Friday, July 14, 2017

YEYE ASIYE NA DHAMBI NA AWE WA KWANZA KUKUTUPIA JIWE


Image may contain: 1 person, sitting and text

“Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. ”
Bwana Yesu asifiwe…( Yohana 8:7 )
Kwa lugha nyingine Bwana Yesu anawaambia ikiwa kama watu hao hawana dhambi basi wawe wa kwanza kumuhukumu huyo mwanamke. Anawaambia watesi wako siku ya leo kwamba ikiwa kama hawana makosa basi wawe wa kwanza kukuhukumu wewe.
Ndiposa nikajifunza jambo moja kubwa hapo, kwamba;
Hata wenye kukuhukumu wewe,kumbe wao pia wanadhambi za kuhukumiwa, hivyo hawastahili kukuhukumu,pia nikajua kwamba; Usalama wako haupo kwa wanadamu bali usalama wako upo magotini pa Yesu.
TUACHE KUHUKUMU KAMA VILE SISI NI MALAIKA HUKU TUKIFAHAMU KUWA WOTE SISI NI WATENDA DHAMBI NA TUNASTAHILI JEHANNAM.
Waacheni hao Watoto wenye watoto WAENDE SHULE.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW