufa yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake"(1 Yohana 2:27). Hivyo, wakati tunaomba kwa maandiko, Roho atatuongoza na kutufundisha. Atawaonyesha sisi kanuni tunahitaji ili kusimama katika hali yoyote.
Mungu anatuagiza tuwe safi kiadili licha ya uovu ulio katika ulimwengu kwa sababu anataka tuwe na hali nzuri ya kiroho na kimwili. (Malaki 2:15) Ulimwengu umejaa habari nyingi sana za ngono. Watu wengi wana maoni ya kwamba kutazama picha na sinema za ngono, kusoma vichapo vyenye mambo machafu ya ngono, na kusikiliza muziki unaoamsha ashiki ni mambo ya kawaida ya maisha. Isitoshe, kuna watu wasiowaheshimu wanawake, wanawaona kuwa vyombo vya ngono tu. Au huenda vijana shuleni wakafanya mizaha michafu na kusema mambo machafu kuhusu ngono. Utashindaje mikazo hiyo yenye kuchafua?
Wengi walikosaje kudumisha viwango vya Mungu wakati wa wale manabii 12?
Wale manabii 12 tunaozungumzia wanatoa mashauri mazuri sana. Waliishi kabla ya kubuniwa kwa majumba ya sinema na maduka ya video. Hata hivyo, wakati huo kulikuwa na ishara za viungo vya uzazi, kulikuwa na ule ulioitwa ukahaba mtakatifu, na matendo mapotovu sana ya ngono. (1 Wafalme 14:24; Isaya 57:3, 4; Habakuki 2:15) Mambo ambayo manabii waliandika yanathibitisha hivyo: “Kwa habari ya wanaume, hujiendea zao wenyewe pamoja na makahaba, nao hutoa dhabihu pamoja na wanawake makahaba wa hekaluni.” “Mwanamume na baba yake wamemwendea msichana yuleyule, kwa kusudi la kulitia unajisi jina langu takatifu.” Baadhi yao walitoa kwa ukawaida “malipo ya kahaba” katika sherehe za uzazi.* Uzinzi ulienea kotekote, huku wake na waume wasio waaminifu ‘wakiwafuata wale wanaowapenda kwa tamaa nyingi.’—Hosea 2:13; 4:2, 13, 14; Amosi 2:7; Mika 1:7.
(a) Mwenendo mpotovu husababishwa na nini hasa?
(b) Watu wa kale wa Mungu walitumbukiaje katika uasherati wa kiroho?
Huenda unajua kwamba upotovu wa maadili unahusiana na mtazamo na nia ya mtu. (Marko 7:20-22) Kuhusu watu wake wenye maadili mapotovu, Mungu wetu alisema kwamba “roho ya uasherati [“tamaa ya ngono,” Contemporary English Version] imewafanya watange-tange” na kwamba “wameendeleza mwenendo mpotovu.” (Hosea 4:12; 6:9) Zakaria alitaja “roho ya uchafu.” (Zakaria 13:2) Watu walikuwa na mtazamo wa kutojali, walipuuza au hata kudharau viwango vya Mungu na mamlaka yake. Kwa hiyo, mtu yeyote mwenye mwelekeo huo anapaswa kubadili kabisa fikira zake na hali yake ya moyoni ili arekebishe nia yake. Wakristo wanapojua hivyo wanapaswa kuthamini hata zaidi jitihada zinazofanywa ili kuwasaidia waepuke ukosefu wa maadili na madhara yake.
USIKOSE SEHEMU YA TATU
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu

KAMA ALLAH SIO MUNGU WA KIPAGANI, KWANINI BABA YAKE MUHAMMAD AMBAYE ALIKUWA MPAGANI ALIITWA ABDULLAH?

Image may contain: one or more people, crowd and text
(Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.
Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?
Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozo wetu.

KAMA UNAMPENDA RAFIKI YAKO, MWAMBIE UKWELI AMBAO NI MCHUNGU

Image may contain: one or more people and text
Wengi tumejikuta tukiona ni vyema tukaambiwa yasiyo na ukweli maishani mwetu na kudanganywa ilimradi tu yanaturidhisha wakati huo lakini ajabu tunachukia na kutopenda ukweli ambao hata kama unaumiza lakini faida yake ni kubwa sasa na pia mbele twendako.
MITHALI 27: 5 Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika. 
6 Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
7 Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
Huwa natumiwa lawama kila siku, kwanini natoa mada chungu kwa Waislam kila siku?
Leo nimewajibu wale wote wanao ulizo hilo swali kwa kutumia aya.
Ukweli unaweza kukumiza lakini, kwa kusema uongo unaweza kuumia milele,Ni wazi kuwa watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, na wakati mwingi baadhi ya watu husema uongo huku wakifikiri kufanya hivyo ni kujipa matumaini katika jambo fulani, lakini ukikaa na kufikiria unaposema uongo au unapokataa ukweli ujue unajidanganya mwenyewe na siku zote utabaki kuwa na maumivu moyoni mwako kutokana na kuishi na uongo ndani ya moyo wako.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

MUHAMMAD ALIPEWA UTUME NA MKEWE KHADIJA

Image may contain: 1 person, smiling, text
Alipokuwa pangoni alichezewa na Shetani: Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya:
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
Katika tukio hili lililompata Muhammad akiwa pangoni , ndipo Waislamu wote ulimwenguni wanapolieleza kuwa hapo ndipo Muhammad s.a.w alipoletewa wahyi (ufunuo) na kupewa unabii na utume. Lakini unapotafakari juu ya ujumbe huo utaona kuwa hata yeye mwenyewe hajui nini kilichokuwa kimemtokea kule pangoni.
Ndiyo maana tunasoma kuwa alipofika nyumbani kwake mkewe Bi. Khadija alimfunika nguo mumewe akidhani ana homa. Muhammad alimweleza mkewe kilichomtokea kuwa ni “Shetani” hakumsema malaika yeyote kama Waislamu wanavyotaka kutuaminisha leo. Kwa sababu kama angekuwa ni malaika kama tunavyosoma ndani ya Biblia, asingesita kujitambulisha kwa Muhammad kuwa yeye ni nani. Hii ni hoja ya kwanza.
Mwisho wake Bi Khadija akamsimika UTUME Mume wake Muhammad.
Leo umejifunza kuwa Muhammad alipewa utume na Mkewe.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
www.maxshimbaministries Org

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: text
Ibn Isaq/Ishaq (aliyekufa mwaka 145/767 au 151/773 BK) alikuwa Msuni wa mlengo wa Kishafi ambaye baadaye alianzisha shule yake mwenyewe iliyodumu kwa muda mfupi. Aliandika kitabu kiitwacho Sirat Rasullallah (Maisha ya Nabii wa Allah). "[Wahamiaji] walibakia sehemu ileile waliyokuwepo [Ethiopia] hadi waliposikia kuwa watu wa Maka wameukubali Uislam na wamejinyenyekeza. Hii ilikuwa ni kwa sababu sura ya Nyota [Sura 53] ilikuwa imetumwa kwa Muhammad na mtume aliinena. Mtu mmoja Muislam na mwenye kuamini miungu wengi alisikiliza kimya hadi alisema maneno haya ‘Je umemwona al-Lat na al-uzza?’ Walimsikiliza kwa uangalifu sana wakati waumini walimwamini [nabii wao]. Baadhi yao waliiasi imani yao walipoisikia ‘saj’ ya Shetani na kusema, ‘Kwa uwezo wa Allah tutawatumikia (mawinchi) ili kwamba watulete karibu na Allah.’ Shetani alifundisha aya hizi mbili kwa kila mtu aliyekuwa anaamini miungu wengi na ndimi zao zilizielewa kwa urahisi. Jambo hili lilimsunbua Mtume hadi Gabriel alipokuja kwake na kulalamika …." (Anaelezea mlolongo wa kuenea kuwa Yazid bin Ziyad-> Muhammad bin Ishaq -> Salama -> Ibn Hamid -> ibn Isaq
Ibn Jarir al-Tabari (aliyekufa mwaka 923 BK) alikuwa Msuni wa mlengo wa Kishati aliyeandika kitabu chenye juzuu 38 cha Kiislam cha Historia ya ulimwengu hadi mwaka 915 BK. Alipewa jina la "shehe wa wafafanuaji." Anaandika kwenye juzuu ya 6 uk.108-110, "Mjumbe wa Mungu alipoona jinsi kabila lake lilivyomkataa na kuhuzunishwa alipowaona wanauacha ujumbe aliowaletea toka kwa Mungu, alitamani moyoni mwake kuwa kitu chochote kimjie toka kwa Mungu ambacho kitampatanisha na kabila lake …. Na alipoyafikia maneno: ‘Je umewafikiria al-Lat na al-Uzza na Manat, wa tatu, Yule mwingine?’ Shetani alimlaumu, kwa sababu ya midahalo yake ya ndani na vitu alivyokusudia kupeleka kwa watu wake, maneno: ‘Haya ni mawinchi yanayopaa juu zaidi; hakika maombezi yao hupokelwa kwa kuthibitishwa [kwa mpokezano: kuhitajiwa au kutegemea].’ Waquraysh waliposikia hili, walifurahi sana na kupendezwa na namna alivyosema kuhusu muingu yao, na walimsikiliza, wakati Waislam, wakiwa wanamwamini kabisa nabii wao kuhusu ujumbe aliouleta kutoka kwa mungu, hawakumshuku kuwa amepotoka, anaota, au kafanya makosa. … Kisha [baadaye] Gabriel alikuja kwa Mjumbe wa Mungu na kusema, ‘Muhammad, umefanya nini? Umenena kwa watu kitu ambacho sikukuletea toka kwa Mungu …’"
Wanazuoni wa Kiislam wa miaka ya mbele waliosema jambo hili:
Abu Ma’shar kutoka Chorassan (787-885 BH)
Ibn Abi Hatim
Ibn al-Mundhir
Ibn Hajar from Asqalaan (773-852 BH)
Ibn Mardauyah
Musa ibn ‘Uqba
Ufafanuzi mashuhuri sana wa Zamakhshari wa Sura 22:52. (1070-1143 BH)
Wanazuoni sita ni kwa mujibu wa kitabu kiitwacho The Book of the Major Classes, kilichotafsiriwa na S. Moinul ‘Haq.
Ushahidi usiokuwa wa moja kwa moja wa Aya za Shetani:
Kurani na Hadithi
Bukhari alikufa karibu na mwaka 870 BK (hata miaka mitatu baada ya vyanzo vitatu kati ya vinne vilivyoorodheshwa.) Wakati Muhammad alipoisema Sura ya Nyota, wapagani na Waislam walisujudu. (Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 19 na.173, uk.100 juzuu ya 3 kitabu cha 19, na.176, uk.101; juzuu ya 6 kitabu cha 60 na.385-386 uk.364-365; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 481 na.1401, uk.369). Wapagani hawasemekani kusujudu kwa ajili ya Muhammad kusema maneno mengine yoyote, ni kwa nini wakubaliane kiasi hiki na sura hii, hasa kwa vile Bukhari na Abu Dawud hawasemi kuwa hao wapagani waliwahi kuwa Waislam, na hii ilikuwa kabla ya vita na hawa wapagani wa Maka!
Pia, Sura 22:52 inasema, "Hatukuwahi kumtuma mtume au nabii Kabla yako, lakini, alipoumba nia, Shetani alimtupia (ubatili) kiasi kwenye nia yake: lakini Mungu atafuta kitu chochote (batili) ambacho Shetani anatupia ndani, na Mungu atafanya dhahiri (na kuthibitisha) Ishara Zake…"
Sura 17:73-75 inasema, "Na lengo lao lilikuwa kukujaribu na kukupeleka mbali na jambo tulilolifunua kwako, kuweka badala yake kitu tofauti kabisa kwa kutumia jina letu: (Kwa ajili hiyo), tazama! Watakuwa wamekufanya kuwa rafiki (yao)! Na je hatujakupa wewe, ungeweza kuelekea upande wao kiasi. Katika hali hiyo tulipaswa kukufanya uonje mara mbili (ya adhabu) kwenye maisha haya, na kiasi kama hichohicho mautini: na zaidi ya hapo usingepata mtu wa kukusaidia dhidi yetu!"
Kumbuka kwamba ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa Sura 17:73-75 ilifunuliwa wakati wa "Kupaa kwa Nabii", Tabari na Ibn Sa’d waliandika kuwa Sura 17:73-75 ilifunuliwa karibu na wakati wa aya za Shetani. Waislam hata wana neno maalum la kunong’oneza kwa Shetani, ambalo matamshi yake yanafanana na "wiswas".
USIKOSE SEHEMU YA TATU
Shalom

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA NNE)

No automatic alt text available.
YOSEFU ALIUKIMBIA UASHERATI
Yosefu alishawishiwa jinsi gani, naye alifanya nini?
Yosefu, ndugu-nusu ya Dina, aliyekuwa kijana mzuri aliyempenda Mungu, aliukimbia uasherati. (Mwanzo 30:20-24) Alipokuwa mtoto, Yosefu aliona matokeo mabaya ya upumbavu wa dada yake. Inaonekana kukumbuka mambo hayo, na vilevile kutamani kukaa katika upendo wa Mungu, kulimlinda Yosefu miaka mingi baadaye huko Misri wakati mke wa bwana wake alipokuwa akijaribu kumshawishi “siku baada ya siku.” Bila shaka, kwa sababu Yosefu alikuwa mtumwa, hangeweza kuacha kazi na kuondoka! Ilimbidi ashughulikie hali hiyo kwa hekima na uhodari. Alifanya hivyo kwa kukataa tena na tena vishawishi vya mke wa Potifa, na mwishowe, kwa kumkimbia.—Mwanzo 39:7-12.
Fikiria hili: Ikiwa Yosefu angetumia muda mwingi akiwaza kuhusu mwanamke huyo au kuwaza-waza juu ya ngono, je, angeendelea kuwa mtimilifu? Haielekei angeweza. Badala ya kuwazia daima mambo yasiyofaa, Yosefu alithamini uhusiano wake pamoja na Yehova, jambo ambalo lilionekana wazi katika maneno ambayo alimwambia mke wa Potifa. Alisema: “Bwana wangu . . . hakunizuilia chochote ila wewe, kwa sababu wewe ni mke wake. Basi ninawezaje kufanya ubaya huu mkubwa na kwa kweli nimtendee Mungu dhambi?”—Mwanzo 39:8, 9.
Mungu alielekeza mambo jinsi gani katika kisa cha Yosefu?
Wazia shangwe ambayo Mungu alikuwa nayo alipomwona kijana Yosefu akiendelea kuwa mtimilifu siku baada ya siku, ingawa alikuwa mbali na familia yao. (Methali 27:11) Baadaye Mungu alielekeza mambo ili Yosefu afunguliwe kutoka gerezani na vilevile kuwa waziri mkuu wa Misri na msimamizi wa chakula! (Mwanzo 41:39-49) Jinsi yalivyo kweli maneno haya ya Zaburi 97:10: “Enyi mnaompenda Mungu, chukieni yaliyo mabaya. Yeye anazilinda nafsi za washikamanifu wake; huwakomboa kutoka katika mkono wa waovu”!
USIKOSE SEHEMU YA TANO
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

YESU NI MUNGU MUUMBAJI

Image may contain: text
Sifa ya kuumba niya Mungu peke-yake (Yohana 1:3,14) “vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Naye Neno alifanyika mwili; nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli”.
Yesu anaitwa Neno la Mungu (Ufunuo 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(Yohana 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote. Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine.
Katika yeye (Yesu) vitu vyote viliumbwa (Wakolosai 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana; vya Mbinguni na vya duniani.
Maandiko yako wazi kabisa, na kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi kuwa Yesu ni Mungu.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

MAMLAKA ULIYONAYO UNAPOLITUMIA JINA LA YESU KRISTO!

Image may contain: text
“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” (Wafilipi 2:9-11)
Kwa mistari hii michache tunaona ya kuwa jina la Yesu kristo lina mamlaka MBINGUNI, DUNIANI na CHINI YA NCHI au KUZIMU.
“Kwa jina la Yesu kila goti lipigwe” maana yake jina la Yesu lipate heshima linavyostahili kila mahali.Likiwa mojawapo ya funguo za ufalme wa mbinguni, jina la Yesu linatupa MAMLAKA mbinguni, duniani na chini ya nchi.
Kwa mfano: tunaokolewa kwa jina la Yesu (matendo ya mitume 4:12). Tunazaliwa mara ya pili kwa jina la Yesu (Yohana 1:12). Kwa maneno mengine kwa sababu ya jina lake, Yesu alisema; “Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu” (Yohana 16:23-24)
Mtu anapata furaha iliyo timilifu anapoomba kwa jina la Yesu Kristo! Kwa nini? Kwa sababu akiomba kwa jina la Yesu Kristo – anapata kile alichoomba. Heshima yote hii ya kujibiwa maombi yetu na Mungu Baba inatokana na Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na mwokozi wetu. Yesu Kristo alisema, “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.” (Yohana 12:26)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu

KORAN NI SAWA NA TANGAZO LA VITA

Image may contain: one or more people and text
Dhana ya Kiislamu ya Amani, kwa maana ya kufanya ulimwengu kuwa wa Kiislamu, ni mipango ya kishetani kwa ajili ya kufanya vita na kumwaga damu. Ilikuwa si jambo la kufikirika kuwa siku moja Ugaidi wa Kishetani utaweza ingia kwenye Nchi za Kistaarabu, kwa kupitia njia ya "dini" ya amani, nikimaanisha Uislam. Maantiki ya fikra yakinifu katika Uislamu ni tofauti na ile ya Wastani wa Mtu ..., nikimaanisha, katika Uislam, kuuwa kwao ndio amani wanayo itangaza.
Mtu KAMWE hawezi kuuacha Uislamu, unajua, wale ambao waliiuacha Uislam na kujiunga na Imani zingine, wale hawakupigwa Muhuri wa kwenda Jehanamu. Maana Allah ameahidi Jehanamu kwa Waislamu wote Soma: Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike. Kuukacha Uislam na kuingia kwenye hekima hilo ni kosa la kifo katika dini ya amani/Islam. Hapo ndipo panaanza kufanya mtu afikirie, Je, kweli Koran ni kitabu cha Mungu? Mbona kuna kulazimishana kwenye hii dini?
Hivyo, hii ni sehemu ya mantiki hiyo hiyo ya kuwa, Mtu ambaye anabadili dini na au shirika kama vile Al Shabaab au Uislamu ni tu kama nilivyoeleza, mtu wa namna hiyo hakupigwa Muhuru wa kwenda Jehannam na Allah, anyway. Hivyobasi, huyu mtu ni Msaliti na akikamatwa basi aelewe kuwa kifo kipo mkonini mwake, kwa kuikacha dini ha Amani/Islam.
Mwenye akili lazima ataelewa kuwa amani ya Allah na Muhammad ni vita na umwagaji damu. Hakuna jema kwenye hii dini ya Jibril zaidi ya kutangaza kifo kwa makafiri.
Shalom,

USIOGOPE, SIMAMA IMARA KWENYE MWAMBA WA MILELE

Image may contain: one or more people, sky, text, outdoor and nature
Isaya 26: 4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.
Simama imara maana Yesu Mungu Mkuu ni MWAMBA WAKO na hakuna "Mapepo au Majini au Mashetani au Nguvu za giza" zinakazo kutetemesha.
Kumbuka, Mwamba ni Yesu na upo juu yako.
Barikiwa sana ndugu.
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

KAA NDANI YA YESU, NAYE ATAKAA NDANI YAKO

Image may contain: food
Je, wewe ni tawi la Mzabibu unao zaa?
Watu tuliookolewa, ni matawi ya Mzabibu wa Kweli. Yesu Kristo ndiye mizizi na shina. Kutoka kwake tunapata uzima. Chakula, maji na madini mengine hutoka chini kwenye mizizi na kupanda juu kwenye matawi. Uzima au uhai wetu unatokana na Yesu. Wokovu wetu hutoka kwake. Ikiwa tawi linaonekana kijani kibichi linapendeza, kupendeza huko hutokana na mizizi.
Yohana 15:1-8:
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.
Mtu yeyote anayedai kwamba ameokoka, lakini hazai matunda tuliyojifunza; huyu ni tawi lisilozaa. Hukatwa na kuondolewa, na kutupwa motoni. Ili tupate uzima wa milele, hatuna budi kuishi wakati wote maisha yanayoonyesha matunda.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUUMBWA KWA VITU VYOTE DUNIANI NA MBINGUNI



Wakolosai 1:17 “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote; na vitu vyote hushikamana katika yeye”.

Yesu Kristo alikuwako kabla ya Ibrahimu kuwako (Yohana 8:52-58).
Watu walioambiwa maneno hayo na Yesu mwenyewe waliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwa anakufuru. Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho. (Yohana 4:24).Yohana 17:5,24.Waebrania 7:3.
Yesu ni Alfa na Omega, wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (Ufunuo 22:13).
Shalom
Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu.

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA TANO)

Image may contain: text


Madhara Yanayosababishwa na Ponografia:
Habari ya kila aina kuhusu ngono inapatikana kwa urahisi kupitia televisheni, sinema, video za muziki, na Internet. Je, ni kweli kwamba habari hizo chungu nzima za ponografia hazina madhara, kama watu wengi wanavyotaka tuamini?*
Jinsi Ponografia Inavyowaathiri Watu Wazima:
Hata watetezi waseme nini, ponografia inaathiri sana maoni ya watu kuhusu ngono na maadili. Watafiti kwenye Hazina ya Taifa ya Utafiti na Uelimishaji wa Jamii walikata kauli kwamba “kutazama ponografia kunaweza kuwafanya watazamaji wafanye ngono potovu.” Ripoti hiyo inasema “imani ya kwamba wanawake husababisha na hufurahia ubakaji, na kwamba wabakaji ni watu wa kawaida imeenea sana miongoni mwa wanaume wenye zoea la kutazama ponografia.”
Watafiti fulani wanasema kwamba kuzoea kutazama ponografia kunaweza kuathiri uwezo wa kufurahia na kufanya ngono katika ndoa. Dakt. Victor Cline, mtaalamu wa kutibu watu wanaotawaliwa na mambo ya ngono, ametambua kwamba watu wanaotazama ponografia huendelea tu bila kuacha. Mtu anayeanza kutazama ponografia kidogo-kidogo, asipoacha mwishowe anaweza kuwa na zoea la kusoma habari na kutazama picha chafu zaidi za ponografia. Cline anadai kwamba zoea hilo linaweza kuongoza kwenye matendo mapotovu ya ngono. Wanasayansi wanaochunguza tabia za wanadamu wanakubaliana na jambo hilo. Dakt. Cline anaripoti kwamba “upotovu wowote wa ngono unaweza kuanza hivyo . . . na kwamba mtu hawezi kuacha hata akisumbuliwa sana na dhamiri.” Hatimaye, huenda mtu anayetazama ponografia akajaribu kufanya mambo yasiyo ya adili aliyoona, na mara nyingi matokeo huwa mabaya.
Tatizo hilo linaweza kuanza hatua kwa hatua bila kutambuliwa, asema Cline. Aongeza: “Huongezeka na kuenea kama kansa. Kwa kawaida zoea hilo halikomi, wala haliwezi kutatuliwa kwa urahisi. Haishangazi kwamba mara nyingi wanaume waliozoea kutazama ponografia hawakubali kwamba wana tatizo, na ni kawaida kwa wenzi wa ndoa kukosana, nyakati nyingine kutalikiana, na hata mahusiano mengine ya karibu huharibika kwa sababu hiyo.”
USIKOSE SEHEMU YA SITA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA TATU)

No automatic alt text available.
Mapingamizi Tisa ya Kiislam na Maitikio Yake
Pingamizi la 1 la Waislam: Watu wengine mbali ya hawa kumi na moja hawajaziongelea aya za Shetani. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislam ambao hawakundika kuhusu aya za Shetani walkuwa Imam Muslim aliyeandika Sahih Muslim, Abu Dawud, Nas’ai, Ahmad bin Hanbal, and ibn Hisham.
Itikio: Kuna vitu vingi kwenye makusaniko ya Hadithi ambavyo havimo kwenye mikusanyiko mingine. Kwa mfano, Hadithi ndefu za Bukhari hazina mafundisho kuhuu sababu za kutoa zaka, adhabu ya kujilimbikizia vitu, na malaika wawili wanao mtembelea Muislam kila asubuhi kama yanavyopatikana kwenye Sahih Muslim juzuu ya 2 sura ya 371 na.2205, uk.484. Kama mfano wa pili, tunajua kuwa Ibn Hisham aliitumia Bukhari, lakini aliiacha sehemu inayohusu aya za Shetani. Kwenye nakala ya Ibn Hisham ya Ibn Ishaq, alisema aliondoa vitu alivyoona kuwa vibaya. Kama alijisikia aibu sana hata hakuweza kuziweka, huo sio uthibitisho kuwa hazikutokea.
Pingamizi la 2 la Waislam: Aya zinazodaiwa kuwa za Shetani haziendani sawa na sehemu nyingine ya Sura 53.
Itikio: Kumbuka kuwa sehemu ya sasa haikufuatia aya za Shetani, bali ilichukua nafasi zao. Pia nyakati zingine sehemu tofauti za Sura moja zilitolewa nyakati tofauti. Upande mmmoja, al-Wahidi alisema Muhammad alisema hadi maneno ya mwisho. Kwa upande mwingine, hatujui kuwa Sura yote ya Nyota (53) baada ya aya ya 22 iliandikwa wakati mmoja. Aya za 51-53 zinaonekana kuwa hazipo mahali ake kwani zinamongelea Muhammad mwenyewe.
Pingamizi la 3 la Waislam: Sura 53:19-21 inaweza kuwa ilikuwa mapema zaidi kuliko Sura zinazoongelea kunong’ona kwa Shetani.
Itikio: Tabari na ibn Sa’ad wanasema zilifunuliwa wakati mmoja na Sura 17:73-75. Hakuna mtu leo hii anayejua kwa uhakika wakati ambapo aya nyingi za Kurani ziliandikwa. Kwa upande mwingine, hata kama iliandikwa mapema haitaweza kukanusha maneno iliyoyasema. Kama Waislam wasahilina wanaiamini kabisa Kurani, ikiwa ni pamoja na Sura 17:73-75 na 22:52, watatakiwa kuamini kwamba Shetani anaongeza vitu kwenye Kurani. John Gilchrist, kwenye Muhammed and the Religion of Islam uk.120 anasema, "Hoja nyingine ni dhaifu kwa sababu hakuna ushahidi thabiti kuwa sehemu ya kwanza ya Surah 53 inaongelea miraj [kupaa kwa Muhammad] kulikotokea baada ya kuhamia Abyssinia. Kama ilivyokwishaonyeshwa, kuna uhakika wa kiasi kikubwa sana kuwa inaongelea moja ya ziara za mwanzo za Muhammad, ambazo Kurani yenyewe inaonyesha kuwa hazizidi mbili ambazo alizifanya wakati huduma yake ilipoanza. Kwa bahati mbaya inaonekana kuwa hoja zote za Waislam za uhalisi wa vipingamizi vya habari hii ni dhaifu."
Pingamizi la 4 la Waislam: Aya za Shetani zinapingana na mafundisho ya msingi kuwa kuna Mungu mmoja ambayo Muhammad alishikilia kufundisha.
Itikio: Muhammad hajawahi kuthibitishwa kushikilia kitu chochote kile. Kumbuka, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 10 na.490, uk.317; juzuu ya 4 kitabu cha 53 sura ya 38 kabla ya na.400, uk.266; juzuu ya 8 kitabu cha 53 sura ya 38 na.400, uk.267 inarekodi kuwa Muhammad alikuwa amerogwa na mwovu kwa kipindi fulani. Isitoshe waandishi wa maisha yake na watu wengine waliorekodi jambo hili walikuwa bado Waislam, kwa hiyo wana historia hawa wanathibitisha kuwa kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa tayari kumfuata Muhammad hata kama alisema uongo.
Pingamizi la 5 la Waislam: Vifungu vingi kwenye Kurani vinasema Muhammad hakuweza kusema maneno yoyote yasiyokuwa kweli, na kwa ajili hiyo jambo hili haliendani na tafsiri kuwa Shetani anaingilia mambo. Kwa mfano,
Sura 10:15b: "Sema; Si kwa ajili yangu, kwa hiari yangu, kubadilisha hili: Sifuati kitu chochote isipokuwa kile kilichofunuliwa kwangu…"
Sura 41:42: "Hakuna uongo unaoweza kulikaribia kutokea mbele au nyuma yake: Limetumwa na Yeye Aliyejaa Hekima na Mwenye Kustahili Sifa zote."
Sura 15:9: "Tumeutuma, bila shaka, Ujumbe; na tutaulinda kwa hakika (dhidi ya uharibifu)."
Sura 60:44-46: "Kama (Mjumbe) angetunga neno lolote kwa jina letu, Tungemkamata kwa mkono wa kulia na kisha tungeikata ateri ya moyo wake"
Itikio: Kwa upande mmoja, inadaiwa kuwa Shetani, siyo Muhammad, alitunga aya za Shetani, na kulindwa kwa Kurani haukanushi kuingia kwa mafundhisho ya uongo na Mungu kuyarekebisha. Kwa upande mwingine, kama Muislam anatafsiri aya hizi kuwa zinafundisha kwamba hakuna kitu cha uongo kitakachoweza kuingia ujumbe wa nabii, hata kama aya za Shetani hazitahusishwa, jambo hili litakuwa kinyume na kunong’oneza kwa Shetani ambako kumeelezwa kwenye Kurani.
USIKOSE SEHEMU YA NNE
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

SIRI YA KUJIBIWA MAOMBI

Image may contain: one or more people, ocean, sky, cloud, text, outdoor, water and nature
Yohana 15: 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Tukitaka kuona matokeo makubwa zaidi ya maombi yetu, hatuna budi kukaa ndani ya Kristo, yaani kuokolewa na kuwa viumbe vipya (2 WAKORINTHO 5:17). Siyo hilo tu, maneno yake hayana budi kukaa ndani yetu kwa WINGI (WAKOLOSAI 3:16). Neno la Mungu litatuwezesha kuifahamu KWELI yenye uwezo wa kutuweka huru mbali na uongo wa Shetani.
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

UISLAM NI DINI YA KUTUNGA NA HAIKUWEPO KABLA YA MUHAMMAD




Hakuna mwanadamu ye yote kabla ya ujio wa Muhammad, ambaye aliwahi kuwa Muislamu, wala aliyewahi kuujua Uislamu, kama kuna Muislamu ambaye anaweza kunithibitishia kuwa, kuna mtu aliyewahi kuwa Muislamu, kabla ya Quran kuwepo, basi nitasilimu na kuwa Muislam:-
Angalizo :- Unapotoa ushahidi usitumie Quran, wala kitabu cho chote ambacho kimepatikana baada ya kuja Muhammad, bali nahitaji ushahidi katika vitabu vilivyokuwepo kabla ya Muhammad kuja na Quran, na usichukue matukio ambayo Muhammad ameyaiga kutoka kwa watu wa zamani, kama
a) Kutawadha. 
b) kusujudu 
c) Kuvaa kanzu
d) Nk.
Na kusema huo ndo uislamu, bali ukisema hivyo, basi uambatanishe na ushahidi kimaandiko, kutoka kwenye vitabu nje ya Quran, iliyokuja mwaka 610 baada ya Kristo, maandiko yasemavyo kuwa kusujudu, kuvaa kanzu, kutawadha ni uislamu, yakipatikana basi leo hii nitasilimu na kuwa muislamu!
ZINGATIA :- kama hautapata ushahidi wa uwepo uislamu au neno Uislamu (الإسلام) kwenye vitabu vilivyokuwepo kabla ya Quran, basi tambua kuwa umeongopewa kuwa, Uislamu upo tangu zamani za Adamu, maana haiwezekani, watu kama,
Adamu
Habil
Nuhu 
Ibrahimu 
Lutu 
Sara 
Ishamael - Ismail
Isaka - Is-haqa
Yakobo Yaqubu 
Yusufu
Yunusi -Yona
Musa 
Haruni 
Daudi 
Suleiman 
Eliya - Ilyasa 
Zakaria 
Yahya - Yohana
Yesu,
Wasijitambue kuwa wao walikuwa waislamu, mpaka waje kusemewa na Muhammad, mwaka wa 610. Zinduka, ujue kuwa Uislam ni dini bandia na haukuwepo kabla ya Muhammad.
#courtesy of aliyekuwa Ustadh Abel Suleiman Shiliwa ambaye sasa ni Mtumishi wa BWANA Yesu.
For Max Shimba Ministries Org

PASIPO YESU SISI HATUWEZI KUFANYA NENO LOLOTE

Image may contain: one or more people and text
Yohana 15: 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Ni muhimu wakati wote kukumbuka kwamba utoshelevu wetu watoka kwa Yesu (2 WAKORINTHO 3:5). Sisi ni matawi. Matawi yasipopata chakula na maji kutoka kwenye mizizi, hunyauka na kufa. Uwezo wetu wa kufanya neno lolote, unatoka kwa Yesu aliye mizizi. Bila yeye hatuwezi kufanya neno lolote. Hapa neno halisemi bila Yeye hatuwezi kufanya NENO LOLOTE KUBWA, kama kufufua watu, kuponya walio na Ukimwi n.k., neno linasema hatuwezi kufanya neno lolote hata lililo dogo. Katika yote, WAKATI WOTE, hatuna budi kuitumainia NEEMA ya Mungu na kamwe tusijitumainie wenyewe HATUWEZI! (2 WAKORINTHO 1:8-9; 12:9).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

MUHAMMAD ALIPAGAWA NA KUWEWESEKA BAADA YA KUONA KUPATWA KWA JUA

No automatic alt text available.
Sahih Bukhar Volume II Kitabu namba 18 Namba 167. Nabii Muhammad alipagawa na kuweweseka baada ya kuona kupatwa kwa jua. Muhammad alifikiria kuwa kiyama kimefika na ameachwa na Allah. ALikimbia mpka msikitini na kuomba msamaha kwa Allah mara mia moja.
Eti huyu ndio alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, THUBUTU.
Ndio maana Muhammad aliukana utume wake:
SOMA HAPA:
MUHAMAMD ANAOMBWA AFANYE MIUJIZA ILI KUTHIBITISHA UTUME WAKE:
Surat Al Israai 90. Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii
MUHAMMAD ANAJIBU KUWA YEYE SI CHOCHOTE YULE
Surat Al Israal 93. Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na mtumwa tu?
Muhammad hakuwai fanya muuiza wowote ule, hakuponya watu, hakufufua wafu, hakutoa majini zaidi ya kuwaingiza watu majini. Muhammad alikuwa dhaifu.
Kama Muhammad alifikiria kuwa, kupatwa kwa jua ni KIYAMA, kwanini tumfuate mtu wa namna hii aliye ogopa kuachwa na Allah siku ya kiyama?
Kumbe Muhammad hakuwa na uhakika kwa kwenda Akhera.
Qur’an 46;9 (Surat Al-Ahqaf) Sema; mimi si kiroja (mpya) katika mitume wala sijui nitakavyofanywa, wala mtakavyofanywa ninyi, sifuati yaliyofunuliwa kwangu, sikuwa mie lolote, ila ni muonyaji tu ninayedhihirisha.
Eti tuufuate Uislamu chini ya kiongozi Muhammad ambaye hajui hatima yake kama ataenda peponi, au ataenda motoni, bila shaka kwa Mkristo anayejitambua hawezi kuwa Muislamu.
Hakika Muhammad alikuwa Mtume Bandia na Allah ni Mpinga Mungu.
Karibuni kwa Yesu aliye hai,
Shalom,
Max Shimba ntumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA SITA)

Image may contain: one or more people and text
Jinsi Vijana wanavyoathiriwa na picha za utupu:
Takwimu zinaonyesha kwamba watazamaji wengi wa ponografia ni wavulana wenye umri wa kati ya miaka 12 na 17. Kwa kweli, wengi wao hujifunza masuala ya ngono hasa kupitia ponografia. Hilo lina matokeo mabaya sana. Ripoti moja yasema kwamba “ponografia hazionyeshi kamwe mimba za matineja na magonjwa yanayoambukizwa kingono kama UKIMWI, na hilo hutokeza wazo la uwongo la kwamba mambo yanayoonyeshwa katika ponografia hayana madhara.”
Watafiti fulani husema kwamba kutazama ponografia kunaweza pia kuathiri ukuzi wa kawaida wa ubongo wa mtoto. Dakt. Judith Reisman, mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Vyombo vya Habari, akata kauli: “Uchunguzi wa athari za sauti na picha za ponografia katika utendaji wa kawaida wa ubongo unaonyesha kwamba kutazama ponografia huathiri kabisa uwezo wa kawaida wa kufikiri. Pia hudhuru ubongo wa watoto unaoathiriwa kwa urahisi kwa sababu hufanya wasione mambo kihalisi na hudhuru afya yao ya kiakili na ya kimwili, na huwazuia kupata furaha.”
Jinsi Mahusiano yanavyoathiriwa na unagaliaji wa ponografia:
Ponografia huathiri mitazamo na tabia. Ujumbe wake unavutia hasa kwa sababu si halisi na hivyo unaifanya ionekane kuwa yenye kusisimua zaidi kuliko mambo halisi. (Ona sanduku “Utakubali Ujumbe Gani?”) “Watu wanaotazama ponografia hutarajia mambo yasiyo halisi ambayo huharibu mahusiano,” yasema ripoti moja.
Ponografia inaweza kuwafanya wenzi wa ndoa wakose kuwa wanyofu na wakose kuaminiana, sifa ambazo ni muhimu katika ndoa. Kwa sababu ponografia hutazamwa hasa faraghani, mara nyingi humfanya mtu atumie hila na uwongo. Wenzi wa ndoa huhisi kwamba wamesalitiwa. Hawaelewi kwa nini mwenzi wao havutiwi nao tena.
USIKOSE SEHEMU YA SABA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA NNE)

No automatic alt text available.
Pia, hii si mara pekee aya ya Kurani "inapotea kabisa" kwa sababu ilibatilishwa. Sahih Muslim juzuu ya 1 sura ya 244 na.1433, uk.329-330 ni Hadithi muhimu kwa sababu inaonyesha kuwa aya ilibatilishwa, bali baada ya kubatilishwa ilipotea kabisa. Hivyo ama:
a) Kurani kwenye mbao zenye maandishi [mbinguni] ilikuwa na toleo la awali, na toleo lililofuata lilitofautiana na mbao hizo. Kurani ya leo inatofautiana na mbao zenye maandishi za mbinguni.
b) Kurani kwenye mbao zenye maandishi za mbinguni zina toleo la baadaye, na toleo la awali linatofautiana nalo. Kwa hiyo maneno ya kwanza yalitolewa kama kiwakilishi cha mbao zenye maandishi za mbinguni wakati ukweli ni kwamba ilikuwa ni uongo.
Kipi ni kipi? Mbao za maandishi [mbinguni] kwenye Sura 85:20-22 hazidhaniwi kutengenezwa kwa puti ya kipumbavu.
Pingamizi la 6 la Waislam: Tabari anawezakuwa hakukusanya habari kiuhakiki.
Itikio: Ingawa hatuna ushahidi wa mada haya, waandishi wengine watatu wa maisha [ya Muhammad] pia waliandika jambo hili. Wawili kati yao waliandika kabla ya Tabari, kwa hiyo hata kama Tabari alionekana kutokuwa mhakiki, jambo hilo haliwezi kuathiri kitu chochote kwa kiasi kukubwa kwani bado tuna watu wengine watatu. Muislam anaweza kupenda kuona kuwa waandishi wote wa maisha ya Muhammad wanaonekana kuwa na dosari sana, lakini vyanzo mbalimbali vinaonyesha usahihi wao.
Pamoja na hayo, Tabari hakupokea vitu vyote bila kuvihakiki. Kwa mfano, kwenye juzuu ya 1, uk.532 anasimulia tamaduni nyingi za kiislam za Adam na Hawa alizojifunza kutoka kwa watu wenye Torati. Anazinukuu nyingi zake lakini anasema kuwa ana mashaka na uhakika wa hizi Hadithi. (Kutoka kwenye kitabu cha Barbara Freye Stowasser kiitwacho Woman in the Qur’an, Tradition, and Their Interpretation uk.28).
Pingamizi la 7 la Waislam wa Madhehebu ya Suni: Hadithi zenye uhakika hazilisemi jambo hili moja kwa moja.
Itikio: Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 19 sura ya 42 na.173, uk.100; juzuu ya 3 kitabu cha 19 sura ya 43 na.176, uk.101; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 286-287 na.385-386, uk.364-365; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 481 na.1401, uk.369 zinaeleza hali waliokuwa nayo watu wa Maka walipokuwa wanasujudu waliposikia Sura 53. Ni vigumu kueleza tofauti kitu kilichokuwepo kuhusiana na sura hii kilichowafanya wapagani wasujudu kwa ajili ya sura hii, ikiwa hawakusujudu kwa ajili ya kitu kingine. Kurani yenyewe pia inasema kuhusu "kunong’oneza" kwa Shetani.
Pingamizi la 8 la Waislam wa madhehebu ya Suni: Shaykh al-Albani, kwenye vitabu vyake vinavyohusu mtiririko wa waenezaji wa tamaduni, alisema ushahidi wa aya za Shetani una mlolongo mbaya wa ueneaji (isnad).
Itikio: http://answering-islam.org/Responses/ Saifullah/sverses.htm inasema, "Kuhusu al-Albani, nimefahamishwa kuwa siku hizi al-Albani ameelezwa vibaya sana kwa kutokuwa sahihi kuhusu isnads, hata anaandika kwenye kitabu kimoja kuwa mtu fulani ni mkweli lakini kwenye kingine anasema kwamba jambo hilo si sahihi! Kitabu kiitwacho Al-Albani Unveiled kilichoandikwa na Sayf ad-Din Ahmed Ibn Muhammad Amirul Islam kinatoa mifano mingi sana. Upande wa nyuma unasema: Kitabu hiki ni uchunguzi mchanganifu wa mmoja wa mashehe muhimu zaidi wa Hadithi(Muhammad Nasiruddeen al-Albani) wa harakati ya kisasa ya kiislam inayojulikana kama ‘Salafiya’. Mtunzi ameeleza wazi kabisa kupingana kwa Al-Albani kwa kutumia msaada wa kazi iliyoandikwa kwanza kwa Kiarabu (Tanaqadat al-Albani al-Wadihat), na mwanazuoni wa wa Hadithi wa Kijordani anayejulikana sana - Shakh Hasan ibn Ali al-Saqqaf."
Pingamizi la 9 la Waislam: Watu wasio Waislam wanampinga Muhammad na uislam.
Itikio: Tukio hili halikuundwa na watu wasiokuwa Waislam, bali liliandikwa na Waislam wenyewe. Waislam hawa wasahilina walikuwa na vyanzo vya zamani zaidi kuliko Waislam wa sasa. Kulifumbia macho jambo linalokosoa mtazamo wako kwa sababu tu linakosoa maoni yako, hakuendani na kuufuata ukweli. Kwa kuwa Wakristo wanadai kufundisha ukweli, tunao wajibu wa kumtaja nabii wa uongo. Hatufanyi hivi kwa sababu ya chuki au matakwa binafsi, bali kwa sababu ya upendo na haja ya kuwaona Waislam wanaepukana na mafundisho ya uongo, na kumgeukia Yesu wa kweli na kuwa nasi mbinguni pamoja na Mungu wa kweli.
Unakwenda wapi kutoka hapa?
Waislam wenyewe hawajakubaliana endapo maneno ya Shetani yalikuwemo kwenye Kurani mwanzoni.
Chaguo la 1: Itakuwa vipi endapo Muhammad aliongea kama nabii kuhusu maombezi ya mabinti wa Allah? Jambo hili litamfanya Muhammad kuwa nabii wa uongo kwa kipindi fulani.
Chaguo la 2: Itakuwa vipi endapo Muhammad hakuwahi kusema aya za Shetani? Waandishi wote wanne wa maisha ya Muhammad watakuwa wamekubaliana kukosea kuwa Muhammad alikuwa nabii wa uongo. Baadhi ya watu watachagua, kwa hiari yao wenyewe, kufuata kitu hata kama wanaamini kuwa kiongozi wao aliongea mambo ya Shetani. Hata kama jambo hili ni kweli, utafanya nini na aya za Kurani zinazohusu minong’ono ya Shetani ambayo Muhammad aliipata?
Kwa vyovyote vile, uislam unafundisha kuwa Allah anaruhusu maneno yake yabadilishwe kiasi kikubwa sana, na Allah anaruhusu wafuasi wake wazuri wajifunze njia za uongo kama njia ya ukweli. Hii ni kwa sababu Kurani kwenye Sura 43:44-45, inaonyesha kuwa manabii wote waliotangulia walikuwa na ujumbe mmoja. Sura 41:43 inasema kwamba hakuna kitu kilichotumwa kwa Muhammad ambacho hakikuwahi kutumwa kwa manabii waliomtangulia pia. Kwa hiyo kwa Waislam, ama
a) Allah aliruhusu ujumbe wake uliopotoshwa hapo awali,
b) Au, Kurani ndio ujumbe uliopotoka.
Kwa vyovyote vile, uislam unasema, Allah hawezi kutumainiwa kulitunza neno lake dhidi ya mabadiliko makubwa ya mafundisho.
Mwamini Mungu
Mungu Mwenye nguvu anao uwezo wa kuutunza ujumbe wake. Watu wanatakiwa kumwamini Mungu zaidi.
Mwamini Mungu kuwa amelitunza neno lake. Sura 5:46-48 inasema kwamba Yesu aliithibitisha Torati (kwa wakati wake), Mungu alituma Maandiko kwa Wayahudi na Wakristo, na hata wakati wa uhai wa Muhammad wangeweza kuupima ukweli kwa kuyatumia [Maandiko]. Sura 3:48 na 5:110-111 zinamwonyesha Yesu kuwa alikuwa na Torati na Injili. Wanafunzi wa Yesu pia walikuwa wamevuviwa. Kwenye Biblia, Isaya 59:21; 40:8; Zab. 119:89 zinaonyesha kuwa neno la Mungu hudumu milele. Neno lake halikuwa na kosa lolote hapo awali, na limetunzwa bila makosa (bila makosa makubwa) hadi leo hii. (Isa. 55:11; 1 Petro 1:23-25; Zaburi 119:89, 91, 144, 160).
Tumaini kuwa Mungu anataka uufuate ukweli na uje kwake. Mungu hataki mtu yoyote aangamie (Ezekiel 18:23, 32; 2 Petro 3:9). Watu wote wanatakiwa kuiamini Injili ya Yesu Kristo kwenye 2 Wathesalonike 1:8.
Usimtumaini mwanadamu ambaye maisha yake yana ukomo. Usiwatumaini watu wengine ambao wanakugeuzia mbali na Mungu. "Usiwe mwenye hekima machoni pako (Mithali 3:7). Badala yake, "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako" (Mithali 3:5-6). Je unaamini kuwa Mungu anaweza kunyoosha njia zako kama ukimkiri?
Mtumaini Yesu; Yeye ametoka kwa Mungu na ujumbe wa Mungu umetunzwa. Yesu si mwizi wala mnyang’anyi (Yohana 10:8-10). Amini kuwa Yesu alitoa uhai wake kama fidia ya ukombozi (Mathayo 20:28), ili iwe sadaka ya dhambi (Warumi 8:3), kwa njia ya damu yake aliyoimwaga msalabani (Waeb. 10:19).
Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa (Matendo 16:31). "… ‘Kila amwaminiye hatatahayarika’" (Warumi 10:11). Kwa hiyo mtumaini Mungu, na amini kuwa anaongoza kwa uaminifu. Hakuacha neno lake lipotoshwe, kwa hiyo Biblia inaaminika. Mpe Yesu maisha yako, na atakupa amani na furaha.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW